Online Marketing System Pro

Online Marketing System Pro Ninawasaidia Wafanyabiashara njia rahisi ya kutumia matangazo ya kulipia kunasa wateja mtandaoni!

Anza sasa kujifunza kuuza!
20/10/2023

Anza sasa kujifunza kuuza!

Usikate tamaa mapema ukahisi unachokifanya hakizai matunda. Jipe muda na uwe mvumilivu wakati wako utafika.
19/09/2023

Usikate tamaa mapema ukahisi unachokifanya hakizai matunda.

Jipe muda na uwe mvumilivu wakati wako utafika.

Njia ya mafanikio sio moja.K**a unavyoweza kuona kwenye picha kuna njia nyingi sana za kuweza kukufikisha kwenye 10. Kwa...
14/09/2023

Njia ya mafanikio sio moja.

K**a unavyoweza kuona kwenye picha kuna njia nyingi sana za kuweza kukufikisha kwenye 10.

Kwahiyo k**a bado hujapata njia ya kukufikisha unapotaka kufika endelea kuitafuta kwa maana sote hatuwezi kutumia njia moja.

Cha msingi ni kufikia lengo hata k**a hujatumia njia ambayo imetumiwa na wengine.

Hatua ya kwanza: k**a huna page ya biashara Facebook tengeneza. Hakikisha jina la page yako linabeba BRAND yako. Page ni...
13/09/2023

Hatua ya kwanza: k**a huna page ya biashara Facebook tengeneza. Hakikisha jina la page yako linabeba BRAND yako.

Page ni k**a kipeperusha tangazo lako mtandaoni. Bila page huwezi ukarusha tangazo Facebook. Lakini ukiwa na page Facebook unaweza kurusha tangazo likaonekana Facebook na Instagram hata k**a huna account instagram.

Hatua ya pili: K**a account yako ya Instagram ni ya kawaida (personal) ibadili kuwa business account.

Hatua ya tatu: unganisha page yako ya Facebook na account yako ya Instagram.

Ukifanya hivyo itakusaidia kurusha tangazo moja kupitia ads manager ambalo kwa bajeti moja litaonekana kote Facebook Na Instagram.

Hatua ya nne: Fungua ads manager. Hii ni account maalumu kwa ajili ya kurusha matangazo ya kulipia.

Hatua ya tano: Andaa tangazo. Tangazo linaweza kuwa la video na caption au caption na picha.

Hatua ya sita: Kupitia ads manager yako rusha tangazo lako.

K**a ungependa kujifunza hatua zote 6 kwenye video bonyeza iliyopo kwenye comment ya kwanza hapa chini

Sababu moja kubwa kwanini wafanyabiashara hawafanikiwi mtandaoni ni kukosa malengo na mpango mkakati. Nimekutana na wafa...
11/09/2023

Sababu moja kubwa kwanini wafanyabiashara hawafanikiwi mtandaoni ni kukosa malengo na mpango mkakati.

Nimekutana na wafanyabiashara wengi ambao wanahitaji kupata wateja mtandaoni.

Swali langu la kwanza kwao hua ni hili: unahitaji wateja wangapi kila mwezi kufikisha lengo lako?

Jibu lao huwa ni: WATEJA WENGI.

Unaona?? Wateja wengi ndo nini?? Wingi unaanzia 2 kwahiyo hata wateja 2 ni wengi.

Huwez ukapata kitu ambacho hukitafuti. Lazima ujue unataka nini halafu ndo uweke mpango mkakati wa kukitafuta hicho unachokitaka.

Labda tuseme una lengo la kutengeneza faida ya 1,000,000 kwa mwezi.

Hatua ya kwanza lazima ujue ni wateja wangapi unahitaji kuweza kutengeneza hiyo faida.

Hatua ya pili ni kuweka mpango mkakati wa kuwapata hao wateja idadi ya kukufanya ufikishe faida ya lengo lako.

Sasa utakuta mtu hana lengo na hana mpango mkakati halafu analalamika kwanini biashara yake haikui.

Itakuaje wakati hujui unachokitafuta ni nini.

Weka malengo na mpango mkakati wa kuyatimiza hayo malengo halafu rudi uniambie matokeo yake.

