Jeremia Damiano

Jeremia Damiano Informations de contact, plan et itinéraire, formulaire de contact, heures d'ouverture, services, évaluations, photos, vidéos et annonces de Jeremia Damiano, Agence marketing, Democratic Republic of the.

SARE YA SIMBA YA JANA INA THAMANI KULIKO INGESHINDA.Hatimae jana tambo za Dabi zilipata majibu kwa timu za Simba na Yang...
02/03/2026

SARE YA SIMBA YA JANA INA THAMANI KULIKO INGESHINDA.

Hatimae jana tambo za Dabi zilipata majibu kwa timu za Simba na Yanga kutoka suluhu ya bila kufungana(0-0). Kwa maana hiyo timu zote ziliambulia pointi moja moja.

Mchezo wa jana pamoja na matokeo kuwa suluhu umetupa picha nyingi za Dabi. Kwamba Dabi ni harakati na mbinu zaidi ya uwezo wa kucheza soka uwanjani. Kwamba kumbe k**a Simba asingepelekwa Gwantanamo na waamuzi wasingetoka Hamelini ni wazi tena bila kificho kwamba Simba angeibuka na ushindi mnono.

Nimefurahishwa sana jana nilipobaini kuwa mashabiki, wapenzi na wadau wa soka wanaojitambua na wasiokuwa na roho mbaya na bila kujali wao ni wa upande wa Simba au Yanga waliongea lugha moja tu kuwa katika mechi hiyo Simba alicheza mpira safi, alitawala mchezo, na walistahili ushindi.

Linapokuja swali kuwa ni kwanini basi pamoja na kutawala mchezo Simba hawakupata ushindi, hapo ndipo tunapoangukia kwenye majibu mengi tofauti. Moja ya majibu ambayo ndiyo yalikuwa maoni ya wengi lilikuwa ni jibu la Mwamuzi au waamuzi. Ni kweli kuwa kuna namna haikuwa sawa katika kulikataa goli la Suleiman Mwalimu wa Simba. Unapolikataa goli ambalo uwanja mzima unaliona ni goli halali unakuwa unaiathili kisaikolojia timu husika; kwamba wachezaji wake wanajiona kumbe wanafanya kazi bure hata wakifunga tena goli linaweza likataliwe.

Tabia hii ya waamuzi kuamua matokeo ya michezo ya ligi haikuanza jana wala juzi, tabia hii imekomaa. Tunaweza kudhani tuna mabingwa au washindi wa halali wa michezo; kumbe sivyo. Nilidhani adhabu kali zaidi ziendelee kutolewa kwa waamuzi wanaoharibu mpira. Ni kweli kuwa ukishakoseshwa ushindi na mwamuzi hata yeye akiadhibiwa wewe uliyepoteza hupati kitu, lakini ni vizuri adhabu ikawa kubwa kiasi kwamba wewe mwamuzi na aliyekukodi mkae muijutie. Wengine wakiona mwenzao amefungiwa miaka 5 na adhabu ya milioni 10 hawatathubutu kununuliwa na kupoteza kazi na taaluma yao. Bila kufanya hivyo, kila siku wanyonge watakuwa wanaonewa.

Tukiachilia mbali Dabi na makandokando yake, niwatahadhalishe Simba kuwa kuanzia sasa wamejipalia mkaa. Katika michezo yao ijayo wajiandae kuwa hawatakuwa wanacheza na timu moja. K**a walivyokuwa makini Zanzibar akina Magori waendelee hivyo hivyo na ufuatiliaji katika viwanja vyote. K**a yaliyofanyika kwa Dodoma jiji ndiyo yeleyele yamefanyika Zanzibar, basi hayohayo watataka yafanyike Mkwakwani, Majaliwa na kwingineko.

Juu ya tahadhali hiyo, kwa viongozi, wapenzi na mashabiki wa Simba, chonde chonde tuwalinde wachezaji wetu. Mlindeni Chama, mlindeni Luemba, mlindeni Geuye, mlindeni Mpanzu, mlindeni Kapombe, mlindeni Rushine, mlindeni Kibabage, mlindeni Mwalimu, mlindeni Aoura, mlindeni Kassali, mlindeni Toure na walindeni wengine wote. Wale jamaa wameshajua kuwa timu hii inakuja kuwa tishio na habari ya mjini. Zitatumika kila hila kuwapoteza wachezaji hawa katika anga la soka nchini. Watapondwa kwenye mitandao, watasakamwa na vyombo vya habari, wataalikwa kwenye viwanja vya starehe, watazushiwa mambo chungu nzima, watalogwa, watapelekewa mijimama, watashawishiwa kwa pesa waisaliti timu n.k. Bila umakini wa ulinzi hii timu haitadumu hadi mwisho wa msimu. Tutawaona na hawa hawafai na tutasajili wengine wapya.

