Fatuma Hussein Daily Updates

Fatuma Hussein Daily Updates Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Fatuma Hussein Daily Updates, Graphic designer, Kinondoni, Dar es Salaam.

05/07/2025

Je? unajua kwa kutumia Pressure cooker yetu unaweza vyakula zaidi ya 50

Tupigie kupitia nambari +255 677 088 088

Au tembelea tovuti yetu ya www.JikoPoint.co.tz ufurahie mapishi yako mchana huu.

16/06/2025

George Masaju anaingia kwenye orodha ya Watanzania wachache waliobahatika kushika nafasi ya Jaji Mkuu wa Mahak**a ya Tanzania.
Cheo hicho alichoteuliwa Masaju na Rais Samia Suluhu Hassan Juni 13 mwaka huu, ni cha juu zaidi katika mhimili wa mahak**a unaohusika na utoaji wa haki.

21/05/2025
21/05/2025

Rais wa Namibia, Netumbo Nandi, amesema kuwa kwa muda mrefu jamii imekuwa ikiwekeza zaidi kwa mtoto wa k**e, jambo ambalo sasa linaanza kuleta pengo katika maendeleo ya watoto wa kiume.
Akihutubia leo Mei 21,2025 katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, Rais Nandi amesema kuwa mtoto wa kiume anazidi kuachwa nyuma kwa sababu juhudi nyingi zimeelekezwa kwa mtoto wa k**e pekee.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha mtoto wa kiume anapewa fursa sawa ili kuepuka kizazi chenye pengo kubwa la kijinsia katika maendeleo ya kijamii na kielimu.

19/05/2025

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaonya wanaharakati wa mataifa mengine wanaojaribu kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, akisema kuwa k**a wameshadhibitiwa kwao, wasitafute kuharibu amani ya Tanzania.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatatu Mei 19, 2025, wakati wa uzinduzi wa sera mpya ya mambo ya nje (Toleo la 2024) jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache yaliojaa amani na utulivu.

“Tumeanza kuona mwenendo wa wanaharakati kuvamia mambo yetu huku. K**a kwao wameshadhibitiwa, wasije kutuharibia huku. Nchi iliyobaki haijaharibika ni yetu tusitoe nafasi kwa watovu wa adabu kutoka nchi nyingine kuja kuvuruga hapa,” amesema Rais Samia.

14/05/2025

Katika mwaka 2025/26, Wizara ya Viwanda na Biashara imepanga kuendeleza miradi ya kimkakati k**a kuwezesha uanzishwaji na uendelezaji wa viwanda nchini, kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati ya sekta.

Vipaumbele vingine ni kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma kwa kuboresha mazingira wezeshi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mitaa ya viwanda (Industrial Clusters) kwa ajili ya viwanda vidogo na vya kati pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na kuchochea ukuaji wa Sekta binafsi.

07/05/2025

Unasubiri nini kufurahia kifaa hiki

23/04/2025

Bajeti ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora yapaa kwa asilimia 25.54
Vipaumbele vya 2025/2026 ni pamoja na ajira mpya 41,500 na maboresho ya mifumo ya Tehama.
Miradi ya maendeleo kupata Sh183 bilioni.

Dar es Salaam. Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, imewasilisha bungeni ombi la kuidhinishiwa bajeti ya jumla ya Sh1.35 trilioni kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ikiwa ni ongezeko la asilimia 25.54 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi hiyo bungeni jijini Dodoma leo Aprili 23,2025, Waziri wa Nchi George Simbachawene amesema bajeti hiyo inalenga kuimarisha utendaji wa taasisi zilizo chini ya ofisi hiyo na kuandaa mazingira bora kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

“Bajeti ya mafungu yote yaliyo chini ya Ofisi ya Rais imelenga kuweka mazingira yatakayosaidia nchi kuingia katika uchaguzi na kuunda Serikali mpya kwa kuzingatia katiba, sheria na miongozo iliyopo ili kujenga imani kwa wananchi,” amesema Waziri Simbachawene.

Kwa mujibu wa waziri huyo jumla ya Sh1.17 trilioni zimetengwa kwa matumizi ya kawaida huku Sh183.3 bilioni zikiwa ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Hata hivyo, licha ya bajeti ya wizara kuongezeka kwa asilimia 25 bajeti ya miradi ya maendeleo imeongezeka kiduchu mwaka na kufikia asilimia 2.81 ya bajeti nzima.

Ofisi ya Rais Utumishi inahusisha mafungu saba ya kibajeti ambayo ni Ofisi ya Rais Ikulu (Fungu 20 na 30), Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma (Fungu 33), Menejimenti ya utumishi na utawala bora (Fungu 32), Sekretarieti ya ajira katika utumishi wa umma (Fungu 67), Tume ya utumishi wa umma (Fungu 94), na Idara ya kumbukumbu na nyaraka za taifa (Fungu 04).

Vipaumbele vya Ofisi ya Rais (Utumishi)
Katika mwaka wa fedha ujao, Ofisi ya Rais (Utumishi) imepanga kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushughulikia vibali 41,500 vya ajira mpya, kuhakiki madai ya malimbikizo ya mishahara kwa taasisi 425, kusafisha taarifa za watumishi katika mfumo wa e-Watumishi na kutekeleza miradi ya Tehama inayolenga kuboresha usimamizi wa rasilimali watu.

Shughuli nyingine ni pamoja na kukamilisha marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma (Toleo la nne), kufanya uchambuzi wa miundo ya wizara baada ya uchaguzi, kuboresha mfumo wa e-Utendaji, kuendeleza mifumo ya kushirikisha taarifa (Data sharing gateway), pamoja na kuanzisha scholarship portal kwa ajili ya fursa za ufadhili wa masomo.

Waziri Simbachawene pia ameongeza kuwa kuidhinishwa kwa bajeti hiyo kutaiwezesha Serikali kuimarisha uwajibikaji, kukuza maadili ya viongozi na watumishi wa umma na kuongeza ufanisi wa matumizi ya rasilimali za Taifa.

“Bajeti hii ni nguzo muhimu katika kuimarisha taasisi za kiutumishi, kuendeleza maadili na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi,” amefafanua Waziri Simbachawene.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa K**ati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Florent Kyombo aliyekuwa akiwasilisha mapendekezo ya k**ati hiyo ameeleza kuwa bajeti hiyo imeongezeka kwa asilimia 25.54 kutoka Sh932.8 bilioni za mwaka wa fedha 2024/2025.

“K**ati imebaini ongezeko kubwa la bajeti ya matumizi ya kawaida, hivyo ni maoni yetu kuwa Serikali ipange bajeti inayoendana na mahitaji halisi ya Taifa,” amesisitiza Kyombo.

Hata hivyo, Kyombo amesema ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa gharama za bidhaa, huduma na idadi ya watumishi wa umma.

Kuipata bidha hii original chimbo ni moja tu Tembelea JikoPoint.co.tz
22/04/2025

Kuipata bidha hii original chimbo ni moja tu

Tembelea JikoPoint.co.tz

Address

Kinondoni
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fatuma Hussein Daily Updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share