The Real Life TV

The Real Life TV Digital Media Platform
News • Entertainment • Exclusive Interviews

21/09/2026

Kibu Denis na Feisal wamekutana tena visiwani zanzibar. Team ya taifa Taifastars itaweka kambi hapo kabla ya mchezo wake wa kwanza utakaopigwa 28 September 2026.

21/09/2026

Kumekuwa na mijadala mbalimbali mitandaoni kuhusu vazi la msanii nandy ambae ni mke wa Billnas. Vazi hilo limekosolewa na baadhi ya watu wakidai sio vazi sahihi kwa mwana ndoa, huku wengine wakisema ni zuri na limempendeza.

19/09/2026

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. EDWARD MPOGOLO , amesema mtu atakayebainika kutupa taka hovyo jijini Dar es Salaam atatozwa faini ya shilingi 300,000 hadi milioni moja au kuhukumiwa kifungo cha miezi 12 hadi 24, kwa mujibu wa Kifungu cha 41 cha Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya Mwaka 2024 (GN Na. 1011).
Akizungumza leo, Septemba 19, 2026, baada ya kuhitimisha zoezi la usafi wa mazingira jijini, Mpogolo amesema sheria hiyo imeanza kutekelezwa kikamilifu ili kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi, salama na yenye mazingira bora.

“ Atakayekutwa anatupa uchafu hovyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Adhabu ni faini ya kuanzia shilingi laki tatu hadi milioni moja au kifungo cha miezi 12 hadi 24. Kila mmoja anatakiwa kutambua wajibu wake na kuacha mara moja tabia ya kutupa uchafu hovyo,” amesema.
Amesema Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi, lakini hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaotupa taka hovyo, kutiririsha maji au kufanya vitendo vingine vinavyokiuka sheria za usafi na mazingira.

Mpogolo amesema utekelezaji huo hauengi adhabu pekee, bali kujenga nidhamu, uwajibikaji na utamaduni wa usafi. Halmashauri pia itaendelea kuweka maeneo na vifaa vya kuhifadhi taka, pamoja na kuhamasisha utenganishaji wa taka kulingana na aina zake.

19/09/2026

"Mtumishi wa Mungu sio lazima uvae mavazi yale ya dini dini, au uwe mpoooole, hata ukiwa mwongeaji sana madamu unahubiri neno ni sawa tu" Maneno ya Niva Mbaga

Tazama full ipo Youtube THE REAL LIFE TV
Msafii Smp

19/09/2026

Shabiki wa Simba Sports Club ambae ni Niva Mbaga ameeleza yeye ni mchungaji kabisa na huduma yake amepangiwa kuhubiri watu wa mpira. Akizungumza na mwandishi, Mchungaji huyo amefunguka mambo mengi huku akihoji juu ya wacgungaji ambao wanatumia mafuta na chumvi kufanya miujiza ikiwa Yesu kristo alisema "Mkiwa na Imani ndogo k**a punje ya haradali mnaweza kuhamisha milima"

Tazama full interview Youtube THE REAL LIFE TV

19/09/2026

Niva Mbaga ameuliza maswali mengi kuhusu watumishi wa Mungu (Wachungaji) ambao hawatendi sawa maagizo ya Mungu. Mchungaji huyo ameeleza jukumu la wachungaji ni pamoja kufufua wafu!

19/09/2026

Mandala awageukia mashabiki wa Young Africans Sports Club baada ya uvumi kuwa wanataka kuomba card ya Aziz ki ifutwe ile aliopewa katika mchezo wa Yangasc dhidi ya Geita gold uwanja wa KMC.

Mandala amesema yanga walitamba kuwa na kikosi kikubwa lakini leo wanaomba rufaa ya card kufutwa jambo ambalo amelitafasri k**a woga wa Derby ya kariakoo 10 Octeber.

18/09/2026
18/09/2026

Shabiki wa Young Africans Sports Club Hamza Kizinga Jr. ameeleza ubora wa Simba Sports Club haupimwi kwa Mighty Wanderers wala Azam Football Club

Katika mahojiano Kizinga amesema kipimo cha simba kipo kwa yanga na hapo ndo wataona mifumo 555 ya Kocha wa yanga. 😆




18/09/2026

Shabiki wa Young Africans Sports Club ambae hajapenda kutaja jina lake amesema Simba Sports Club kucheza na yanga ndiyo jambo gumu kwa simba, lakini Yanga kucheza na simba ni kawaida sana! Vipi mtazamo wake uko sahihi? 😃😃

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Real Life TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share