CROWN FM/TV MEDIA

CROWN FM/TV MEDIA media/news/entertainment

Calculator za wananchi zinademaje huko?
19/01/2025

Calculator za wananchi zinademaje huko?

Man city kafungwaArsenal kafungwaLiverpool kafungwa Yanga kafungwaTimu kubwa zote leo zimepoteza🥹🥹🥹 Faraja ni kubwa😁😁😁
03/11/2024

Man city kafungwa
Arsenal kafungwa
Liverpool kafungwa
Yanga kafungwa
Timu kubwa zote leo zimepoteza
🥹🥹🥹
Faraja ni kubwa
😁😁😁

16/09/2024
Cv ya Leonel Ateba Mshambuliaji Mpya wa Simba 2024/2025 | Straika Mpya wa Simba 2024/2025Klabu ya Simba Sc imekamilisha ...
15/08/2024

Cv ya Leonel Ateba Mshambuliaji Mpya wa Simba 2024/2025 | Straika Mpya wa Simba 2024/2025

Klabu ya Simba Sc imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Lionel Ateba kwa mkataba wa miaka miwili kwa ada inayodaiwa kuwa dola laki mbili (Tsh 542,000,000). Ateba (25) raia wa Cameroon alijiunga na USM Alger mnamo Januari, 2024 kwa dau la dola laki tatu akitokea Dynamo Douala ya nyumbani kwao Cameroon akiifungia USM Algers bao MOJA tu na ‘assist’ 8 kwenye mechi 16.

Cv ya Leonel Ateba Mshambuliaji Mpya wa Simba 2024/2025
Leonel Ateba, anayejulikana kwa jina kamili Christian Leonel Ateba Mbida, ni mchezaji wa kimataifa mwenye uraia wa Cameroon ambaye amejiunga na klabu ya Simba SC kwa msimu wa 2024/2025. Alizaliwa tarehe 6 Februari 1999, na kwa sasa ana umri wa miaka 25. Akiwa na urefu wa mita 1.83, Ateba ni mshambuliaji wa kati (Centre-Forward) ambaye pia ana uwezo wa kucheza k**a winga wa kushoto na kulia. Hii inamfanya kuwa mchezaji wa kipekee mwenye uwezo wa kushambulia kutoka pande zote za uwanja.

Wataleta timu kweli🤔🤔
11/07/2024

Wataleta timu kweli🤔🤔

Simba itakutana na mshindi wa mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Uhamiaji Fc ya Zanzi...
11/07/2024

Simba itakutana na mshindi wa mchezo wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Uhamiaji Fc ya Zanzibar dhidi ya Mshindi wa kombe la Shirikisho la Libya ambaye ataoatikana baadae.

Coastal Union wao watakutana na FC Bravos ya Angola katika hatua hiyo ya awali na mshindi wa jumla atakutana na FC Lupopo ya Congo DR katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho barani Afrika

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga watapambana na Vitalo ya Burundi kwenye hatua ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrik...
11/07/2024

Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga watapambana na Vitalo ya Burundi kwenye hatua ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.K**a Yanga wataitoa Vitalo ya Burundi watacheza na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia huku Azam FC wamepangwa kucheza na APR ya Rwanda kwenye hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
K**a Azam FC wataitoa APR basi watapambana na mshindi kati ya JKU ya Zanzibar dhidi ya Pyramids FC ya Misri anayochezea nyota wa zamani wa Yanga Fiston Mayele

Rais William Ruto amelivunja baraza lake la mawaziri isipokuwa kwa nafasi ya Kiongozi wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya ...
11/07/2024

Rais William Ruto amelivunja baraza lake la mawaziri isipokuwa kwa nafasi ya Kiongozi wa mawaziri na Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi.

Uamuzi huo wa Rais Ruto ameutangaza leo, Alhamisi Julai 11, 2024 nchini Kenya akisema mabadiliko hayo yatasaidia kuunda serikali itakayosaidia kuongoza kasi ya utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na changamoto nyingi zinazowakabili wananchi.

Katika hotuba yake hiyo iliyopokelewa kwa shangwe na wananchi wa Kenya hususan vijana maarufu (GEN Z), Ruto amesema, licha ya kuvunja baraza hilo nafasi ya Naibu wa rais haijaathiriwa na mabadiliko hayo pia.

Uamuzi huo alioutangaza Rais Ruto unahusishwa moja kwa moja na maandamano ya vijana wa Kenya waliokuwa wakipinga Muswada wa Sheria wa Bajeti Kuu ya Nchi hiyo ambao ulilalamikiwa kwakuwepo na ongezeko kubwa la kodi litakalomuumiza mwananchi wa kawaida na hivyo Rais Ruto kukataa kuusaini na kuurejesha muswada huo bungeni.

Hata hivyo Rais Ruto amesema itamchukua muda kufanya majadiliano ya kuunda baraza jipya la mawaziri litakalohusika na uendeshaji wa serikali suala lililopokelewa na maoni mseto kutoka kwa wananchi.

Rais Ruto amesema baraza hilo litaangalia namna ya kusaidia kuongeza ufanisi na kasi ya kukabiliana na mzigo wa madeni, kuongeza rasilimali za ndani, kupanua nafasi za kazi, kuondoa ubadhirifu wa fedha, kupunguza gharama na matumizi makubwa ya serikali na kukomesha ufisadi wa fedha za umma.

Address

Arusha

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when CROWN FM/TV MEDIA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share