Nyema books

Nyema books ili uweze kupata kitabu hiki wasiliana nasi kupia no zetu

22/01/2026
08/01/2026
04/01/2026

Asante Kaka Majidi na team nzima ya Lantern ebook

01/01/2026

Niwatakie heri ya Mwaka Mpya na ufurahie mwanzo wa simulizi ya Hazina ya Mshona viatu

31/12/2025

SAFARI YA DEBORA
MWANAMKE WA AJABU SOKONI
Debora alionekana akitembea katikati ya barabara iendayo jiji la kijani kibichi, kwa hatua za kujiamini kana kwamba ardhi aliyokanyaga ilikuwa imeshazoea ndoto zake. Mbele yake lilisimama gari kubwa aina ya wanteni ya kisasa, liking’aa chini ya jua la asubuhi kana kwamba nalo lilitaka kushuhudia hadithi yake.
Kila aliyemwona Debora alibaki na swali moja moyoni:
“Ni mwanamke wa aina gani huyu?”
Alikuwa ametoka kwenye soko kubwa la mazao ya shambani, soko lililojaa sauti za wauzaji, harufu ya matunda mabichi, na ndoto za watu wanaotafuta kesho bora. Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Gatu, baada ya kumwona Debora mara kadhaa sokoni hapo, aliona haiwezekani kuendelea kupita kimya kimya.
Alimsogelea kwa adabu akamsalimia.
“Samahani dada, naona mara kwa mara unakuja hapa. Naomba nifahamu, nini hasa kinakuleta sokoni kila siku?”
Debora alitabasamu—tabasamu lenye fumbo, tabasamu la mtu aliyepitia mengi lakini hakupoteza tumaini.
“Mimi ni mkulima na mfanyabiashara wa mazao ya shambani,” alimjibu kwa sauti tulivu.
Maneno yale yalimshangaza Gatu.
Mkulima? Na gari k**a hili?
Akakumbuka methali ya wahenga: “Usimdharau mtu kwa muonekano, hujui alipotoka wala aendako.”
Gatu alitamani kuuliza mengi zaidi, lakini Debora alimkatisha kwa upole.
“Kama unataka kunifahamu zaidi, njoo mashambani kwangu kijijini Mtokambali.”
Kabla hajapata jibu, Debora alikuwa tayari amepanda gari lake na kuondoka, akimuacha Gatu amesimama na mawazo mazito kuliko mzigo wa gunia la mahindi.

NDOTO YA GATU
Usiku ule haukuwa wa usingizi kwa Gatu. Mawazo yalimsongamana kichwani k**a soko la mnada. Alijiuliza kwa nini yeye, kijana aliyemaliza masomo, bado alikuwa akingoja ajira ya serikali k**a mvua ya masika, ilihali Debora—mdogo kwake—alikuwa ameshajenga ufalme wa mazao.
Gatu alikuwa miongoni mwa vijana waliokulia katika imani kwamba:
“Ukisoma, ajira itakuja yenyewe.”
Lakini maisha yalikuwa yakimfundisha somo tofauti.
Aliwakumbuka marafiki zake waliokwenda nje ya nchi kwa ufadhili. Kila alipoona picha zao mitandaoni, moyo wake ulijaa wivu na maswali. Lakini sasa, kukutana na Debora kulianza kubadilisha mwelekeo wa fikra zake.
“Asiyejaribu, hawezi kujua,” alijisemea kimoyomoyo.
Siku ya Nanenane ilipofika, Gatu alitembelea soko la wakulima. Alishangazwa na kuona bidhaa nyingi zikiwa na nembo ile ile aliyokuwa ameiona kwenye kadi ya Debora. Ndipo alipokutana na rafiki yake wa zamani, Fasta, aliyekuwa sasa mshirika wa Debora katika kilimo cha mahindi na tikiti maji.
Gatu alimuliza swali Fasta, umewezaje kuwa mshirika wa karibu wa Debora?
Fasta kajibu kwa kusema kuwa,
“Debora alininyanyua kutoka sifuri,” Fasta alisema kwa fahari.
“Alinionyesha kuwa kusubiri ajira ni sawa na kusubiri kivuli cha mti usiopandwa.”
Maneno yale yalipandikiza mbegu mpya moyoni mwa Gatu.
Alijua safari yake haikuwa tena ya ndoto, bali ya maamuzi pia alitamani sana kumjua Debora hata kwa uchache kupitia Fasta.
Fasta unaweza nieleza kidogo historia ya Debora k**a unamfahamu vyema?
Ndio namfahamu vyema bosi wangu,ngoja nikueleze kwa uchache historia ya bosi Debora naona unashahuku ya kujifunza kutoka kwake. Inaendelea.............

31/12/2025

Mwandishi anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumwezesha kuifikisha kazi hii mwisho. Shukrani za dhati zinaelekezwa kwa familia, marafiki, walimu na wale wote waliotoa moyo, mawazo na msaada katika safari ya uandishi.
Shukrani za pekee ziende kwa vijana wote wa Tanzania na Afrika kwa ujumla—ambao ndoto zao, mapambano yao na ujasiri wao vimekuwa chanzo kikuu cha msukumo wa riwaya hii. Aidha, jamii za vijijini, simulizi za jadi, methali, nahau na hekima za wazee zimeipa hadithi hii mwanzo na uhai wa kipekee.
Kwa kila msomaji anayeshika kitabu hiki, shukrani za dhati—kwa sababu kusoma ni hatua ya kwanza ya kubadilisha fikra, na fikra hubadilisha dunia.

31/12/2025

Riwaya ya Narudi Nyumbani ni sauti ya ndoto iliyosafiri mbali, ikapitia maumivu, matumaini, kuporomoka na kusimama tena. Ni simulizi ya vijana waliokataa kukata tamaa, waliothubutu kuota hata pale mazingira yalipowavunja moyo. Kupitia wahusika k**a Magonogangi, Debora, Amani na Gatu, hadithi hii inaonesha kuwa maendeleo ya kweli huanza pale mtu anaporudi kwenye asili yake, akaikumbatia jamii yake na kuamua kuibadilisha.
Hii ni hadithi ya safari—si safari ya mwili pekee, bali safari ya mawazo, dhamira na ujasiri. Ndoto za kijijini zinaweza kuwa ndoto za taifa, endapo zitapewa nafasi, uongozi wenye maono na ushirikiano wa dhati. Narudi Nyumbani si mwisho wa hadithi, bali ni mwanzo wa mjadala, tafakuri na hatua mpya kwa kizazi cha sasa na kijacho.

31/12/2025

KARIBU KATIKA RIWAYA MPYA YA NARUDI NYUMBANI AMBAYO LEO INAANZA KUTOKA RASMI. UKIITAJI KITABU HIKI WEWEZA NIPIGIA SIMU 0625 865 580 AU KUNITUMIA UJUMBE KWA WHASAP NA KULIPIA 5000/= UKAKIPATA MOJA KWA MOJA. KITABU HIKI KITAKUWA KINATOKA KWA MAANDISHI NA MASIMULIZI.

31/12/2025

huu ni mwanzo tu wa epsodi ya kwanza wa hadithi ya narudi nyumbani

Address

Mahenge
Morogoro

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nyema books posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Nyema books:

Share