Utajishukuru mwenyewe kwa kufanya hivyo.

Mambo hayatokeagi tu k**a miujiza. Lazima mahesabu yafanyike.

Easy weekend Homies!
10/09/2023

Easy weekend Homies!

Furaha ya maisha ipo kwenye kushukuru yale ambayo tayari tumejaliwa. Hayo ambayo hatujayapata yasiwe ndio kipimo cha fur...
07/09/2023

Furaha ya maisha ipo kwenye kushukuru yale ambayo tayari tumejaliwa.

Hayo ambayo hatujayapata yasiwe ndio kipimo cha furaha yetu kwa maana hatujui ni muda gani tutayapata hivyo tukisema tuyasubirie ndo tufurahi tunaweza kujikuta maisha yetu yanajawa na simanzi na msongo wa mawazo na wakati tunazo baraka na neema nyingi zinazotuzunguka tayari.

Kitendo cha kuwa na afya njema itoshe kukufanya ushukuru maana hiyo ni ishara kwamba bado unayo nafasi ya kuweka mambo sawa!

1. Copywriting.Hii ni sanaa na sayansi ya kuandika maneno yenye uwezo wa kumshawishi mtu kufanya unachokitaka wewe.Ujuzi...
06/09/2023

1. Copywriting.

Hii ni sanaa na sayansi ya kuandika maneno yenye uwezo wa kumshawishi mtu kufanya unachokitaka wewe.

Ujuzi huu utakusaidia kuandika tangazo zuri lenye mvuto na ushawishi kwa wateja.

2. Media buying know how

Hii inamaanisha kujua kurusha matangazo ya kulipia Facebook Na Instagram.

Matangazo ya kulipia ni njia ya haraka ya kupata wateja kwahiyo ukijua kuyarusha vizuri, biashara yako lazima ifanikiwe.

3. Closing skills

Huu ni uwezo wa kumshawishi mtu mwenye uhitaji wa bidhaa yako kuwa mteja.

Usipokuwa na ujuzi huu utajikuta unatafutwa na watu wengi wenye uhitaji wa bidhaa yako lakini wachache ndo wananunua.

Umejifunza nini kwenye post hii? Share na mimi kwenye comment hapa chini.

Binadamu tuna tabia ya kuchukulia poa vitu tunavyovipata kirahisi. Na vitu ambavyo tunapitia magumu kuvipata tunavithami...
05/09/2023

Binadamu tuna tabia ya kuchukulia poa vitu tunavyovipata kirahisi.

Na vitu ambavyo tunapitia magumu kuvipata tunavithamini sana.

Ndio maana maisha yakawa magumu ili tuthamini vitu tunavyovipata kwa shida!

Biashara nyingi zinakufa kwasababu waanzilishi wanasahau msingi wa biashara yoyote kukua. Ili biashara ikue lazima kuwep...
02/09/2023

Biashara nyingi zinakufa kwasababu waanzilishi wanasahau msingi wa biashara yoyote kukua.

Ili biashara ikue lazima kuwepo na soko lenye uhitaji wa bidhaa husika.

Soko hili na uhitaji wa bidhaa husika havitengenezwi.

Utakuta mfanyabiashara unaleta bidhaa sokoni pasipo kufanya utafiti wa soko lako kuwa na uhitaji wa bidhaa yako.

Matokeo yake unaleta bidhaa ambayo soko halina uhitaji nayo.

Akili ya kawaida inakutuma kwamba utawashawishi watu wanunue bidhaa yako.

Hiyo ni ndoto ya mchana kweupe.

Bidhaa itakudodea.

Kazi ya bidhaa ni kwenda kukidhi mahitaji ya watu katika maisha ya kila siku.

K**a uhitaji wa bidhaa yako haupo sahau kabisa kuuza aina hiyo ya bidhaa maana utachemsha.

Epuka kutanguliza bidhaa kwanza kabla ya kujua k**a kuna soko lenye uhitaji wa hiyo bidhaa.

Ishi na hiyo kwa leo.

Cheers🥂

No risk no story. Weka kituo kikubwa na upigie mstari!
01/09/2023

No risk no story. Weka kituo kikubwa na upigie mstari!

Address

Dar Es Salaam
14000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Online Marketing System Pro posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share