09/03/2024
Ephesians 3:1-9
[1]For this cause I Paul, the prisoner of Jesus Christ for you Gentiles,
Kwa sababu hiyo mimi Paulo ni mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa;
[2]If ye have heard of the dispensation of the grace of God which is given me to you-ward:
ikiwa mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu;
[3]How that by revelation he made known unto me the mystery; (as I wrote afore in few words,
ya kwamba kwa kufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, k**a nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache.
[4]Whereby, when ye read, ye may understand my knowledge in the mystery of Christ)
Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.
[5]Which in other ages was not made known unto the sons of men, as it is now revealed unto his holy apostles and prophets by the Spirit;
Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; k**a walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho;
[6]That the Gentiles should be fellowheirs, and of the same body, and partakers of his promise in Christ by the gospel:
ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili;
[7]Whereof I was made a minister, according to the gift of the grace of God given unto me by the effectual working of his power.
Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
[8]Unto me, who am less than the least of all saints, is this grace given, that I should preach among the Gentiles the unsearchable riches of Christ;
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;
[9]And to make all men see what is the fellowship of the mystery, which from the beginning of the world hath been hid in God, who created all things by Jesus Christ:
na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote;