Mjamaa Digital

Mjamaa Digital Mjamaa Digital ni jukwaa la kisasa la kidijitali linalolenga kuhabarisha, kuburudisha na kuunganisha jamii kupitia maudhui bora na yenye ubora wa hali ya juu.

Tunajikita katika:
🎥 Uandaaji na usambazaji wa video za habari na matukio.

18/08/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimpokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mheshimiwa Felix Antoine Tshisekedi kwa ziara ya Kikazi leo Agosti 18,2026 Ikulu Ndogo, Zanzibar.

KAZI KUBWA IMEFANYWA NA SERIKALI KATIKA VYUO VYA ARITA NA ARIMO; MZAVADodomaKamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasil...
14/08/2026

KAZI KUBWA IMEFANYWA NA SERIKALI KATIKA VYUO VYA ARITA NA ARIMO; MZAVA

Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imepokea na kujadili taarifa ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) na Chuo cha Ardhi Mororgoro (ARIMO) ambavyo vipo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma na utendaji wa vyuo hivyo.

Kikao cha Kamati hiyo kimefanyika Agosti 14, 2026 Bungeni jijini Dodoma kulingana na ratiba iliyotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mzava.

Pamoja na michango ya wajumbe wa Kamati, Mwenyekiti wa k**ati hiyo Mhe Mzava amesema kazi kubwa imefanywa na Serikali katika kuviboresha vyuo hivyo na kusisitiza, jitihada zaidi kuendelea kuchukuliwa ili kutatua changamoto zinazojitokeza ikiwemo uboreshaji miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kwa lengo la kuandaa wataalamu wa sekta ya ardhi watakaoweza kujiajiri.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Kaspar Kaspar Mmuya amewashukuru wajumbe wa k**ati hiyo kwa maelekezo yao aliyoyaeleza kuwa, yanalenga kuboresha vyuo hivyo hatua inayosaidia kuongeza udahili wa wanachuo na kuandaa wataalamu wengi zaidi wa sekta ya ardhi nchini.

Aidha, kikao hicho cha k**ati, kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga, wajumbe wa Menejimenti ya Wizara pamoja na wawakuu wa vyuo hivyo.

13/08/2026

MMUYA AWAPA NGUVU WANAWAKE:
"SIMAMENI IMARA, MILIKINI ARDHI"

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe Timotheo Mzava (Mb...
13/08/2026

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe Timotheo Mzava (Mb) leo tarehe 13 Agosti 2026 wamekutana na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikiongozwa na Naibu Waziri wake Mhe. Kaspar Mmuya Bungeni jijini Dodoma.

Katika kikao hicho Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ilipokea na kujadili taarifa kuhusu migogoro ya ardhi nchini ikiwa ni sehemu ya jukumu la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia pamoja na kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika sekta ya ardhi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kupitia kikao hicho ilielezwa na Wizara aina za migogoro, vyanzo vyake, namna ilivyoshighulikiwa pamoja na changamoto zinazoikabili Wizara wakati wa kushughulikia migogoro hiyo. Aidha, ilielezwa namna Wizara ya Ardhi ilivyojipanga kushughulikia changamoto za sekta ya ardhi.

Kwa upande wake Kamati ya Kudumu ya Bunge kupitia Mwenyekiti wake Mhe. Mzava (Mb) ameeleza kuwa, inatambua kuwa, bado zipo changamoto nyingi kwenye sekta ya ardhi ambapo imebainisha kuwa, kutokana na hali hiyo lazima wizara iumize kichwa kuona namna bora ya kushughulikia changamoto hizo za ardhi kwa kuwa ndiyo yenye dhamana ya kusimamia sekta hiyo.

"Tunahitaji kupata mikakati madhubuti ya namna ya kuitekeleza katika kushughulikia changamoto za ardhi, ni lazima tikubaliana na tunahitaji mkakati uandaliwe ili utuongoze katika kukabiliana na changamoto za Ardhi". Amesema.

