Matukio ya Ajabu Duniani

Matukio ya Ajabu Duniani We are a team of passionate marketers and advertisers who love to share the latest trends and insights in the world of advertising and marketing.
(2)

We also enjoy sharing fun and entertaining videos, interesting news articles and a variety of other niches. stay with us for more experience

NANI MKALI WA RHUMBA/BOLINGO HAPA KATI YA HAWA?1. Franco luambo makiadi.2. Tabu Ley Rochereau.3. Papa wemba.4. Pepe kale...
13/05/2026

NANI MKALI WA RHUMBA/BOLINGO HAPA KATI YA HAWA?

1. Franco luambo makiadi.
2. Tabu Ley Rochereau.
3. Papa wemba.
4. Pepe kale.
5. Koffi Olomide.
6. Awilo Longomba.
7. Samba Mapangala.
8. Tx Moshi William.
9. Ngurumo.
10.Banza Stone Mwanawasa.
11.Ally Choki.
12.Werrason
13.Ferre Gola.
14.Fally Ipupa

k**a una mkali wako ongeza hapa.

Watu maarufu ambao hawakuwahi kupata Watoto Maishani mwaoTujikumbushe watu maarufu k**a wanasiasa, wanamuziki, wacheza f...
12/05/2026

Watu maarufu ambao hawakuwahi kupata Watoto Maishani mwao

Tujikumbushe watu maarufu k**a wanasiasa, wanamuziki, wacheza filamu nk ambao hawakuwahi kupata watoto wa kuwazaa katika maisha yao hapa Duniani.

Wanaweza wakawa ni kutoka hapa Bongo au nje ya Bongo. Naanza na hawa:

1. Kamuzu Banda - Rais wa kwanza Malawi
2. Omar Al Bashir - Rais wa Sudan
3. Steven Kanumba-Muigizaji
4. Wema Sepetu-Muigizaji
5. JB-Muigizaji
6. Ngwea-Mwanamuziki

Unaweza ukaendelea na wewe...

Ukifanikiwa kimaisha kabla ya kuoa kuna uwezekano mkubwa ukaoa mwanamke asiye na mapenzi nawe.Ukisikia mtu anasema wanaw...
05/05/2026

Ukifanikiwa kimaisha kabla ya kuoa kuna uwezekano mkubwa ukaoa mwanamke asiye na mapenzi nawe.

Ukisikia mtu anasema wanawake wengi wanaolewa na mwanaume wasiempenda, usifikiri anachekesha. Uhalisia ni kwamba, mwanaune anaoa mwanamke anaempenda, mwanamke anaolewa na mwanaume ambae yupo tayari. Utakapoweka maisha yako kwenye mstari wanawake watakuona na watakujia na mitego ya kila mamna wakunase. Hautajua nani shetani nani malaika maana wote watakujia na tabasamu.

Watakuendea kwa mchungaji, watakuendea kwa mganga, watajifanya wema kwa wazazi wako, watawachangamkia marafiki zako n.k. Women are opportunistics. They can't engage where there is no benefits.

As a man, your value skyrockets with every level you attain. When you rise to the top you bacome the prize. Don't hand your commitment to any woman who flashes smiles and curves. F**k her if you must, but keep looking for value.

Usijali sana masuala ya kutaka kupendwa. Hakuna upendo wa bure kwa mwanaume hapa duniani. There is no unconditional love for a man. As a man you will be loved on condition that you're able to provide and protect.

Sio vibaya kupendwa lakini sio kitu cha kulilia au cha lazima. As a man just focus to be a man no one can ignore. Masuala ya kutaka kupendwa waachie wanawake na watoto.

Vet ruthlessly, you didn't build your life to throw it away on a liability. Check her past. Past is not just a past, it's a pattern of habits and behavior, and the strong predictor of future loyalty. Judge a woman harshly and ruthlessly based on her past.

Kumbuka hata utakampopata mmoja alienyooka, haimaanishi kwamba na wengine wataacha kujileta kwako. Mwanamke hatafuti mwanaume mwaminifu wa peke ake, anataka mwanaume mwenye thamani ya juu katika circle yake. Ni bora awe demu wa nane kwa Lugumi kuliko kuwa peke ake kwa winga. Sijui utawafanya nini hawa, but either way don't take them serious.

