22/07/2026
Karibu KUSINI,
Kwa miaka mingi, Nyanda Za Juu Kusini imekuwa ikisifika kuhusu mambo mbalimbali, Imesifika kwa Kilimo, Utalii, Mila na Desturi, Hali ya hewa nzuri na Historia tamu.
Lakini ni nani anaeweza kuzungumzia vizuri zaidi na kwa undani zaidi pamoja na kusogeza kwa karibu kabisa mambo yote mazuri yanayopatikana katika Mikoa ya Nyanda za juu kusini?
KUSINI PAZURI, Ni jukwaa maalum ambalo linatoa fursa ya kukusogezea wewe karibu mema na mazuri yote yanayopatikana Nyanda Za Juu Kusini, lakini kukosoa na kupaza sauti kwenye yale yote yanayohitajika kufanyiwa marekebisho kwa faida ya wananchi.
Bila kusahau burudani na matukio maalum yanayoendelea kwenye mikoa yetu.
Hapa utapata nafasi ya kusikia kutoka kwa viongozi na watu mashuhuri wa Nyanda Za Juu Kusini, pamoja na kukuonesha mazingira yote mazuri bila kusahau fursa za biashara, ajira na uwekezaji.
Hakikisha una βSUBSCRIBEβ kwenye Youtube Channel yetu, na kutufuata kwenye mitandao mengine k**a vile TikTok na Instagram.
KUSINI PAZURI βUnveiling The Soul Of The Southβ