Sare ya Simba imetusaidia sana kujitambua na kutupa hamasa ya kutenda zaidi. Imetuondolea mawazo ya kuamini kuwa timu imeshakamilika hivyo hatuhitaji nguvu na umakini zaidi. Tungeshinda jana tungetawaliwa na njozi za ubingwa na kujikuta kesho tutastukizwa na kufungwa kizembe na akina TRA, Mbeya city na wengineo. Ni vizuri jana imenyesha na tumepaona panapovuja. Sasa tuzibe na tusilibe kabisa.

Tusijidanganye kuwa kutoa sare Gwantanamo wenyewe wamefurahi; laxima nao wanakwenda kujipanga upya. Usikute mechi ijayo tukapelekwa gereza jingine moto zaidi la Black Dolphin, CECOT, au tukaletwa hapa hapa jirani Ukonga k**a danganya toto ili tujisahau tujilegeze watufunge. Mwendo uwe ni uleule wa man to man hadi kieleweke.

Pongezi nyingiii kwa wachezaji waliopambana, pongezi kwa kocha Barker kwa jitihada zake ndani ya kipindi kifupi, pongezi maalum kwa Mwenyekiti wa Bodi kwa usimamizi mzuri wa timu, pongezi kwa mashabiki na wapenzi wa Simba waliovuka maji kuhakikisha wachezaji hawawi wanyonge Zanzibar; na pongezi kwa wote waliobaki kwa maombi na michango yenu ya hali na mali. Hii ngoma bado kabisa. Haijaisha na haiishi mpaka iishe.

MUNGU IBARIKI SIMBA.

08/07/2025

Heshima utu na KAZI

Simba SC wamekataa ofa ya $350,000 kutoka MC Algers kwa ajili ya Kibu Denis, imethibitishwa. 🚨🇹🇿Mohammed Dewji amesema 𝐇...
05/02/2025

Simba SC wamekataa ofa ya $350,000 kutoka MC Algers kwa ajili ya Kibu Denis, imethibitishwa. 🚨🇹🇿

Mohammed Dewji amesema 𝐇𝐀𝐏𝐀𝐍𝐀 baada ya simu asubuhi ya leo.

Ameweka wazi: Simba wanapambana kwa ajili ya taji la ligi na pia wapo kwenye robo fainali ya Kombe la Shirikisho — haiwezekani kumwachia mchezaji wao nyota aondoke.

Dewji pia amesema kuwa ni kuchelewa sana kwani dirisha la usajili Tanzania limefungwa na hawawezi kupata mbadala wa Kibu.

Imeelezwa: Waalgeria wako tayari kuongeza dau hadi nusu milioni ya dola ili kumsajili Kibu, lakini kila kitu kinategemea uamuzi wa Mo Dewji.

Happy birthday Binti yangu  nakupenda sana ♥️♥️♥️
26/09/2024

Happy birthday Binti yangu nakupenda sana ♥️♥️♥️

26/09/2024

🙏🙏

04/03/2024

CAF:
SCHEDULE & RESULTS
TotalEnergies CAF Champions League Quarter-Final Teams confirmed
Published: Sunday, 03 March 2024

Title holders Ahly joined by seven strong contenders
Five former title holders in last eight
Exciting knock-out stage matches expected
Tunisia’s Esperance Sportive de Tunis laboured hard to secure a Quarter-Final berth in the TotalEnergies CAF Champions League Quarter-finals on Saturday night to complete the list of the top eight teams in Africa that will compete for the Trophy.

The Tunisians, playing at home, managed a 1-0 victory against Al Hilal SC in a highly competitive match.

Five former champions are among the sides that secured their places in the quarter-finals while two teams from Tanzania - Simba and Young Africans - will play in the last eight.

Of the eight teams that have officially booked their places, three are yet to taste continental success, with Al Ahly (11), TP Mazembe (5), Esperance (4), Asec Mimosas (1) and Mamelodi Sundowns (1), all having previously lifted Africa’s most coveted club football trophy.

Defending champions and Egyptian giants Al Ahly remain on course for their title defence after a 1-0 home victory over Young Africans on Friday to finish top of Group D with 12 points.

The Tanzanians clinched second place in the group despite losing the game in Cairo even though Belouizdad defeated Medeama 3-0 in the group's other match.

Sundowns secured Group A's top spot with 13 points after defeating TP Mazembe 1-0 in Pretoria on Saturday but the visiting side also advanced after finishing second with ten points.

