PR ICON

PR ICON kuwa updated na story kali na za kusisimua about PUBLIC RELATIONS ACTIVITY, SUPER BRAND COMPANY BEIN

DKT. POSSI : UTETEZI WA MAWAKILI SERIKALI DHIDI YA TAASISI ZAKE, KUSIMAMIA MASHAURI YA MADAI, USULUHISHI NI KWA MASLAHI ...
23/05/2026

DKT. POSSI : UTETEZI WA MAWAKILI SERIKALI DHIDI YA TAASISI ZAKE, KUSIMAMIA MASHAURI YA MADAI, USULUHISHI NI KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA.

Arusha.

Rai hiyo imetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi wakati Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali , alisisitiza umuhimu wa umoja, mshikamano, upendo na weledi kazini kwa Mawakili wa Serikali kutetea Serikali na waambata wa Taasisi zake ili kulinda maslahi mapana ya Taifa, 21 - 22 Mei 2026 - Jijini - Arusha

Mkutano huo umekutanisha watumishi kutoka ofisi za mikoa 18 Tanzania Bara kujadili mafanikio, changamoto na namna ya kuimarisha utendaji kazi na ustawi wa watumishi. Naye, Wakili Alice Mtulo aliwapongeza watumishi kwa ushirikiano wao na kuwataka kutekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria, maadili na viwango vya taaluma.

PROF NOMBO : SHIVYAWATA YATOA MCHANGO WA MAONI WA MAPITIO YA SHERIA ELIMU, KUKIDHI MAHITAJI YA SASA YA SEKTA YA ELIMU. D...
22/05/2026

PROF NOMBO : SHIVYAWATA YATOA MCHANGO WA MAONI WA MAPITIO YA SHERIA ELIMU, KUKIDHI MAHITAJI YA SASA YA SEKTA YA ELIMU.

Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliyowakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa Tanzania imeendelea kuhimiza wananchi kushiriki zoezi la Ukusanyaji wa maoni ya Mapitio na Maboresho ya Sheria ya Elimu, Sura ya 353 kwa mifumo ya kidigitali na kieletroniki ya tovuti na mitandao ya kijamii ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Leo 22 Mei 2026 - Jijini Dodoma.

Aidha, Katibu Mkuu huyo, Prof. Nombo amesema mchakato huo unalenga kuhakikisha sheria mpya ya elimu inakidhi mahitaji ya sasa ya sekta ya elimu kuwa nyumbufu na shirikishi ikitoa nafasi kwa wananchi kutoa maoni hadi mwezi Juni kabla ya hatua za mwisho za kuwasilisha mapendekezo katika ngazi za maamuzi iinayojumisha Kamati ya Elimu, Utamaduni na Michezo kwa ngazi ya Bunge.

Mkutano huo uliodumu kwa siku mbili (2) umeshirikisha wadau muhimmu kutoka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wamepongeza ushirikishwaji huo na kusisitiza umuhimu wa elimu jumuishi, matumizi rasmi ya lugha ya alama katika ngazi zote za elimu, na kuhakikisha hakuna mwanafunzi mwenye ulemavu anayeachwa nyuma.

MHE. WANU: ASISITIZA MATUMIZI YA MIFUMO  KIDIGITALI, KUSANYA MAONI YA KUBORESHA SHERIA YA ELIMU - NCHINI. Dodoma. Naibu ...
21/05/2026

MHE. WANU: ASISITIZA MATUMIZI YA MIFUMO KIDIGITALI, KUSANYA MAONI YA KUBORESHA SHERIA YA ELIMU - NCHINI.

Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (mb) amesema Serikali inaendelea na Mapitio ya Sheria ya Elimu Sura ya 353 ikishirikisha wadau mbalimbali wa elimu kwa lengo la kuhakikisha sheria hiyo inakidhi na. kuendana na mahitaji ya sasa ya kisekta, Mabadiliko ya Sera, maboresho ya Mitaala na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.Aidha, Mhe.Wanu akizungumza Leo 21 Mei 2026 - Jijini Dodoma kupitia Kikao cha Wadau wa Kujadili Taarifa ya Awali ya Mapitio hayo, amesisitiza umuhimu wa wadau kuendelea kutoa maoni yao kwa uhuru na uwazi, ikiwemo kupitia tovuti ya Wizara.

