12/05/2025
Huyu mzee anaitwa JOAO MARINHO NETO inasadikika kwamba ndie mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani. Lilithibitishwa hilo hilo na LONGEVI QUEST huko APUIARES,CEARA nchini BRAZIL. Mzee huyo ambae ni mzaliwa wa mwaka 1912 inaelezwa ya kwamba ndie mtu pekee ambae amezaliwa miaka hiyo na ameweza kuishi mpaka leo. Mzee huyo alipohojiwa baada ya ugunduzi huo ni vipi aliweza kuishi miaka yote hiyo alijibu kwamba "nafikiri ni mipango ya MUNGU pamoja na upendo wa dhati ninaopata kutoka kwa watu wanaonizunguka, wanafanya nahisi amani na furaha wakati wote". Bila shaka mzee huyu mwenye umri wa miaka 113 anathibitisha upendo hufanya watu waishi kwa muda mrefu USHAURI "TUWAPENDE WAZEE WETU NA TUWATUNZE KWA KADRI TUNAVYOWEZA KWANI UPENDO WETU KWAO NDIO UTAWAPA MATUMAINI YA KUISHI TENA NA TENA IWE WEWE NI MJUKUU AMA MTOTO HATA JIRANI PIA HUNA BUDI KUONYESHA UPENDO KWA WATU WA AINA HII KWANI NDIO TUMAINI PEKEE AMBALO HUWA WANAKUWA WAMELIBAKIZA"...... NAJUA HUJUI ACHA NIKUJUZE.......