01/01/2024
Kwanza Lazima tule.
“Kwanza lazima ule, then mambo mengine yatafuata”
Yeyote anayeuza bidhaa zinazohitajika, anahitajika.
Muulize Mhe. Bakhresa alipata utajiri wapi….
Kilimo na chakula ndiyo moyo wa uchumi wa Tanzania. Naomba watanzania wote mnisikilize katika fursa ya kilimo na chakula, iko hivi Kilimo kimeajiri Zaidi ya watanzania , yaani watanzania wengi wameajiriwa na kilimo lakini hicho kilimo kinaingiza 25% ya GDP inakuja hiyo?
Katika mazao yote yanayozalisha, 40% ya mazao yote yanaharibika k**a post-harvest loss, inakuja hiyo?
Yaani iko hivi ikitokea mwaka ambao tumevuna sana post harvest loss inaongezeka, yaani ni kwamba hata k**a uzalishaji ukiongezeka kuna hasara kubwa zaidi kwa wakulima....
Afrika ikiwa na idadi kubwa ya watu Zaidi wenye miaka chini ya 40, ambao hawa watu ni wafanyakazi na walaji wakubwa.
Na pia kuna hawa watu wanaitwa middle class, ni wafanyakazi , maofisa mbalimbali, wale watu wanaopenda mambo ya kisasa, watu hawa wanaongezeka kila siku ambao wana uhitaji wa kila aina za vyakula mezani, hii ni fursa kubwa kwa watu wenye maono makubwa ya kusimama katika Fursa ya chakula na kilimo.
Zaidi ya 60% ya ardhi ni yenye rutuba haijaguswa Tanzania, na idadi ya watanzaania inaongezeka kila mwaka hii maana yake nini? Fikiria hekta 44million?
Idadi ya walaji inaongezeka.
Kuna demand ya vyakula ndani na nje ya Tanzania, yaani hii kitu watanzania hawajajua tu kuhusu sekta ya kilimo na chakula.
Acha mengine, sikia Chakula Afrika ni multi billion dollar market, na itaendelea kukua kila mwaka.
Chakula na kilimo ni pamoja na kilimo chenyewe, ufugaji, uvuvi pamoja na usindikaji..
Utajiri wa kilimo na chakula zaidi ya madini ya Mwadui- Shinyanga.
Kila mwaka bei za bidhaa za vyakula zinapanda, wakati vijana wanakimbia kutoka vijijini kulikojaa mashamba ya bei rahisi na kujazana mijini kutafuta kazi za kunyongea tai na wengine kuishia kuwa wezi, wengine makonda wa daladala wakati wana uwezo wa kusimamisha biashara zao kupitia kilimo.
Afrika ya sasa inazalisha chakula kidogo sana ukilinganisha miaka 50 iliyopita. Wengi wetu tunajisahau kuwa Afrika imejaa midomo mingi inayohitaji kula kuliko kuongea. Matajiri wakubwa duniani wengi wanakimbilia katika fursa ya vyakula.
Wengi wetu tukisikia kilimo, nini kinakuja akilini?
Zinakuja picha za mzee aliyechoka, asiye na elimu akiwa ameshika jembe kijijini?
Wengi wetu bado tunafikiri kuwa kilimo ni kwaajili ya watu masikini wasio na Elimu.
Hivi unajua kuwa Afrika imekalia mgodi katika kilimo lakini wengi wetu hatuna macho ya kuona? K**a wewe ni kipofu naomba uniruhusu nikufungue macho.
Unajua kuwa Tajiri mkubwa Afrika , Aliko Dangote, amewekeza zaidi $1 bilioni katika uzalishaji wa mchele tu? Hujajua kuwa analima na nyanya pia? Wewe endelea kuagiza mizigo chaina au tujazane mjini k**a sisimizi.
Kila mwaka Afrika tunatumia mabilioni ya dola kuagiza mchele kutoka nje, Dangote amenusa akaona hela na hicho ni kiasi kidogo sana ukilinganisha na uhitaji?
Hivi unajua kuwa 2009 maelfu ya wawekezaji kutoka USA, Ulaya, Middle East na Asia wameivamia Afrika wananunua na kukodi maelfu ya maekari ya mashamba kwaajili ya kilimo?