12/08/2026

YANGA BINGWA
Young Africans Sports Club

MMUYA AWAPA NGUVU WANAWAKE: “SIMAMENI IMARA, MILIKINI ARDHI”Serikali imewataka wanawake nchini kusimama imara na kutumia...
12/08/2026

MMUYA AWAPA NGUVU WANAWAKE: “SIMAMENI IMARA, MILIKINI ARDHI”

Serikali imewataka wanawake nchini kusimama imara na kutumia fursa zilizopo kisheria kupata, kumiliki na kutumia ardhi kwa usalama, ikisema umiliki salama wa ardhi ni msingi muhimu wa uwezeshaji wa wanawake, ustawi wa familia na maendeleo ya jamii.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 12, 2026, na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, wakati akizungumza katika Kongamano la Kampeni ya “Linda Ardhi ya Mwanamke (Stand for Her Land)” linalofanyika jijini Dodoma.

Mhe. Mmuya amesema ardhi si rasilimali ya kiuchumi pekee, bali ni msingi wa maisha, maendeleo, usalama wa familia na ustawi wa jamii, hivyo wanawake wanapaswa kuwa na nafasi sawa katika umiliki na kufanya maamuzi kuhusu ardhi.

Amesema Serikali imeweka misingi ya kisheria inayolinda haki za wanawake katika masuala ya ardhi kupitia Sheria ya Ardhi, Sura ya 113 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji, Sura ya 114, akisisitiza kuwa hakuna mila, desturi au taratibu zinazopaswa kutumika kumnyima mwanamke haki yake ya kumiliki, kutumia na kunufaika na ardhi kwa mujibu wa sheria.

Ameongeza kuwa mwanamke mwenye ardhi salama anaweza kuitumia kwa shughuli za kilimo, biashara na uwekezaji, pamoja na kuitumia k**a dhamana ya kupata mikopo pale inapokubalika kisheria, kujenga nyumba na kuweka msingi bora wa maisha ya familia.

Aidha, Mhe. Mmuya amewataka viongozi wa Serikali za Mitaa, viongozi wa vijiji, viongozi wa kimila na wadau wa sekta ya ardhi kuhakikisha wanawake wanashirikishwa kikamilifu katika maamuzi yanayohusu ardhi, huku akiwataka wanawake kuongeza uelewa kuhusu haki zao na taratibu za kisheria za kulinda milki zao.

Kongamano hilo la Kampeni ya “Linda Ardhi ya Mwanamke” limewakutanisha viongozi wa Serikali, wataalamu wa ardhi, wadau wa maendeleo na viongozi wa wanawake, likiwa na kauli mbiu isemayo “Imarisha Haki na Milki Salama za Ardhi na Hatua za Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi kupitia Uongozi wa Wanawake wa Ngazi ya Jamii.”

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MABARAZA YA ARDHIDODOMAKamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imekutana le...
12/08/2026

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MABARAZA YA ARDHI

DODOMA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imekutana leo tarehe 12 Agosti 2026 Bungeni jijini Dodoma kupokea na kujadili taarifa kuhusu utendaji wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, ikiwa ni sehemu ya jukumu la Bunge la kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika sekta ya ardhi.

Katika kikao hicho, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeieleza Kamati hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika kuboresha utendaji wa Mabaraza hayo, ambayo yako chini ya Wizara hiyo.

Miongoni mwa hatua zilizobainishwa ni kuongezeka kwa idadi ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, kupungua kwa mashauri na malalamiko, kuimarishwa kwa matumizi ya mifumo ya kidijiti pamoja na kuboreshwa kwa mfumo wa uendeshaji wa shughuli za madalali.

Pamoja na mafanikio hayo, Kamati imeelezwa kuwa bado zipo changamoto kadhaa zinazoathiri utendaji wa Mabaraza hayo na kwamba Wizara inaendelea kuzifanyia kazi ili kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amewaeleza wajumbe wa Kamati kuwa, Serikali inaendelea kushughulikia changamoto zinazoyakabili Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, akieleza kuwa kutatuliwa kwa changamoto hizo kutasaidia kuyafanya Mabaraza kuwa bora zaidi na yenye manufaa makubwa kwa wananchi.