Vile vile, kumbuka pia utakapotoboa na kujiwekea standards mfano bikira, hautaki single mother, hautaki mshangazi wa 30+ n.k, wanajamii watataka kukufundisha morality. Utasikia singo maza ni wapambanaji, sijui past does not matter na ujinga jinga mwingine Wapuuze.

Wakati unahustle hakuna aliekua ana time na opinions zako, kwanini waje kukupangia sasa hivi. Stand firm, don't compromise your standards, be ruthless with your choice, because you earned that power. Power is not meant to be polite.

Leo una hamu ya nini?Kwema, salamu zisiwe nyingi.Twende kazi una hamu ya kitu gani leo?A.Kazi.B.Chakula gani?C.Ibada.D.M...
30/04/2026

Leo una hamu ya nini?

Kwema, salamu zisiwe nyingi.
Twende kazi una hamu ya kitu gani leo?

A.Kazi.
B.Chakula gani?
C.Ibada.
D.Mapenzi
E.Pombe.
F.Kulala.
G.Kukata gogo.
H.Umbea.

Na vingine uvitaje wewe.

Wanawake mnaopenda kulambwa mnatukosea sanandugu zangu.Ukiwa na akili yale mazingira yanatisha hakika , yanaogopesha mno...
29/04/2026

Wanawake mnaopenda kulambwa mnatukosea sana

ndugu zangu.

Ukiwa na akili yale mazingira yanatisha hakika , yanaogopesha mno hasa linapokuja swala la kulamba .

Wanaume tumekua tukionewa na kunyanyasika dhidi ya dhuluma hii na wengine wanafanya si kwa kupenda kwao bali ni kwakulinda penzi lao akidhani kulamba hatoachwa.

Hakika mnatukosea mno na mnatutisha sana ,

Kufikia hapo sina la ziada.

Usiishi na Mwanamke Mzuri kisasa. Mzalishe chapuchapu angalau watoto wawili, watatu. Huna hasara hata mkiachana.1. Sitac...
29/04/2026

Usiishi na Mwanamke Mzuri kisasa. Mzalishe chapuchapu angalau watoto wawili, watatu. Huna hasara hata mkiachana.

1. Sitachoka kuwafundisha ninyi vijana. Maana wengi wenu hamkuishi na Wazee nazungumzia wazee waliozaliwa kabla ya mwaka 1940. Hao ndio Wababu.

2. Mtibeli nilibahatika kuishi na Wazee waliozaliwa miaka ya 1920-1945. Nikajifunza baadhi ya issues kutoka kwao. Na bahati nzuri walikuwa rafiki zangu. So nje ya kupenda kusoma pia nimejua baadhi ya ishu kwa kukaa na wazee.

3. Ninaheshimu Wazee kwa uzoefu wao wa maisha. Haimaanishi nilikubali Kila walichoeleza.

4. Moja ya Falsafa nilizojifunza kutoka kwao. Mzee wangu Mmoja aitwaye Clifford Tenga ambaye sasa ni Marehemu, tukiwa kwenye matembezi katika kijiji cha Kisiwani, Wilaya ya Same. Katika Stori akaniambia;

5. Ukioa mwanamke mzuri usimkawize, mzalishe watoto angalau wawili watatu chapuchapu. Nikamuuliza kwa nini?

6. Akaniambia, akijibu k**a Mwanasiasa, kwani alikuwa Diwani wa kata ya Kisiwani kupitia CCM. Akasema, Resources lazima uzitumie vilivyo. Na fursa usiyo na uhakika nayo lazima uhakikishe unaitumia kikamilifu.

7. Bado Namsikiliza. Hapo nilikuwa kidato cha tano Likizo. Nimeenda Kumsalimia Babu Clifford.

8. Akaendelea, Mwanamke Mzuri ni k**a rasilimali nyeti ambayo wanaume wengi hupambana kuipata. Unapomiliki mwanamke Mzuri usimkawize. Usiishi naye kwa akili ya kuwa atakuwa wako Milele. Kwa namna hiyo use her effectively.

9. Mzee tulipiga stori nyingi Sana lakini hiyo Leo nimeikumbuka. Na nimeamua kushiriki nanyi kwa ambao wataona waitumie hewala.

10. Kanuni hii sisi Watibeli tunaitumia. Watibeli hatunaga Hasara kwa sababu tunajua wakati na jinsi ya kutumia rasilimali.