Kwasasa ni trend…huko majuu …yaani imekuwa kawaida …wawekezaji wengi wanakimbilia Afrika kujipatia maelfu ya maekari vijijini wakati sisi tumejazana mijini?
Watanzania walio wengi wakipata hela kidogo wanakimbilia Kariakoo kwenda kufungua frame, umewahi kuona Mzungu haswaa achana na wachina anakuja Tanzania na kwenda kariakoo kufungua Frame….akili kichwani
Kilimo ni mgodi uliosahaulika na waafrika wakati wawekezaji kutoka nje wanajinyakulia tu kwa bei rahisi.
Hivi unajua kuwa sekta ya kilimo itakuwa na thamani ya zaidi ya $1 trillion mwaka 2030?
Bado huelewi tu?
Kulingana na projection za UN k**a hii ikitokea basi fahamu kuwa kilimo kitakuwa zaidi ya UTAJIRI WA MAFUTA AFRIKA.
Katika facts hizi zote, tunaona matajiri wote wakubwa duniani wanawekeza Afrika; inakuaje waafrika wengi tumebaki vipofu na kucheka cheka wakati tumekalia migodi?
Tumeyakimbia maeneo makubwa vijijini kuja kujazana mijini kuwa machinga na vibaria tunabanana kwenye daladala k**a tumefukuzwa kwetu na kuyaacha mashamba makubwa vijijini yakisimamiwa na wazee.
Nikupe picha:
• Agriculture (Kilimo): kilimo ni faida lakini kuna aina za kilimo. Kuna kilimo cha kubangaiza ambacho wengi wanafanya na kilimo faida. Hapa ni pamoja na kuchagua aina ya mazao ya kulima kulingana na mtaji na faida, business model utakayotumia, wateja utakaowatarget . Wengi wetu wakisikia kilimo anaenda kulima mahindi wakati mtaji wake ni wa Million moja, sasa mtu k**a huyo usitegemee atapata faida..atalima mahindi ya kula mwenyewe. Lazima uchague zao ambalo tunaita high value crops, ambazo unaweza kuanza na mtaji mdogo na ukafanya kibiashara.
• Manufacturing (Usindikaji): Hapa mnaelewa, hapa tutahitaji kuchambua kiundani sana hapa
• Fast Moving Consumer Goods: Bidhaa za vyakula zinazotembea kwa haraka sana na zinahitajika sana sokoni kwa haraka. Lazima uwe mjanja siyo unaenda tu.
• Kusimamisha brand ya chakula itakayobamba Africa Tanzanian brands: Kusimamisha brand yako ya vyakula mbalimbali
• kuna Niche market hii ni pamoja na huduma mahoteli, shule, jeshi, viwanda, catering nk
Tukianza na fursa ya kwanza katika chakula ni hii hapa:
# Kuzalisha nafaka zinazoagizwa sana kutoka nje. Hizi zinaingizia taifa hasara kubwa. Inakera sana
Faida ipo k**a ukizalisha na kusindika kabisa.
Nafaka k**a ngano, soybeans, nafaka k**a mtama nk.
Nitakuambia kwanini?
Tanzania kwa Afrika tunajitahidi sana kuzalisha mchele, hiyo ni sawa, lakini bado. Vyakula vya nafaka k**a hivyo, ukijenga network na taasisi mbalimbali za kimataifa zikiona una mwelekeo mzuri zinawekeza kwako pia na kukupa nafasi ya kusimamia…
Jambo la msingi hapa katika Fursa hii….usiwe k**a wakulima wengine wanaoenda kwa kuhemka.
Jenga ukaribu, tafiti viwanda mbalimbali vya bia, wazalishaji mbalimbali wa mikate, cakes, sweeterners and ethanols, viwanda vingine vingi vya vyakula….
Ukitoka hapo, unatakiwa kujiuliza k**a unaweza kuwa msindikaji mkubwa wa bidhaa hizo kwa kuzalisha mikate ama bidhaa mbalimbali zitokanazo na mazao hayo ya nafaka…zipo nyingi….Kuna mkate wa mchele, ndiyo kuna mikate ya mchele nadhani mnaijua wengi na bidhaa nyingi tu…
Tutaendelea.
podcast
.
www.mazaohub.com