Habari za Zanzibar

Habari za Zanzibar Ukurasa utakaokupa habari mbalimbali kutoka Zanzibar na Ulimwenguni kote.

๐—ง๐—ฎ๐—ป๐˜‡๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ฎ - ๐—ฉ๐—ถ๐—ฒ๐˜๐—ป๐—ฎ๐—บ ๐—•๐˜‚๐˜€๐—ถ๐—ป๐—ฒ๐˜€๐˜€ ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ ๐—œ๐—ป๐˜ƒ๐—ฒ๐˜€๐˜๐—บ๐—ฒ๐—ป๐˜ ๐—™๐—ผ๐—ฟ๐˜‚๐—บStrengthening parternship, unlocking opportunities driving sustainable g...
14/08/2026

๐—ง๐—ฎ๐—ป๐˜‡๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ฎ - ๐—ฉ๐—ถ๐—ฒ๐˜๐—ป๐—ฎ๐—บ ๐—•๐˜‚๐˜€๐—ถ๐—ป๐—ฒ๐˜€๐˜€ ๐—ฎ๐—ป๐—ฑ ๐—œ๐—ป๐˜ƒ๐—ฒ๐˜€๐˜๐—บ๐—ฒ๐—ป๐˜ ๐—™๐—ผ๐—ฟ๐˜‚๐—บ

Strengthening parternship, unlocking opportunities driving sustainable growth

Focus Areas
- Textile
- Agro - processing
- Pharmaceuticals
- Sez Development
- Leather
- Blue Economy

Save the Date
๐Ÿ“† 3 - 4 September, 2026.
๐Ÿ“Ho Chi Minh Vietnam

For more Information, Contact +255679205203

Tanzania na Ujerumani Kuendeleza Ushirikiano katika Sekta za KimkakatiJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shir...
14/08/2026

Tanzania na Ujerumani Kuendeleza Ushirikiano katika Sekta za Kimkakati

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani zimekubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimkakati, ikiwemo biashara na uwekezaji, afya, mazingira, maji, uchumi wa buluu, ujenzi wa miundombinu, teknolojia na utawala bora, kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Hayo yamejili leo, Agosti 13, 2026, jijini Dodoma wakati wa mazungumzo kati ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na ujumbe kutoka Ujerumani. Kwa upande wa Tanzania yameongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo, na Katibu Mkuu Balozi Dkt. Samwel Shelukindo huku kwa upande wa Ujerumani yakiongozwa na Mkuu wa Kitengo kinachoshughulikia masuala ya Afrika katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo Mhe. Joachim Schmitt.

Akizungumza na ujumbe huo, Waziri Dkt. Kombo na Katibu Mkuu Balozi Dkt. Shelukindo wamepongeza mchango wa Ujerumani katika shughuli mbalimbali za maendeleo nchini Tanzania, huku wakisisitiza utayari wa Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na Ujerumani katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kuboresha ustawi wa wananchi.

Kwa upande wake, Mhe. Schmitt amesema Ujerumani inaendelea kuiona Tanzania kuwa mshirika muhimu wa maendeleo barani Afrika na imedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Ameeleza kuwa Serikali ya Ujerumani iko tayari kutazama maeneo mapya ya ushirikiano yanayoendana na mahitaji na fursa zilizopo, ikiwemo teknolojia, ulinzi na usalama pamoja na uchumi wa kidijitali.

Ujerumani ni miongoni mwa nchi kumi zinazoongoza kwa uwekezaji wa kigeni nchini Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), kufikia Oktoba 2025, miradi 187 ya uwekezaji kutoka Ujerumani ilikuwa imesajiliwa nchini, ikiwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 535.63 na kutoa fursa za ajira taktribani 16,427 katika sekta mbalimbali za uchumi.

Ushirikiano huo unaakisi uhusiano wa muda mrefu na unaoendelea kukua kati ya Tanzania na Ujerumani, huku pande zote zikilenga kuutumia k**a msingi wa kukuza biashara na uwekezaji, kuhamasisha maendeleo endelevu na kuongeza fursa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.

MHE. BALOZI OMAR: AIMWAGIA SIFA TRA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANIWaziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb), am...
13/08/2026

MHE. BALOZI OMAR: AIMWAGIA SIFA TRA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb), ameimwagia sifa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA kwa utendaji uliotukuka uliowezesha Mamlaka hiyo kuendelea kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kila mwezi na kueleza imani yake kwamba kwa kushirikiana na walipakodi, wataweza kuvuka lengo walilopangiwa la kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 42 katika Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Mhe. Balozi Omar, ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya TRA, Kizimkazi, Zanzibar, litakalokuwa na ghorofa moja, ambapo hadi kukamilika kwake linatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 3.6.