Ivorian side ASEC Mimosas topped Group B with 11 points despite losing away to former champions Wydad Casablanca, who crashed out following Simba's heavy 6-0 win over Jwaneng Galaxy in the group's other game on Saturday.

Simba were equal on nine points with Wydad but advanced thanks to their better record.

Angola’s Petro de Luanda and Tunisia’s Esperance qualified for the quarter-finals from Group C following their victories on Saturday.

Petro de Luanda finished top of the group with 12 points after their 2-0 win over Etoile du Sahel while Esperance's 1-0 victory over Al Hilal helped them to secure second place with 11 points.

CAF will announce the date for the draw of the quarter-finals in the coming days.



Below is the list of quarter-final teams

Mamelodi Sundowns (South Africa)
TP Mazembe (DR Congo)
ASEC Mimosas (Cote d’Ivoire)
Simba (Tanzania)
Petro de Luanda (Angola)
Esperance (Tunisia)
Al Ahly (Egypt)
Young Africans (Tanzania)
TotalEnergies CAF Champions League Group Standings and Match Day 6 Results HERE

🙏🙏

27/02/2024

As Vita 0-1 Simba
Simba 1-0 Ahly
Merreikh 0-0 Simba
Simba 3-0 Merreikh
Simba 4-1 As Vita
Ahly 1-0 Simba

CRB 3-0 Yanga
Yanga 1-1 Ahly
Medeama 1-1 Yanga
Yanga 3-0 Medeama
Yanga 4-0 CRB
Ahly Vs Yanga

2020/21 Simba waliingia robo ya CAFCL baada ya mechi 4, Yanga wao baada ya mechi5

Mwana Simba hii si ya kukosa twenzetu Kwa mkapa jumamosi tuendelee kutoa darasa Kwa 🐸🐸
27/02/2024

Mwana Simba hii si ya kukosa twenzetu Kwa mkapa jumamosi tuendelee kutoa darasa Kwa 🐸🐸

27/02/2024
27/02/2024
From Simba sports club kesho Jumatatu saa 2:00 usiku kupitia Azam TV tutafanya mnada maalum wa kibegi pamoja na jezi zil...
30/07/2023

From Simba sports club
kesho Jumatatu saa 2:00 usiku kupitia Azam TV tutafanya mnada maalum wa kibegi pamoja na jezi zilizopelekwa kileleni mwa Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya uzinduzi wa jezi za msimu 2023/24.

Pesa ambazo zitapatikana kwenye mnada huo zitatumika katika ujenzi wa wodi za mama na mtoto kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Zanzibar. Watu wote mnakaribishwa kushiriki.

Orodha ya timu za Ligi ya Mabingwa 2023/24 iliyowasilishwa kwa CAF jana ambayo tuliiona. 🌍⚽️Misri: Al Ahly na Piramidi 🇪...
01/07/2023

Orodha ya timu za Ligi ya Mabingwa 2023/24 iliyowasilishwa kwa CAF jana ambayo tuliiona. 🌍⚽️

Misri: Al Ahly na Piramidi 🇪🇬
Moroko: FAR Rabat na Wydad 🇲🇦
Tunisia: Etoile Sahel na ES Tunis 🇹🇳
Algeria: CR Belouizdad na Constantine 🇩🇿
Afrika Kusini: Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates 🇿🇦
dR Congo: AS Vita Club na TP Mazembe 🇨🇩
Angola: Petro Luanda na de Agosto 🇦🇴
Nigeria: Enyimba na Remo Stars 🇳🇬
Guinea: Hafia na Horoya 🇬🇳
Tanzania: Yanga na Simba 🇹🇿
Zambia: Power Dynamos 🇿🇲
Ghana: Medeama SC 🇬🇭
Mauritania: FC Nouadhibou 🇲🇷
Rwanda: APR 🇷🇼
Ivory Coast: ASEC Mimosas 🇨🇮
Togo: AS Kara 🇹🇬
Uganda: Vipers SC 🇺🇬
Liberia: LISCR FC 🇱🇷
Burundi: Bumamuru FC 🇧🇮
Kamerun: Mchezo wa Coton 🇨🇲
Botswana: Jwaneng Galaxy 🇧🇼
Kenya: Gor Mahia 🇰🇪
Eswatini: Green Mamba 🇸🇿

Safari nyingine inaanza! 🏆✨

Adresse

Democratic Republic Of The

Site Web

Notifications

Soyez le premier à savoir et laissez-nous vous envoyer un courriel lorsque Jeremia Damiano publie des nouvelles et des promotions. Votre adresse e-mail ne sera pas utilisée à d'autres fins, et vous pouvez vous désabonner à tout moment.

Partager