11. Mapenzi kwetu ni k**a kunywa Uji wa vuguvugu. Yaani shwaaa! Kwa sababu hatuishi kwa hisia bali tunaishi kwa Kanuni.

12. Ndio Maana Leo mimi Mtibeli, nakuambia kijana wangu. Utakapopata mwanamke Mzuri. Mwenye hadhi, cheo, au msomi. Akaingia kwenye 18 zako.

13. Jua, it's your turn, ni zamu yako. Na muda wa kudumu naye itagemea how you play your balls. Nitakurahisishia kazi hapa.

14. Elewa mwanamke hisia zake zinaenda kwa kubadilika. Hivyo usizitegemee hisia zake k**a nguzo kuu ya mapenzi na uhusiano wenu. Anavyokupenda Leo na kukuona Leo sivyo atakavyokuwa hivyo miaka mitatu au mitano ijayo.

15. Kwa kujua hilo, unatakiwa kuongeza ziada ya hisia zake. Ziada hiyo ni utegemezi usiovunjika kirahisi.

16. Utegemezi na connection isiyovunjika kirahisi. Hapo ndipo kumzalisha watoto inapokuwa mbadala wa hisia zake.

17. Mwanamke kadiri unapompa mzigo wa watoto ndivyo anavyopoteza ramani ya kujua akuache vipi.
Hisia hata zikiisha, sasa atawaza watoto wangu (wenu) itakuwaje? Mtoto mmoja kwa mwanamke sio tatizo anaweza kukuacha mapema tuu ingawaje pia atafikiri mara mbilimbili.

18. Mwanamke Mzuri unapomzalisha watoto wawili watatu. Kiukweli hauna hasara. K**a ni biashara imelipa. Umejua kutumia resources vizuri.

19. Muda sahihi wa kumzalisha mwanamke watoto. Ni kipindi hisia zake zipo juu Sana kwako na kipindi ambacho hajapata uhalisia wa maisha.

20. Iko hivi wanawake wengi wanapenda kuzaa watoto wengi, yaani kuanzia wanne. Hilo weka kichwani. Wanawake hupenda kuzaa na mwanaume mmoja tuu.

21. Katika umri chini ya miaka 25 wanawake wengi bado hawajakomaa kujua uhalisia wa maisha. Hivyo suala la kuzaa watoto hulichukulia kirahisi.

22. Usiishi kisasa na Mwanamke mrembo. Utaumia Mzee. Leta uzungu kwa mwanamke mzuri alafu huyo mwanamke akutane na Sisi watibeli. Tunambomoa utashangaa mimba zinaingia na kuzaa k**a sungura.

23. Mwanamke ukishaishi naye. Miaka Ile mitatu kwenda minne ya mwanzo hakikisha tayari unawatoto wawili.
Hiyo ni kutengeneza uwezekano na uhakilka kwa sehemu kubwa.

24. Hapo yeye ndiye atawaza familia said hasa kuwahusu wewe mumewe, watoto wenu na yeye. Wakati wewe kwa kusogeza kete hiyo utakuwa unawaza kutafuta pesa na kutunza familia.

25. Pressure kubwa itakuwa kwake kwamba akifanya ujinga akavunja ndoa tayari anawatoto wawili watatu. Ninakuhakikishia sio rahisi mwanamke kuvunja nyumba akiwa na watoto wawili watatu. Yaani mpaka uwe umefanya Jambo kubwa Sana tena kwa muda mrefu.

Na sio Ile ya ati amedanganywa na wanaume wa mjini. Nani alikuambia mwanamke anadanganywa? Hawadanganywi Bali wanawake hufanya mambo Yao wakiws tayari wamesha calculate faida na hasara. Na wapo tayari kwa matokeo.

26. Ukishaona mwanamke mzuri anakuambia anahofu ya kuzaa na upo naye. My friend kuna sehemu umefeli pakubwa. Tayari akili zake zimerejea. Kikawaida mwanamke akikupenda na akiwa na hisia na lile wenge la Kwanza kwako haoni shida kuzaa watoto wengi.

Na Sisi wanaume ndio tunakuwa na hofu ya watoto kutokana na kuangalia hali ya maisha. Kwamba utawaleaje watoto wakati uchumi haujakaa vizuri.