Awali, wajumbe wa Kamati wameitaka Wizara kuweka mkazo zaidi katika matumizi ya usuluhishi wakati wa kushughulikia migogoro ya ardhi badala ya kila shauri kulenga kupata mshindi na mshindwa.

Wamesema, usuluhishi unaweza kusaidia kupunguza migogoro, kuharakisha utatuzi wa mashauri na kujenga mahusiano mazuri miongoni mwa wananchi.

Wajumbe hao wameeleza kuwa, pamoja na mafanikio yanayoonekana katika utendaji wa Mabaraza, bado ipo haja ya Wizara kuchukua hatua za haraka kukabiliana na changamoto zilizopo ili Mabaraza hayo yaweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuendelea kujenga imani ya wananchi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Timotheo Mzava, amesisitiza umuhimu wa Wizara kuongeza idadi ya wenyeviti wa Mabaraza, kupanua upatikanaji wa Mabaraza katika wilaya mbalimbali pamoja na kukamilisha mfu

KAMATI YA BUNGE YAPOKEA TAARIFA YA WIZARA YA ARDHIKamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utali, ikiongozwa na ...
12/08/2026

KAMATI YA BUNGE YAPOKEA TAARIFA YA WIZARA YA ARDHI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utali, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Timotheo Mnzava, leo tarehe 11 Agosti 2026 bungeni jijini Dodoma imekutana na watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiongozwa na Naibu Waziri, Mhe. Kaspar Mmuya, kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa kuhusu utendaji na usimamizi wa watumishi wa kada ya ardhi pamoja na hatua zilizofikiwa atika uanzishaji wa Kamisheni ya Ardhi.

Katika kikao hicho, Wizara imeieleza Kamati hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kuimarisha usimamizi wa watumishi wa sekta ya ardhi, kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kukabiliana na changamoto majukumu ya sekta hiyo.

Kikao hicho kimefanyika Bungeni Jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya usimamizi wa Bunge katika kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Serikali katika sekta ya ardhi.

Naibu Katibu Mkuu Bi Lucy Kabyemera, wajumbe wa Menejimenti ya Wizara pamoja na wakuu wa Taasisi zikizochini ya wizara pia walishiriki katika kikao hicho.

11/08/2026

Macho kwenye video

09/08/2026

MMUYA: NDEGE NYUKI KUTUMIKA KUPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amesema Serikali imeanza maandalizi ya kuingiza matumizi ya teknolojia za kisasa katika upimaji wa ardhi, ikiwemo teknolojia ya ndege nyuki, kwa lengo la kuongeza kasi ya upimaji na upatikanaji wa taarifa sahihi za ardhi nchini.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha kila kipande cha ardhi nchini kinapimwa na kuwa na taarifa sahihi.

Mhe. Mmuya amesema katika kujiandaa na matumizi ya teknolojia hiyo, Wizara imeanzisha Chuo cha Taifa cha Ubunifu wa Taarifa za Kijiografia (TNGC), kitakachosaidia kuandaa wataalamu wenye ujuzi wa teknolojia za kisasa za upimaji na ukusanyaji wa taarifa za kijiografia.

Amesema baada ya wataalamu hao kupata ujuzi unaohitajika, teknolojia hiyo itakuwa na nafasi kubwa katika kuongeza ufanisi wa upimaji wa ardhi, kutambua mipaka na maeneo kwa usahihi na hatimaye kusaidia kupunguza migogoro ya ardhi nchini.

Mhe. Mmuya amesema hayo leo Agosti 8, 2026, alipotembelea banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane 2026, yaliyofanyika katika Viwanja vya Maonesho ya Kilimo vya Dkt. John Malecela, jijini Dodoma.

Ameongeza kuwa uwekezaji huo katika elimu, wataalamu na teknolojia ni sehemu ya maandalizi ya Serikali ya kujenga uwezo wa ndani wa kukabiliana na changamoto za upimaji wa ardhi na kuimarisha usalama wa umiliki wa ardhi kwa wananchi.

Address

Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mjamaa Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share