17/10/2022
"Hello Swahili, Nlikuwa na mwanaume ambae nimemzidi mwaka mmoja,Nikapata ujauzito kwa kuwa alikuwa mwanafunzi hakuweza kuhudumia ujauzito hata mtoto alipozaliwa,Kwa bahati mbaya Mzazi wake mmoja alifariki,Wakapewa Yale mafao kila mtu mill 3
lkn walivyopewa nkamwomba elfu 50 tu akanizungisha wee mara naenda kulimia,mara ntakutumia mara haipatikani tena,na ndugu zake wote walijua nimezaa nae lkn hawakumtumia hata mia, mtoto alivyotimiza miaka miwili nlimwomba aje amwone mtoto Akasema hana nauli
nlimtumia nauli na nguo nkamshonea,Ili apendeze wazazi wasimdharau,akala naul na hajaja akazima cm,baada ya mtoto kutimiza miaka mitatu na Nusu alinitafuta tena Akasema yupo mitaa ya ninapoishi kweli nlifunga Kaz nkamwacha mtoto nkaenda kumuona,
Nlikuwa nimemmisi kwa kuwa nlikuwa nampenda nlisahau mabaya yote nkamwona Mpya,Nkalipia gest tukafanya yetu,kwa kweli sijawai msaliti tangu kuniacha na mimba hadi Mtoto miaka 3 na Nusu,nlijua bado mtoto hajui maana ya familia,baada ya kufanya yetu nikarudi Akasema atalala pale pale kesho aje rasmi kumuona mtoto nyumbani,
Na nlimwachia laki na cm yangu kubwa Tecno Y3 enzi hizo,nkabaki na Moja Tecno W3 ajifanye ameleta zawadi lkn alitokomea sikumuona,kwa mara ya kwanza nlikasirika mno,nlimchukia sana,Nikaamua kuachana nae nlilia sana lkn nsingemsahau
nikaamua kuwa na mwanaume mwingine aliyenizidi umri nkidhani yule ni mtoto huyu ataniendesha mm kwa kuwa ni mkubwa,Bas baada ya kutokomea alikaa miezi k**a sita akapiga cm oooh samahani bhana nliibiwa zile hela na cm nkaona aibu kuja,
nkamuuliza c ungesema na namba yangu unayo kichwan ningejua Cha kufanya kwa sasa huna nafasi kwangu nkakata cm,Nkaendelea na mpnz wangu Mpya mwanangu ana miaka minne baba yake hajawai mwona,
Bas taratibu za utambulisho zikatimia nkaanza kukaa na mwanaume Ila ndoa rasmi bado,Nkamzalia mtoto mmoja baada ya kukaa nae kumbe yule bwana ana mke ,laana kweli mtoto mie,majanga tu nikaamua kusepa tu na kitoto changu,
jamaaa wa kwanza nae alioa pia wakaachana Ila hawakuzaa,Sasa najiendesha nalea wanangu k**a single mama, Sisubutu kupenda naogopa mno,Et yule baba wa kwanza anasema sa hv kakua nimsamehe Aje amwone mtoto ajitambulishe tuanze Maisha hata k**a nimezaa ,
Nawaza nawazua nisijejikoroga tena mie mja laana kwa kutaka ndoa,Au nilee tu wanangu, Ushauri jamani
Kwa sasa Mtoto ana miaka 10 mkubwa na mdogo miaka 5 ,Nina miaka 4 nipo single mama,"