27. Hiyo kwako ni fursa ambayo hutakiwi kuiacha ipite. Hata k**a unamaisha magumu kiasi gani. Ukiwa na mwanamke mzuri unayempenda Sana akawa na kiu ya kuzaa watoto wengi. Usiogope zaa. Wakifika wawili au watatu hapo stop kidogo ndio unaweza kufikiria ugumu.

28. Hiyo ni fursa kwako isiyojitokeza mara mbili. Usiwe wale wanaume wa ngoja mambo yakae Sawa ukiwa mbele ya mwanamke mrembo. Hakuna cha mambo kukaa sawa. Mpe anachotaka. Utamuelewa baadaye. Wanawake warembo hawapendi wanaume waoga wa maisha na majukumu. Yaani uogope kuwatunza watoto wawili au watatu?

29. Oooh! Tayari tunamtoto mmoja. Acha nijiendeleze kielemu. My friend k**a mwanamke wako ukimtazama hivi unamuona ni Kifaa, kisu, pisikali iliyonyooka. Achana na mambo ya kisasa kwa muda ila tumia akili Sana.

30. Bahati nzuri ada utatoa wewe. So unamuambia atasoma mwaka huu. Ikifika tarehe za kulipia vyuoni hata k**a unahela Fanya mambo yanaingiliana.

Mpe moyo kuwa lazima atasoma huku ukimpenda na kumfanyia mind games. Mtie mimbia ya pili. Akishajifungua mtoto wa pili. Mshukuru, mpe na pesa kabisa k**a zawadi.

31. Kisha wakati wa chuo. Mpe hela ya usajili na ada kabisa aparangane mwenyewe.

32. Mwanamke mzuri aliyekuzalia watoto kuanzia watoto wawili - watatu. Huyo hauna hasara. Lakini k**a ndio mtoto mmoja au hauna kabisa, lazima roho ikutoke.

33. Mapenzi kwa vijana wa miaka 20-30 ni mchezo wa kuviziana k**a Draft tuu. Mwanamke anamvizia mwanaume vivyohivyo kwa mwanaume kumvia mwanamke. Ni umri wa kutokuwa na uhakika na uwezekano. Hivyo unatakiwa kucheza kete zinazokupa uhakika na uwezekano mkubwa. Hata k**a deal likifa bado unafaida kwenye mchezo.

34. Kwa kijana ukishakuwa na watoto wawili watatu kwa mwanamke mmoja. Asilimia kubwa matatizo ya mwanamke hayatakuwa kwenye mambo ya kuangalia wanaume wengine huko. Kwani ushamuwekea Msalaba. Kiburi cha mwanamke kinaenda chini.

35. Malalamiko yandoa kwa wanawake wenye watoto wawili watatu husababishwa na wanaume kutokuwa waaminifu huku mwanamke akiwa analinda zaidi familia yake kwa maslahi ya watoto

36. Wanawake wakishakuwa na watoto wawili kuendelea plan zao hubadilika. Mbinu za kivita zinabadilika. Wanajipanga kwa vita ya baadaye.

37. Wengi husema nasubiri watoto wangu wakue alafu huyu mwanaume nitamnyoosha. Hapa ni k**a mwanaumee alikuwa mkandamizaji na anayemdhulumu mkewe.

38. So ukiwa umemzalisha mtoto wawatu watoto wawili watatu kuendelea. Sio sababu ya kumkosea na kumdhulumu haki yake. Unafanya hivyo kwaajili ya kulinda himaya na maslahi yako Kwa future k**a unampango wa kuishi mpaka uzee na mkeo mzuri.

39. K**a unamtesa mkeo jiandae kwa vita ya pili muda usiotarajiwa hasa baada ya watoto kukua.

40. Kwa Watibeli hatuwezagi kutesa Wanawake zetu. Ingawaje tunajua njia za kujihami endapo itatokea ukaoa mwanamke atakayeanzisha vita vya uzeeni dakika za jioni.

Maisha ya sasa ya msanii Saida Karoli.Nimerejea Bukoba kwa likizo baada ya miaka kadhaa, na kwa masikitiko makubwa nilik...
27/04/2026

Maisha ya sasa ya msanii Saida Karoli.