PROF. MKENDA : MABORESHO YA SHERIA NA MFUMO IMARA WA ELIMU, KUFANIKISHA UTEKELAZAJI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO - 2014 ,...
21/05/2026

PROF. MKENDA : MABORESHO YA SHERIA NA MFUMO IMARA WA ELIMU, KUFANIKISHA UTEKELAZAJI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO - 2014 , TOLEO 2023.

Dodoma.

RAI hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST), Mhe. Prof. Adolf Mkenda, leo 21 Mei 2026 kupitia Kikao cha kujadili Taarifa ya awali ya mapitio ya Sheria ya Elimu Sura 353 ikiwa ni Utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu mageuzi ya Sekta ya Elimu ni muhimu kwa kuwa yanasimika msingi wa maboresho ya Sera, Mitaala na Sheria - Jijini Dodoma.

Amebainsha kuwa, Serikali imekwisha andaa Timu ya Watalaamu kwaajili ya Mapitio ya Awali, Wizara inaendelea na hatua za ukusanyaji maoni toka kwa Wadau wa Kisekta ili kuwezesha Uwasilishaji wa Mapendekezo kwa ngazi za maamuzi yanayozingatia shahidi za kisayansi.Vilevile, ameeleza Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wadau wote wa Sekta ya Elimu na kusisitiza umuhimu wa Ushirikishwaji mpana wa utoaji maoni ili kufanikisha kazi ya Mapitio ya Sheria hiyo.

Aidha, Prof. Mkenda ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa washiriki kuzingatia umuhimu wa kazi hiyo huku akisisitiza kuwa kazi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inayoasisi Mageuzi ya Sekta ya Elimu na kuwahakikishia wadau wote muhimu wa sekta ya Elimu kuwa Milango ya Wizara ya Elimu ipo wazi kupokea maoni na kuwaelekeza Viongozi wa wizara hiyo kuhakikisha zoezi la upokeaji wa maoni linaratibiwa kwa ufanisi na baadae kuwasilishwa katika Kamati husika.

Amehitimisha kwa kueleza kuwa Zoezi la Ukusanyaji maoni limechukua muda mrefu kwa lengo la kutoa fursa ya kila mdau kushiriki kikamilifu pamoja na kupongeza wadau wote walioshiriki kikamilifu kuwezesha zoezi hilo ikiwemo Sekta ya Umma, Wadau wa Maendeleo na Sekta Binafsi.

WIZARA YA UJENZI : SERIKALI KUJENGA ZAIDI YA KILOMETA 1,495 KWA KIWANGO CHA BARABARA YA LAMI HADI KUFIKIA 2026/31. Dodom...
21/05/2026

WIZARA YA UJENZI : SERIKALI KUJENGA ZAIDI YA KILOMETA 1,495 KWA KIWANGO CHA BARABARA YA LAMI HADI KUFIKIA 2026/31.

Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega (mb) amesema Serikali ya Awamu ya Sita (6) inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inatarajia kujenga Kilometa 1,494.45 kiwango cha Lami na Madaraja makubwa 18 kwa miaka mitano (5) wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha wa 2026/2027, hatua itakayoimarisha miundombinu ya Sekta ya Usafirishaji kuwa fungamanishi na kuchochea ukuaji wa Uchumi.