Sifa hizo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, zinafuatia maelezo ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA Bw. Yusuph Mwenda ambapo alisema katika mwezi Julai mwaka huu, Mamlaka yake imevuka malengo kwa kukusanya shilingi trilioni 3.2 ikilinganishwa na malengo waliyopangiwa ya kukusanya shilingi trilioni 2.

Alisema kuwa mafanikio ya TRA katika ukusanyaji wa mapato yanatokana na ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, Bunge na wadau wa kodi, ambapo mwezi Julai pekee, Mamlaka ilikusanya zaidi ya Shilingi trilioni 3.245 ikilinganishwa na lengo la mwezi la kukusanya shilingi trilioni 2.971, sawa na ufanisi wa asilimia 109 ya lengo, na ukuaji wa asilimia 21.

โ€œKutokana na usimamizi wako mzuri Mhe. Waziri wa Fedha, na ushirikiano na walipakodi, tunakuhakikishia tutavuka lengo hilo na kupita, ishara inayoonesha kwamba tumeanza mwaka wa fedha kwa nguvu kubwa, na tuna imani tutafikia na kuvuka malengo tuliyowekewaโ€ alisema Bw. Mwenda.

Aidha, CPA Mwenda alisema kuwa katika kipindi hicho cha Julai, 2026, TRA imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 325, fedha mabazo ni asilimia 70 ya makusanyo yote na kuzipeleka moja kwa moja kwenye Mifuko 11 ya ujenzi wa miundombinu katika sekta mbalimbali zikiwemo Barabara, maji, utalii na sekta nyingne.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa Ofisi za TRA, Kizimkazi-Unguja Zanzibar inayojengwa na Kampuni ya CRJE ya China, ni sehemu ya ujenzi wa Ofisi k**a hizo 49 zinazojengwa nchi nzima zikitarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 32 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya ulipaji kodi na kusogeza huduma karibu na wananchi.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb) aliwahakikishia watanzania kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha kuwa inajitegemea kwa kutumia mapato yake ya ndani kutekeleza miradi yake ya maendeleo ambapo katika Mwaka wa Fedha 2026/2027, imepanga kujitegemea kwa zaidi ya asilimia 74.

Alisema kuwa ujenzi wa Ofisi za TRA Kizimkazi na maeneo mengine nchini, ni mikakati ya Serikali ya kuimarisha huduma, kurahisisha shughuli za biashara, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato na kuwawezesha watumishi kufanya kazi katika mazingira bora kwa ajili ya kuongeza mapato yanayowezesha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, nishati, maji, kuimarisha huduma za afya na kuwekeza katika elimu.

Mhe. Balozi Omar ameuagiza Uongozi wa TRA kuhakikisha kuwa wanashirikiana na Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA kutumia miundombinu ya Ofisi hizo na nyingine zitakazo jengwa Visiwani Zanzibar, ili wadau wa kodi wapate huduma kikamilifu, jambo ambalo Kamishna wa TRA Bw. Mwenda aliahidi kulifanyia kazi.

Aidha aliwataka wafanyabiashara na wananchi kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa wakati, kwa ukamilifu na kwa hiari, akisisitiza kuwa ulipaji wa kodi unapaswa kuwa jambo la fahari kwa kila mwananchi anayewajibika na Serikali itaendelea kushirikiana na wafanyabiashara katika kuboresha huduma za kodi na kupunguza changamoto zinazowakabili, huku ikitarajia wafanyabiashara nao kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini, Mhe. Othman Ali Maulid, alitoa wito kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA) kuendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi na kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa wananchi, lakini pia kusikiliza changamoto za wananchi na wafanyabiashara.

Akiongea kwa niaba ya Wafanyabishara wa sekta ya hoteli na utalii Zanzibar, Bw. Henry Kaunda, aliishukuru TRA na ZRA kwa kushirikina na wafanyabiashara na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hatua iliyochangia ulipaji kodi kwa hiari na kuomba elimu zaidi ya mlipakodi iendelee kutolewa kwa wafanyabiashara.

TABASAMU HILI LA WAZIRI MKUU NA SHABIKI WA SIMBA LILIKUWA MBELE YA MUDA SANAA!Mashabiki wa soka ebu tujiulize hivi lile ...
13/08/2026

TABASAMU HILI LA WAZIRI MKUU NA SHABIKI WA SIMBA LILIKUWA MBELE YA MUDA SANAA!