Nimerejea Bukoba kwa likizo baada ya miaka kadhaa, na kwa masikitiko makubwa nilikumbana na hali iliyonishtua sana. Nilimkuta msanii nguli wa muziki wa asili, Saida Karoli aliyewahi kutoa nyimbo zilizopata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hadi kuvuka mipaka ya Tanzania akiishi maisha ya dhiki yasiyoendana kabisa na hadhi na mchango wake mkubwa katika sanaa na utamaduni wa taifa.

Kwa sasa, Saida Karoli anaishi katika nyumba ya kupanga ya vyumba viwili, katika mazingira yasiyofurahisha, hali ambayo haistahili hata kidogo kwa msanii aliyewahi kuiwakilisha nchi yetu kimataifa kwa heshima kubwa. Hali hii inanifanya nijiulize maswali mazito kuhusu mfumo wetu wa kulinda wasanii, hasa wale waliotoa mchango mkubwa kabla ya enzi ya mifumo ya sasa ya kidijitali.

Kwa wajuzi wa masuala ya commercial entertainment, je, hakuna njia ya kusaidia wasanii k**a Saida Karoli kufaidika na royalties za kazi zao walizofanya miaka ya nyuma? Je, sheria na taasisi zetu za hakimiliki zinawafikia kwa vitendo, au zipo tu kwenye maandishi?

Zaidi ya hapo, tukio hili linapaswa kuwa funzo kwa wasanii wanaong’ara kwa sasa. Umaarufu ni wa muda, lakini maisha ni ya kudumu. Ni muhimu kwa wasanii wa kizazi cha sasa kupambania sera imara za kulinda kazi zao, kudai haki zao za kisheria, kusaini mikataba yenye kuwanufaisha hadi baadaye

Kwa kweli, hali niliyoikuta imenihuzunisha sana.

Hawa ni wasanii ambao wametoa ngoma kali na kuweza kuhit ukanda wa ziwa wote. Ni wasanii ambao wanajaza sana kwenye show...
27/04/2026

Hawa ni wasanii ambao wametoa ngoma kali na kuweza kuhit ukanda wa ziwa wote. Ni wasanii ambao wanajaza sana kwenye show zao.

1. Malingita
2. Bhudagala mwanamalonja
3. Bahati wa bugalama
5. Ngelela
6. Kisima
7. Juma marco
8 Gudegude
9. Inaga
10. Bushemeli

21/04/2026

Asubuhi Asubuhi wana wakazichapa,nani ameupiga mwingi?
fans Bongonewz Tanzania

Tangu Vanessa Mdee aache muziki, hakuna mwanamuziki wa k**e yeyote aliyeziba pengo lakeKatika historia ya muziki wa Bong...
16/04/2026

Tangu Vanessa Mdee aache muziki, hakuna mwanamuziki wa k**e yeyote aliyeziba pengo lake

Katika historia ya muziki wa Bongo Flava na Afrika Mashariki kwa ujumla, jina la Vanessa Mdee linabaki kuwa alama ya mafanikio, ubunifu, na ushawishi mkubwa.
Vanessa allijijengea himaya yake si tu k**a mwimbaji, bali pia k**a mtangazaji napo alifanya vizuri sana.

Vanessa alitushtua wengi alipotangaza ameamua kuachana na muziki rasmi aishi maisha yake nje ya muziki.

Wengi mwanzoni tulidhani ni kiki k**a zilivyo kiki nyingine ,kumbe bhana bi dada alidhamiria kweli kweli .

Kilishotushangaza zaidi Vanessa aliamua kuacha muziki akiwa kwenye peak , yani kila wimbo akitoa ni hit tu back to back.

Niwarudishe nyuma kidogo.....

Vanessa Mdee alianza kujulikana kupitia utangazaji kabla ya kuingia rasmi kwenye muziki. Aliwahi kufanya kazi na MTV Base, jambo lililompa exposure kubwa sana kimataifa hivyo hata kuingia kwake kwenye muziki kulianza kwa kishindo kikubwa , na haraka akawa mmoja wa wasanii wa k**e waliotawala chati za muziki Tanzania.

Licha ya kwamba wakati huo tasnia ya muziki ilikuwa imejaa wanaume wengi, lakini Vanessa aliweza kusimama imara na kujitengenezea nafasi yake.

Aidha, alifanikiwa kushinda na kuteuliwa kwenye tuzo mbalimbali k**a:
MTV Africa Music Awards
All Africa Music Awards

Vanessa alifanikiwa pia kupata dili kutoka kampuni mbalimbali kuwa balozi wao kutokana na nguvu ya ushawishi aliyokuwa nayo.

