Fad designer

Fad designer Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Fad designer, Mafichoni, Manyara.

Islamic Reminder
Ujumbe wa Imani, Mwanga wa Moyo

Karibu kwenye Farida Islamic Reminder, kituo cha kupata mafundisho sahihi ya Kiislamu, dondoo za Qurโ€™an, Hadithi za Mtume ๏ทบ, nasaha za kimaisha, dua, na ukumbusho wa kila siku unaoujenga moyo na kuutuliza.

Tupendane kwa ajili ya Allah, tutembeleane, tukae pamoja katika kheri, na tusaidiane kwa ajili Yake.Allah atujaalie tuwe...
15/08/2026

Tupendane kwa ajili ya Allah, tutembeleane, tukae pamoja katika kheri, na tusaidiane kwa ajili Yake.

Allah atujaalie tuwe miongoni mwa wale wanaopendwa na Yeye. ๐Ÿคฒ๐Ÿฝ

Ungana nasi katika channeli yetu kupata Faida zaidi
https://whatsapp.com/channel/0029Vb60V3jIHphNTJGsUm3p

07/06/2026

ULIMI WAKO NI AMANA ๐Ÿ—ฃ๏ธ

Maneno yana uwezo wa kujenga au kubomoa.

Neno moja jema linaweza kuponya moyo uliovunjika, na neno moja baya linaweza kuacha jeraha la muda mrefu.

Kabla hujanena, jiulize: Je, maneno yangu yana manufaa? Je, yatamridhisha Allah? Je, yatamfurahisha au kumuumiza mwenzangu?

Wakati mwingine ukimya huwa ni hekima kuliko maneno mengi.

๐ŸŒน Kumbuka: Muumini wa kweli huchagua maneno yake kwa uangalifu, kwa sababu anajua kila analolisema linaandikwa.

Tujifunze kuzungumza kwa upole, ukweli, na heshima, kwani tabia njema huanza na ulimi mwema.

Mwenye kumuamini Allah na Siku ya Mwisho, basi aseme yaliyo mema au anyamaze.

02/06/2026

๐Ÿ•Œ FADHILA YA BAITUL MAQDIS ๐Ÿ•Œ

Mtume Muhammad ๏ทบ amesema kuwa Nabii Sulaiman bin Daud (A.S.) alipomaliza kujenga Baitul Maqdis, alimuomba Allah mambo matatu:

โœจ Hekima na uamuzi unaolingana na haki ya Allah.
โœจ Ufalme wa kipekee ambao hakuna atakayekuwa nao baada yake.
โœจ Na kwamba yeyote atakayekwenda kuswali katika msikiti huo kwa ikhlasi, atoke akiwa ametakaswa madhambi k**a siku aliyozaliwa na mama yake.

๐Ÿ“– Rejea: Sunan Ibn Majah, Hadithi Na. 1408 (Sahih)

Hadithi hii inatukumbusha umuhimu wa ibada ya kweli, ikhlasi katika kumuabudu Allah, na fadhila kubwa za sehemu tukufu za ibada.

Ewe Allah! Tujalie ikhlasi katika ibada zetu, tusamehe madhambi yetu, na utujaalie kuwa miongoni mwa wenye kupata rehema na maghfira Yako. Aamiin.

๐ŸŒฟ Hakika mafanikio ya kweli ni kupata radhi za Allah na msamaha Wake. ๐ŸŒฟ

30/05/2026

TANBIHI YA LEO

Allah anajua maumivu ambayo hukuyasema kwa mtu yeyote.

Endelea kumuomba kwa siri, kwani Yeye husikia hata sauti za mioyo. ๐ŸŒธ

๐Ÿ–‹๏ธ๐Ÿ–‹๏ธ Fad designer

27/05/2026

EID MUBARAK

Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh

Familia ya Farida Islamic Reminder tunawatakia nyote Eid Mubarak yenye furaha, amani na baraka nyingi kutoka kwa Allah ๏ทป.
Allah azikubali ibada zetu, dua zetu na sadaka zetu, na atujaalie kuwa miongoni mwa wenye kufaulu duniani na Akhera. ๐Ÿคฒ

Katika siku hii tukufu, tuendelee kupendana, kusameheana na kusaidiana kwa ajili ya Allah.
Furaha ya Eid iwe mwanzo wa kheri mpya katika maisha yetu. ๐ŸŒธ

ุชูŽู‚ูŽุจู‘ูŽู„ูŽ ุงู„ู„ู‘ูŽู‡ู ู…ูู†ู‘ูŽุง ูˆูŽู…ูู†ูƒูู…ู’ ุตูŽุงู„ูุญูŽ ุงู„ุฃูŽุนู’ู…ูŽุงู„ู
Allah akubali mema yetu na yenu.

Eid Mubarak to you and your family!

https://whatsapp.com/channel/0029Vb60V3jIHphNTJGsUm3p

Eid ni wakati wa kujitoa kwa ajili ya Allah, kuonyesha shukrani na kuwasaidia wenye uhitaji.K**a Allah amekujaalia uwezo...
25/05/2026

Eid ni wakati wa kujitoa kwa ajili ya Allah, kuonyesha shukrani na kuwasaidia wenye uhitaji.

K**a Allah amekujaalia uwezo, basi usikose kushiriki ibada hii tukufu ya kuchinja.

Tuifanye Eid yetu iwe yenye ibada, upendo na kusaidiana.

24/05/2026

TANBIHI YA LEO

Kila ninapochoka, namkumbuka Allah na moyo wangu hupata utulivu.๐ŸŒธ

Utulivu wa kweli haupatikani kwa dunia, bali kwa kumkumbuka Allah.

๐Ÿ–‹๏ธ๐Ÿ–‹๏ธFad designer

23/05/2026

Nimejifunza kumtegemea Allah zaidi kuliko hofu zangu, maana rehema Zake hazina mwisho

๐Ÿ–‹๏ธ๐Ÿ–‹๏ธFad designer

Address

Mafichoni
Manyara

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Fad designer posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share