23/09/2025
🚨Ila Simba 🙌, timu ina mchezo wa ligi Jumatano tarehe 25 (yaani kesho kutwa), ila Meneja wa Habari anajigamba kuwa timu imepewa siku mbili za mapumziko na mashabiki wamelipokea kwa mikono miwili kana kwamba ni habari njema.
✍️Timu bado inapata matokeo kwa shida na haijakaa sawa. Ndani ya wiki moja pekee, Simba ina michezo miwili mikubwa tarehe 25 na 28, ila wachezaji bado wanapewa mapumziko. Swali linabaki: muda wa kuandaa kikosi upo wapi ikiwa timu haijatulia?
✍️Yanga wapinzani wao wamecheza Yanga Day, wakaingia moja kwa moja kwenye Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, kisha wakasafiri kwenda Angola. Wamerudi na kuunganishwa moja kwa moja na maandalizi ya ligi. Pamoja na msongamano huo, wachezaji wao wameonyesha kuungana na matokeo yanaonekana wameshinda mechi zote. Hata k**a muda ni mfupi, bado wanakaza na hawalalamiki kupumzika.
✍️Kesho Yanga ikisifiwa, mashabiki wa Simba badala ya kuangalia udhaifu wa timu yao, wanatukana na kulalamika kuwa Yanga inapendelewa.
✍️Wakati mwingine, ni lazima ninyi wenyewe muone aibu jinsi timu yenu inavyoendeshwa juu juu, kwa presha bila mpangilio.
Mtanikumbuka ✍️
✍️KALAMU YA USHAHIDI
Ndimi