Pamoja na mafanikio hayo yote,
Kitu kilichowashangaza wengi ni pale Vanessa alipotangaza kuachana na muziki rasmi.

Vanessa aliacha muziki kipindi ambacho bado yupo juu kileleni na mashabaki lukuki wapo nyuma yake kusubiri ngoma zake.

Binafsi ninakumbuka sababu kuu aliyoitaja Vanessa kuachana na muziki ni MASLAHI.

Vanessa alikuwa anadai anatumia pesa nyingi kuandaa wimbo, gharama nyingi kwenye show lakini anachoingiza ni kiduchu .

Hivyo ni uthibitisho tosha kwamba muziki hapa bongo bado sana kwenye maslahi labda k**a msanii target yake ni hapa hapa ,hivyo maandalizi local, bajeti ndogo, ila k**a anataka vitu vya kimataifa ili na yeye akue kimuziki na kupata ridhiki ya kueleweka kwa hapa bongo ni ngumu mno.

Licha ya hivyo , sababu zingine alizozitoa ni hizi.

1. Afya ya akili (Mental Health)
Vanesa alidai kuwa maisha ya muziki yalikuwa yanamchosha kiakili na kihisia, Umaarufu huja na presha kubwa ambayo si rahisi kuhimili kwa muda mrefu.

2. Kutafuta Amani ya ndani
Vanessa alisema alihitaji maisha ya utulivu zaidi nje ya kelele za umaarufu na mashindano ya tasnia ya muziki.

3. Mahusiano na Rotimi
Baada ya kuanzisha familia na kuhamia nje ya Tanzania, vipaumbele vyake vilibadilika. Alianza kuona maisha nje ya muziki yana thamani zaidi kwake binafsi.

4. Imani na Mwelekeo Mpya
Katika baadhi ya kauli zake, aligusia pia mabadiliko ya kiimani na mtazamo mpya wa maisha uliomfanya aone kuwa muziki haukuwa tena njia sahihi kwake.

Binafsi nina imani huenda ipo siku atarudi tena kwenye muziki kutuburudisha , ila sasa ni ngumu sana kuacha muziki kisha ukarudi ukategemea utapata mapokeo yaleyale k**a mara ya kwanza, tuchukulie mfano mzuri Mzee Yusuph, alikuwa na mashabiki tele kabla ya kutangaza kuachana na muziki.

Baada ya kukaa nje kimuziki kwa muda mrefu kisha akarejea, kila wimbo anaotoa ni flopp , hakuna wimbo wowote uliohit tangu arudi kwenye muziki.

Watanzania waliopata umaarufu wa ghafla mitandaoni na kisha kupotea.itandao ya kijamii imetoa fursa kubwa sana kwa mtu y...
15/04/2026

Watanzania waliopata umaarufu wa ghafla mitandaoni na kisha kupotea.

itandao ya kijamii imetoa fursa kubwa sana kwa mtu yeyote ‘kwenda mjini’ chap. Hii ni orodha ya baadhi ya watu ambao kusingekuwa na intaneti, wasingepata umaarufu walioupata.

DKT. LOUIS SHIKA
Dkt. Louis Shika alijipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za mfanyabiashara Said Lugumi. Alifahamika zaidi kwa msemo wa “900 itapendeza” baada ya kupiku watu wengine waliokuwa kwenye mnada huo. Shika alifikia hatua ya kuwa balozi wa makampuni kadhaa na stori yake ya kutekwa Urusi ilikuwa ni moja ya mada muhimu katika mahojiano mengi aliyofanya na vyombo vya habari. Kwa sasa Dkt. Shika ni marehemu. Alifariki Agosti, 2020.

PIERE LIQUID
Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa jamaa aliyeishika mitandao ya kijamii wakati fulani. Huyu jamaa jina lake halisi ni Peter Gumbo, na amejizolea umaarufu baada ya video iliyomuonesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka 2018. Katika wakati wake akiwa juu ya kilele cha umaarufu, Liquid amebahatika kuwa balozi wa suehemu za starehe na kutumika kupromote baadhi ya bidhaa.