Mashabiki wa soka ebu tujiulize hivi lile tabasamu la shabiki wa Simba na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba pale Nanenane Morogoro lilikuwa la kawaida tu, au Mheshimiwa Dkt. Mwigulu alikuwa tayari anajua yatakayotokea pale New Amani Complex Zanzibar ? ๐Ÿ˜‚

Lakini mpira ni furaha, ushindani na utani. Leo Yanga anacheka, kesho inaweza kuwa zamu ya Simba.

KITUO KIPYA CHA MIKUTANO ARUSHA KUHUDUMIA WATU 5000 KWA WAKATI MMOJA-WAZIRI KOMBOWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano w...
12/08/2026

KITUO KIPYA CHA MIKUTANO ARUSHA KUHUDUMIA WATU 5000 KWA WAKATI MMOJA-WAZIRI KOMBO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amesema kuwa, ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Mlima Kilimanjaro (MK-ICC) jijini Arusha, utaongeza uwezo wa Tanzania katika kuandaa mikutano ya kitaifa, kikanda na kimataifa kwa kuondoa changamoto ya muda mrefu ya nchi ya kutokuwa na kumbi za kubeba watu wengi kwa wakati mmoja.

Waziri Kombo ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) chini ya mwenyekiti wake, Mhe. Najma Murtaza Giga (Mb) na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma Agosti 12, 2026.

Balozi Kombo alieleza kuwa ujenzi huo ni utekelezaji wa vitendo wa Diplomasia ya Uchumi kupitia utalii wa mikutano; kuvutia uwekezaji wa ndani na nje; kuongeza ajira; kuvutia utalii; kuongeza mapato ya Serikali; kuongeza mapato ya fedha za kigeni na kuchochea maendeleo ya sekta za utalii, biashara, huduma na usafiri.

Kituo hicho kinachojengwa kwa ushirikiano kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) kinahusisha ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa kisasa unaijumuisha, ukumbi mkuu wa mikutano wenye uwezo wa kuhudumia washiriki 5,000; kumbi ndogo za mikutano zenye uwezo wa kuhudumia washiriki kati ya 30 hadi 500; ukumbi wa hadhi ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa wenye uwezo wa kuhudumia watu 300, ukumbi wa maonesho wenye eneo la uwezo wa kuhudumia washiriki 10,000 na jengo la utawala.

Vilevile kutakuwa na hoteli ya nyota tano yenye vyumba 500; eneo la maegesho ya magari yenye uwezo wa kuhudumia magari 2,000; pamoja na miundombinu yote ya nje inayohitajika kwa uendeshaji wa Kituo hicho yenye jumla ya ukubwa wa mita za mraba 50,000.

Kwa upande wao wajumbe walipongeza ujenzi huo na kubainisha kuwa utakuwa alama kwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Aidha, waliitaka Wizara kupitia AICC kujipanga vyema ili kituo hicho kiweze kutoa huduma bora na kukifanya kuwa shindani duniani.

12/08/2026

Nukuu za Waziri Mkuu katika Sekta ya Afya

MHE. BALOZI OMAR: MBEYA INA FURSA KUBWA YA KUONGEZA MCHANGO WAKE KATIKA UCHUMI WA TAIFAWaziri wa Fedha, Mhe. Balozi Kham...
12/08/2026

MHE. BALOZI OMAR: MBEYA INA FURSA KUBWA YA KUONGEZA MCHANGO WAKE KATIKA UCHUMI WA TAIFA

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb), amesema Mkoa wa Mbeya na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini yana fursa kubwa ya kuongeza mchango wake katika uchumi wa Tanzania kwa kuimarisha uzalishaji, kuongeza thamani ya mazao na kukuza shughuli za viwanda.

Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipokuwa akizungumza wakati alipotembelea Ofisi za Mkoa za Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Mbeya, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo.

Alieleza kuwa eneo la Nyanda za Juu Kusini linachukua takribani asilimia 20 ya eneo lote la Tanzania, lakini mchango wake katika pato la Taifa bado haujaendana kikamilifu na ukubwa wa eneo na fursa zilizopo.

Mhe. Balozi Omar alisema hali hiyo inaonesha kuwa bado kuna nafasi kubwa ya kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo, madini, viwanda na sekta nyingine za uzalishaji ili Mkoa wa Mbeya na Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla uwe na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa Taifa.

โ€œBado tuna fursa kubwa sana ya kuimarisha mchango wetu katika pato la Taifa uendane na eneo tulilonalo, na si kwa sababu hatuna fursa,โ€ alisema Mhe. Balozi Omar.