Mhe. Ulega amesema, Mtandao wa Barabara za Kitaifa (Road tarmac) unaoratibiwa na Wakala wa Barabara TANROADS umefikia Kilometa 37,734.41 ambapo Kilometa 12,225.26 zimeshajengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, Amefafanua wakati Tanzania inapata uhuru mwaka 1961 nchi nzima ilikuwa na Kilometa 1,360 pekee kwa Barabara za kiwango cha lami, huku Serikali ya Awamu ya Kwanza (1) mpaka Awamu ya Tano (5) zikijenga jumla ya Kilometa 9,369.81. Hali inayoonesha Kasi kubwa ya Maendeleo ya Miundombinu katika Ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni Mafanikio yanayoendelea kutekelezwa na kushuhudiwa na Serikali ya Awamu ya Sita (6) nchini.

Aidha , amebainisha kuwa Katika Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2025/2026 Wizara ya Ujenzi ilipanga kujenga na kukarabati Kilometa 450 za Barabara kuu na Mikoa za Kilometa 820 kwa kiwango cha lami na Changarawe. Hadi kufikia Aprili 2026, Serikali ilikuwa imeshakamilisha ujenzi na ukarabati wa Barabara za Kiwango cha Lami za Kilometa 94.36 za changarawe. Pia, Serikali imeeleza kuwa Utekelezaji huo unafungamana na ongezeko la Juhudi na Ubora wa miundombinu ya Usafiri ili kukidhi mahitaji ya wananchi kwa kurahisisha na kuharakisha ukuaji wa shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wa Ujenzi wa Miundombinu ya Madaraja , Mhe. Ulega amebainisha kuwa Serikali imekwisha kamilisha jumla ya ujenzi wa Madaraja Tisa (9) ikiwemo Mitomoni (Ruvuma), Mirimba (Katavi) , Nzali (Dodoma) , Kaleba (Kagera) na Itembe (Simiyu) na ujenzi wa madaraja 11 unaendelea huku Serikali ikiandaa miradi mipya ya madaraja 13 ikiambatana na Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa miradi mbalimbali. Aidha, Serikali imesisitiza miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa uimarishaji miundombinu ya Kisasa na kuongeza fursa za ukuaji wa uchumi wa ndani ya nchi kwa kurahisisha shuguli za kijamii na kiuchumi nchini.

WIZARA YA ULINZI:  TRILLIONI 4.39 KUIMARISHA ULINZI, MIUNDOMBINU NA UTEKELAZAJI WA MAJUKUMU YA JKT - NCHINI. Dodoma. Waz...
21/05/2026

WIZARA YA ULINZI: TRILLIONI 4.39 KUIMARISHA ULINZI, MIUNDOMBINU NA UTEKELAZAJI WA MAJUKUMU YA JKT - NCHINI.

Dodoma.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, amesema Serikali itenga jumla ya TZS Trilioni 4.29 kwa Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa Fedha 2026/2027. Aidha, Kati ya Fedha hizo, TZS Trilioni 3.86 zitatumika kwa matumizi ya kawaida huku TZS Trilioni 426.5 zikielekezwa kwenye matumizi ya Maendeleo. Bungeni - Jijini Dodoma.

Mhe. Nyansaho amebainisha kuwa, Mgawanyo wa fedha hizo, Jumla ya kiasi cha TZS Trillioni 3.2 zinatarajiwa kuelekezwa NGOME kwa matumizi ya kawaida na zaidi ya Shilingi TZS. Bilioni 54.8 zitaelekezwa kwa Maendeleo. Aidha, Fungu nambari 39 la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linatarajiwa kutengewa zaidi ya TZS Bilioni 626 kwa matumizi ya kawaida pamoja na karibu TZS Bilioni 19.9 kwa shughuli za maendeleo.

Vilevile, Mhe Nyansaho ameeleza kuwa, Upande wa Fungu 57 la Wizara ya Ulinzi, Serikali imepanga kutenga zaidi ya TZS Bilioni 35.5 kwa matumizi ya kawaida na Takribani TZS Bilioni 351.7 zitaelekezwa kwa Matumizi ya Maendeleo. Bajeti hiyo inalenga kuimarisha shughuli za ulinzi, maendeleo ya miundombinu, pamoja na utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Kujenga Taifa nchini.