CHIKUMBALAGA
Jamaa huyu alikuja kuwa maarufu sana kwenye mitandao ya kijamii. Chikumbalaga, aka Sukariyao, alitokea nyumbani kwao huko Tunduma Mkoani Mbeya hadi kufika Dar es Salaam ambapo umaarufu ulizidi kukua. Umaarufu wake ulitokana na muonekano wake na namna alivyokuwa akijibu maswali kwenye interviews mbalimbali. Katika moja ya mahojiano na Millard Ayo TV, Chikumbalaga aliulizwa ana miaka mingapi akajibu, “Sabini na tano” na alipoulizwa amezaliwa lini alijibu “2005”.

Sukariyao pia alpata umaarufu kwa njia ya wasanii kumtumia kwenye upande wa kuchekesha pale anaposhea video na audio akizisapoti kwa kucheza au kuimba nyimbo za wasanii hao kisha kupost mitandaoni.

Jamaa hayupo sana kwenye spotlight kwa sasa. Je, yupo wapi?

MZEE WA MJEGEJE
Unakumbuka msemo wa"kata simu, tupo site"? limekuwa maarufu sana kwenye majukwaa ya mtandaoni nchini Tanzania ambapo watumiaji mara nyingi walilitumia. Katika video iliyosambaa sana, Mzee wa Mjegeje alionekana akiongea kwenye simu ndogo, akisema "Kata simu, kata simu, tupo site."

Tangu wakati huo, maneno hayo ya kuchekesha kutoka kwenye video hiyo yamekuwa yakitumiwa sana katika vichekesho, na baadhi ya wasanii hata wameyajumuisha katika nyimbo zao. Mzee Mjegeje, aliyejulikana pia k**a "Raisi wa Bagamoyo," alikuwa mkazi wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani. Umaarufu wake ulivuka mipaka, ukifikia umaarufu wa kimataifa, haswa nchini Kenya mnamo 2022 wakati video yake "Kata simu, tupo site" ilipovuma kwenye mitandao ya kijamii. Sasa hivi Mzee wa Mjegeje ni marehemu.

MAJALIWA MVUVI
Majaliwa Jackson ni mvuvi aliyefanikisha kuufungua mlango wa ndege na kufanikisha kuokolewa kwa abiria 24 waliokuwa ndani ya ndege ya Precision Air iliyotumbukia Ziwa Victoria Jumapili ya Novemba 6, 2022 karibu na Uwanja wa Ndege Bukoba, Mkoani Kagera. Baada ya tukio hilo Majaliwa alipokea zawadi mbalimbali k**a vile shilingi milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwa wakati huo, Albert Chalamila.

Baadaye kijana Majaliwa alipokelewa katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan. Alielezwa kujiunga na Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chongo Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga. Je, kuna mwenye taarifa zaidi kuhusu Majaliwa?

MZEE MPILI
Shabiki na mwanachama mwandamizi wa Yanga SC Mzee Haji Omary Mpili ni mkazi wa Rufiji Pwani katika kijiji cha Ngomboloni. Mzee Mpili ajipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni baada ya kauli yake ya ‘Sisi Tuna Watu, Hatuwezi Kufungwa na Simba’ kutafsiriwa k**a kauli iliyowapa nguvu Wana Yanga kuibuka na ushindi katika pambano la ligi kuu bara Julai 3, 2021. Mzee Mpili huonekana k**a mzee mtata na mwenye uchu wa mafanikio kwa timu yake (Yanga).

STEVE “KULIALIA”
Wakati Yanga ilipofungwa na Simba mabao 5-0 wakati fulani Steven alilia sana, akapigwa picha mbalimbali, akahojiwa na redio na televisheni huku akiwa anabubujikwa machozi, akawasimanga waamuzi kuwa ndiyo chanzo cha klabu yake kufungwa. Alipata umaarufu baada ya video zake kuzagaa mitandaoni. Leo hii Steven ni shabiki mkubwa wa Azam.

KUNZE NA DOTTO
Hawa bwana waliotrend mtandaoni na video yao moja ambapo mmoja anajichukua video akisema, "Oya, Jafe! Mbona hujatokea, sisi tunamaliza mjomba!”. Inaonekana walikuwa wakimpigia mshikaji wao ambaye hakutokea kwenye gradu, hivyo wakawa wanamuonesha mambo yalivyokuwa yamenoga. Hawa jamaa walikuja Dar kutoka kwao huko na wakajaribu kuingia kwenye uchekeshaji. Sina hakika k**a walitoboa.