Aidha, katika kusisitiza uchakataji wa mazao, alisema kuwa Serikali itaendela kuweka mkazo mkubwa katika kuongeza thamani ya mazao ndani ya nchi ili nchi iondokane na mfumo wa kuzalisha mazao na kuyauza bila kuyachakata, hatua ambayo itasaidia kuongeza ajira, mapato kwa wananchi na mapato ya Serikali, huku ikiiwezesha Tanzania kunufaika zaidi na mnyororo mzima wa thamani wa bidhaa zinazozalishwa nchini.

โ€œMsisitizo wetu uwe kwenye mnyororo wa thamani, Tunaweza kulima, kuvuna na kuuza mazao, lakini tunahitaji kuwa sehemu kubwa zaidi ya mnyororo wa thamani kwa kuhakikisha uchakataji unafanyika hapa nchini,โ€ alisema Mhe. Balozi Omar.

Alisema badala ya Tanzania kubaki katika hatua za awali za uzalishaji na kuuza malighafi, ni muhimu kuongeza uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mazao ili bidhaa zinazotokana na rasilimali za Tanzania ziweze kuzalishwa nchini na kuuzwa katika masoko ya ndani na nje na hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira, mapato ya wananchi na Serikali, pamoja na kuchochea ukuaji wa viwanda na kuongeza ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Akizungumzia shughuli za uchimbaji wa madini mkoani Mbeya, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa mazingira na afya za wachimbaji pamoja na wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka shughuli za uchimbaji, kwa kuwa pamoja na manufaa ya kiuchumi yanayotokana na uchimbaji wa madini, Serikali inapaswa kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia usalama wa afya za watu na mazingira.

Kuhusu changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika Wilayani Chunya, Mhe. Balozi Omar alisema kuwa Serikali itafanya jitihada ya kuboresha miundombinu ya umeme utakaowezesha uchimbaji na uzalishaji wa dhahabu ufanyike kwa ufanisi na kuongeza tija kwa wananchi na mapato ya Serikali kwa ujumla.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Patrick Mwalunenge, alisema Mkoa huo una uwezo mkubwa wa kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa kupitia sekta za uzalishaji, hususan kilimo, viwanda na biashara.

Mhe. Mwalunenge alisema kuwa Mbeya inaendelea kuwa miongoni mwa maeneo muhimu ya uzalishaji wa mazao ya biashara k**a chai, kahawa na kakao, hivyo kuna umuhimu wa kuweka mazingira yatakayowezesha wakulima kupata masoko ya uhakika pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya kuchakata mazao hayo.

โ€œNasisitiza Serikali ione umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya biashara na viwanda, ikiwemo ujenzi wa bandari kavu na kongani za viwanda, ili kuifanya Mbeya kuwa kitovu cha biashara na uzalishaji kwa Nyanda za Juu Kusini na nchi jirani, kwa kuwa nafasi ya kijiografia ya Mbeya, pamoja na uzalishaji mkubwa wa kilimo katika Nyanda za Juu Kusini, inatoa fursa ya kuunganisha uzalishaji, uchakataji na masoko ya ndani na nje ya nchiโ€ aliongeza Mhe. Mwalunenge.

Naye Mbunge wa Jimbo la Lupa-Chunya, Mhe. Masache Kasaka, alisema utekelezaji wa miradi ya maendeleo na upatikanaji wa fedha kwa wakati ni muhimu katika kuongeza kasi ya shughuli za uzalishaji na kuimarisha uchumi wa Mkoa wa Mbeya.

Mhe. Kasaka alisema Chunya ina mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa kupitia uzalishaji wa dhahabu na tumbaku, huku akieleza kuwa wilaya hiyo inaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu miongoni mwa wachimbaji wadogo nchini, ikizalisha wastani wa kilo 400 kwa mwezi ambapo k**a Serikali itaboresha upatikanaji wa umeme katika maeneo ya uzalishaji kutasaidia kuongeza uzalishaji wa dhahabu na kuchochea shughuli nyingine za kiuchumi.

โ€œChunya ina fursa kubwa katika uzalishaji wa tumbaku, ambapo licha ya kilimo hicho kufanyika katika eneo dogo ukilinganisha na mikoa mingine, wilaya yetu imeendelea kuwa miongoni mwa wazalishaji muhimu na k**a kutaimarishwa kwa miundombinu ya umeme, maji na barabara, pamoja na kukamilishwa kwa miradi inayotekelezwa, kutasaidia wananchi kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika sekta za uzalishajiโ€ alisema Mhe. Kasaka.