21/05/2026

KITUO CHA TAFITI ZA FIKRA ZA XI JINPING CHA UJAMAA CHAZINDULIWA, KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUELIMU NA MAENDELEO YA CCM NA CPC.

Dar es salaam.

Viongozi kutoka Vyama Sita (6) Rafiki Kusini mwa Afrika wameshiriki Uzinduzi wa Kituo cha Tafiti kuhusu Fikra za Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Maono ya Kichina katika Zama Mpya, hatua inayolenga kuimarisha ushirikiano wa kielimu na maendeleo kati ya CCM na CPC.

20/05/2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amezungumza na Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia Kanda ya Tanzania, Malawi, Zimbabwe na Zambia Bw. Nathan Belete, aliyefika Ikulu hapo kuaga mara baada ya kumaliza muda wa utumishi wake aliohudumu visiwani hapo ikiwa ni pamoja na Utambulisho rasmi wa Mkurugenzi Mpya, Bw. Firas Raad.Tarehe 18 Mei 2026 - Ikulu - Unguja , Zanzibar.

UJUMBE WA RAIS SAMIA WASHIRIKI MKUTANO WA NEISA.- KIGALI Kigali.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Sami...
20/05/2026

UJUMBE WA RAIS SAMIA WASHIRIKI MKUTANO WA NEISA.- KIGALI

Kigali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tarehe 19 Mei 2026 amezuru nchini Rwanda kwaajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA) uliofanyika Jiji la Kigali - Nchini Rwanda.

Mkutano huo umeshirikisha Viongozi wa Bara la Afrika, Mashirika ya Kimataifa, Wawekezaji na Wataalamu wa Sekta ya Nishati walikutana kujadili nafasi ya nishati ya nyuklia katika maendeleo ya bara la Afrika. Aidha, Tanzania imeepiga hatua kubwa ya Uzalishaji wa Umeme na inaendelea kutekeleza Dira ya Taifa 2050 inayolenga kufikia uzalishaji wa umeme wa megawati 70,000 ifikapo mwaka 2050.

Aidha, katika kuhakikisha Serikali inafanikisha lengo hilo, Serikali imeunga mkono Matumizi ya Nishati ya Nyuklia salama ikiwa ni sehemu ya kuongeza vyanzo-mbadala vya Umeme Safi, Salama na vya uhakika. Tanzania imesisitiza Ushirikiano baina ya Serikali, Taasisi au Mashirika ya Kimataifa na Sekta binafsi ili kuwezesha upatikanaji wa fedha, teknolojia na wataalamu wa kuendeleza miradi ya nishati ya nyuklia barani Afrika. Pia, imeelezwa kuwa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi na manufaa ya nishati ya nyuklia ni muhimu ili jamii iweze kuelewa na kushiriki kikamilifu katika mageuzi ya sekta ya nishati.

MATUKIOWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ,(mb), amekutana na kufanya mazu...
20/05/2026

MATUKIO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ,(mb), amekutana na kufanya mazungumzo na mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Ndg.Rio Ferdinand katika kikao kilichohudhuriwa na viongozi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Mei 20, 2026 - Jijini Dodoma.

MATUKIO Dodoma.Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Micheweni, Mhe. Mahesh Shah (mwenye suti nyeusi) akisalimiana na  ny...
20/05/2026

MATUKIO

Dodoma.

Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Micheweni, Mhe. Mahesh Shah (mwenye suti nyeusi) akisalimiana na nyota wa zamani na Beki Bora wa Klabu ya Manchester United Rio Ferdinand (kulia) mara baada ya kuwasili Bungeni ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Mhe. Paul C. Makonda (hayupo pichani) akifuatiwa na - Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ndg. Greyson Msigwa (mwenye suti ya bluu) , Leo tarehe 20 Mei 2026 - Jijini Dodoma.

Address

Kimara
Dar Es Salaam
1061

Telephone

+255719831083

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when PR ICON posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to PR ICON:

Share