KARIM MANDONGA
Miaka kadhaa iliyopita ungemwambia Karim Mandonga ‘Mtu kazi’ bondia mwenye maneno na mbwembwe nyingi wa Tanzania kwamba, angewahi kupata fursa ya kupigana kwenye ulingo nje ya nchi yake, angekubishia. Sidhani kwamba pia k**a alikuwa na ndoto au aliwaza ipo siku angekuwa bondia anayetajwa zaidi Afrika Mashariki kuliko mabondia wengine wote.

Kilichompa umaarufu Bwana Mandonga ni maneno yake mengi na misemo kadha wa kadha ambayo ilionekana kurudisha hype ya masumbwi Bongo na Afrika Mashariki. Alifikia hatua ya kumchapa bingwa wa zamani wa taji la Afica Boxing Union (ABU), Daniel Wanyonyi kwa TKO (Technical Knock Out) huko Nairobi nchini Kenya. Na Wakenya walimshangilia vibaya mno. Mandonga alikuwa anajulikana sana na kila kona alitajwa.

Ukitaja mabondia wakali na wenye rekodi za kufurahisha duniani, Karim Mandonga ‘Mtu Kazi’ hawezi kuwemo. Ukitaja mabondia wakali wa kiwango cha kufikirisha Afrika Mashariki Mandonga hayumo. Na hata ukitaja mabondia wakali watano wa Tanzania hakuwemo. Na umaarufu wake ulikuja kwa kupigwa katika moja ya mapambano yake baada ya kutamba sana kwa maneno.

Alizipa ngumi zake majina k**a vile 'ngumi mpya Sugunyo kutoka Ukraine' au ngumi ya Peresu peresu' ama ndoige'. Hivi viliwabamba wengi. Lakini pia, jamaa alikuwa anapigana mapambano mengi sana ndani ya muda mfupi.

Hata hivyo, aliitumia nafasi yake vizuri na ameonekana kwenye matangazo na promotions za bidhaa nyingi. Natumai alitumia kipindi chake kutengeneza mpunga wa kutosha. Sasa hivi hasikiki, na ninaamini anastahili kuwepo kwenye orodha hii. Je, jamaa anafanya nini sasa?

KOMANDO MADAFU WA IKULU
Mnamo tarehe 12 Machi, 2024 ambapo Rais Samia aliwaalika viongozi pamoja na makundi mbalimbali ya Kijamii kujumuika naye katika viwanja vya Ikulu kwa ajili ya kupata futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhan, walionekana vijana wawili wakiwa wanauza madafu. Vijana hao walikuja kuzua gumzo sana; wengine wakihoji k**a wale walikuwa wauza madafu halisi au walikuwa wanausalama waliojifanya wauza madafu. Hoja hizo zilisababisha mjadala mzito sana nchini. Walikuwa gumzo!

Siku chache baadaye, wakati wa kilele cha Sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Aprili, 2024, Askari mmojawa Kikundi Maalum cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alionekana akishuka kwenye Helikopta kwa ajili ya kwenda kuelezea namna mbalimbali za kwata na mapigano ya mjini. Askari huyu alifananishwa sana na muuza madafu aliyedhaniwa hapo awali kuwa ni mwanausalama wa Jamhuri. Hii ilisababisha jamaa kupata umaarufu zaidi na kufanyiwa interview nyingi na vyombo vya habari serious na vya udaku.

Kilicholeta gumzo zaidi ni pale alipotumia mameno “Ukija bila gadi (guard) nitagawa wastani kwa idadi” ambayo yalisemekana ni kauli za watu waliopita kwata fulani. Hata hivyo, kwenye mahojiano yake alisema kuwa yupo fresh kwenye michezo ya kujihami, jambo lililosababisha wengi kuamini jamaa ni mwanausalama.

Mpaka muda huu Agosti 30, 2024, umaarufu wa jamaa umeshuka na hakuna anayemzungumzia tena kwa ukubwa wa miezi minne iliyopita. Huenda akapotea kabisa midomoni mwa watu siku zijazo.

Well, nitaendelea kuongeza kwa kadiri nitakavyokumbuka na kupata wasaa wa kuongeza hii orodha.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Matukio ya Ajabu Duniani posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Matukio ya Ajabu Duniani:

Share