13/01/2026
SHUKRANI NA OMBI LA RADHI
Kwa niaba ya familia na uongozi kwa ujumla, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa wote walioweza kushiriki kwa namna moja au nyingine katika safari ya mwisho ya ndugu yetu mpendwa, Elibariki Shedrack Mashauri (SAMBAA).
Ushirikiano, upendo, muda, michango na faraja mlizoonesha ni ishara ya mshikamano wa kweli katika kipindi hiki kigumu.
Pia, tunaomba radhi kwa unyenyekevu mkubwa endapo kulikuwa na changamoto au sehemu zozote tulikwazana katika jitihada za kuhakikisha mambo yanaenda sawa. Yote yalifanyika kwa nia njema na kwa lengo la kumpa ndugu yetu heshima ya mwisho.
Shukrani za kipekee ziende kwa Kampuni ya BANKIMOON kwa moyo wao wa kipekee na ushirikiano mkubwa.
Aidha, tunatoa shukrani kwa Umoja wa Madereva Arusha, Umoja wa Noah Karatu, pamoja na wote wengine ambao waliguswa na kushiriki kwa namna yoyote.
Mungu awabariki sana kwa moyo wenu wa upendo na mshikamano.
Pumzika kwa amani SAMBAA.