12/08/2026

Uhuru wa kujieleza ni haki ya kila mtu, lakini uhuru huo haupaswi kuwa sababu ya kumvunjia mtu au viongozi heshima. Tunaweza kukosoa, kuuliza na kutoa maoni kwa nguvu ya hoja, bila matusi, dharau au chuki. Tujenge utamaduni wa kuheshimiana tunapotoa maoni. Je, tunaweza kutofautiana bila kudhalilishana?โ€

Tanzania na Marekani zimeendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika sekta mbalimbali zikiw...
12/08/2026

Tanzania na Marekani zimeendelea kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika sekta mbalimbali zikiwemo madini adimu, nishati, afya, uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi, pamoja na dhamira ya kuendeleza mazungumzo na ushirikiano wa kitaalamu kwa manufaa ya nchi hizo mbili.

Hayo yameafikiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb) na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew Lentz, walipokutana na kufanya mazungumzo ya katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam, ambapo pia walieleza umuhimu wa kuendelea kutumia majadiliano ya kitaalamu na ushirikiano wa Serikali kwa Serikali katika kushughulikia maeneo yenye umuhimu wa kimkakati, ikiwemo maendeleo ya sekta ya Nishati ya Gesi Asilia (Liquefied Natural Gas (LNG).

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Andrew Lentz, alisisitiza kuwa mawasiliano ya karibu na ushirikiano kati ya wataalamu wa pande zote ni muhimu katika kuwezesha utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati.

Aidha, walijadili fursa za kuendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini, ikiwemo miradi mikubwa ya madini na kuongeza thamani ya rasilimali nchini, ambapo walikubaliana kuhusu umuhimu wa kuwa na uratibu mzuri wa Serikali na wawekezaji ili kuhakikisha miradi ya kimkakati inatekelezwa kwa ufanisi na kutoa manufaa kwa uchumi na wananchi.

Kwa upande wa afya, alisema kuwa hivi karibuni, Marekani na Tanzaniaa zimesaini makubaliano ya kuendeleza sekta ya afya yatakayogharimu dola za Marekani bilioni 3.1 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya afya, kukabiliana na magonjwa mbalimbali na kujenga uwezo wa ndani, kuelekea kwenye mifumo endelevu ya afya inayoongeza uwezo wa Tanzania kugharamia na kusimamia huduma za afya kwa muda mrefu, sambamba na kuimarisha uwezo wa kitaifa katika kinga, ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa.

โ€œTunatambua umuhimu wa uwekezaji katika miundombinu ya afya, uzalishaji wa bidhaa za afya nchini na kuimarisha taasisi zinazohusika na afya ya umma na Ushirikiano huu unalenga kuongeza uwezo wa Tanzania kukabiliana na changamoto za kiafya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na endelevuโ€ alisema Mhe. Balozi Lentz.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NI KIUNGO MUHIMU KATIKA MAFANIKIO YA SERIKALI - WAZIRI KOMBOWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano...
11/08/2026

WIZARA YA MAMBO YA NJE NI KIUNGO MUHIMU KATIKA MAFANIKIO YA SERIKALI - WAZIRI KOMBO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema kuwa Wizara kupitia Balozi zake duniani imekuwa kiungo muhimu cha kufanikisha na kuchochea mafanikio ya Serikali katika sekta zote nchini, iwe kilimo, uchukuzi, biashara au nishati.

Waziri Kombo amesema hayo wakati wa kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) na Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Najma Murtaza Giga Katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma Agosti 11, 2026.

โ€œKwa ufupi balozi zetu zinahusika na kila chembe ya mafanikio yanayoonekana hapa nchini ikiwemo upatikanaji wa fedha za ujenzi wa miundombinu k**a vile reli ya kisasa, ununuzi wa ndege, upatikanaji wa vibali vya safari za ATCL, makusanyo ya maduhuli kupitia utalii na mauzo ya visa kwa wageni na upatikanaji wa fursa za uchumi wa buluuโ€, alisema Waziri Kombo

Balozi Kombo aliendelea kueleza kuwa Wizara kupitia Balozi zake imetekeleza majukumu yake ya msingi kwa kuzingatia Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001, Toleo la Mwaka 2024 na kufanikiwa kupata mafanikio makubwa kwa manufaa ya nchi.

Mafanikio hayo ni pamoja na kupanua wigo wa uwakilishi, kuongezeka kwa fursa za biashara na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, kuimarika kwa uhusiano wa uwili, upatikanaji wa misaada na mikopo yenye masharti nafuu pamoja na kukua kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili duniani.

Kwa upande wao, wajumbe wa Kamati wameipongeza Wizara kwa kazi nzuri inayofanya katika kuimarisha diplomasia na kulinda maslahi ya Tanzania na kuitaka kuongeza juhudi ili diplomasia ya Tanzania iendelee kungโ€™ara duniani.

Address

Bagamoyo
61305

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Habari za Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share