The Connect

The Connect Watawala. Maamuzi yaliyobadili dunia
📥 Gusa Follow kuanza safari ya kihistoria

Dunia haikuanza leo - Tunaunganisha nukta za jana
✍️ Makala nzito za matukio yaliyotikisa ulimwengu
🎬 Clip za matukio ya marais na viongozi waliopita
📜 Historia.

Kijana mtanashati wa Marekani mwenye umri wa miaka 21, Otto Warmbier, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Virginia, alikuwa kwe...
02/09/2026

Kijana mtanashati wa Marekani mwenye umri wa miaka 21, Otto Warmbier, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Virginia, alikuwa kwenye foleni ya kukaguliwa pasipoti ili kupanda ndege kurudi kwao. Safari yake ya siku tano ya utalii nchini Korea Kaskazini ilikuwa imemalizika, na alikuwa na furaha ya kurudi nyumbani kujiandaa na muhula mpya wa masomo.

Ghafla, mikono miwili yenye nguvu ilimshika bega kwa nyuma.

Maafisa wawili wa usalama wa Korea Kaskazini waliokuwa wamevaa sare za kijani kibichi na kofia kubwa walisimama pembeni yake kushoto na kulia. Bila kusema neno lolote, walimvuta pembeni. Marafiki zake waliokuwa naye kwenye foleni walishtuka huku Otto anawaangalia kwa hofu na kusema kwa sauti ya chini: "Nadhani nina shida kidogo... nitawapigia simu."

Haikuwa shida ndogo. Hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kwa dunia kumsikia Otto Warmbier akiongea akiwa na akili timamu.

Siku mbili kabla ya kuk**atwa kwake, usiku wa Mwaka Mpya, Otto na kundi lake la watalii walilala kwenye Hoteli ya Yanggakdo jengo refu la ghorofa 47 lililopo kwenye kisiwa katikati ya Mto Taedong jijini Pyongyang.

Hoteli hiyo ilikuwa na ghorofa ya tano ya siri, eneo ambalo halikuwa na batani kwenye lift (elevator) na lilijaa mabango ya propaganda ya serikali. Usiku huo, Otto alijipenyeza kwenye ghorofa hiyo yenye giza na kutoa bango moja la propaganda lililokuwa limeandikwa: "Tujihami vikali kwa imani ya Kim Jong-il!"

Serikali ya Korea Kaskazini iliona kitendo hicho si tu k**a wizi, bali k**a uhalifu mkubwa wa kumpinga Kiongozi Mkuu na Dola.

Wiki sita baadae, mbele ya kamera za vyombo vya habari vya kimataifa jijini Pyongyang, Otto alionyeshwa kwenye runinga. Alikuwa anatetemeka mwili mzima, anatokwa na machozi ya hofu, huku anasoma maelezo aliyolazimishwa na serikali:

"Nilifanya kosa kubwa zaidi maishani mwangu... Nataka kurudi nyumbani kwenye familia yangu! Tafadhali niokoeni!"

Mnamo Machi 16, 2016, Mahak**a Kuu ya Korea Kaskazini ilimuhukumu Otto Warmbier miaka 15 ya kazi ngumu gerezani (hard labor). Hukumu hiyo ilichukua dakika 5 tu kusomwa.

Baada ya hukumu hiyo, Otto alipotea kabisa. Hakuna mwanadiplomasia, daktari, wala Mmarekani yeyote aliyeruhusiwa kumuona au kuongea nae kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Ndani ya wiki chache tu baada ya hukumu hiyo, kitu fulani cha kutisha kilitokea akiwa mikononi mwa vyombo vya usalama vya Korea Kaskazini.

Ingawa serikali ya Korea Kaskazini ilidai kuwa Otto alipata ugonjwa wa (botulism) na kisha kupewa kidonge cha kulala kilichomfanya azimie, madaktari wa Marekani na uchungu*i wa kitabibu baadae ulipinga vikali maelezo hayo.

Ukweli ni kwamba, Otto alipatwa na kiharusi kikubwa cha ubongo (Anoxic Brain Damage) kilichosababishwa na ukosefu wa hewa ya oksijeni kwenye ubongo kwa muda mrefu. Hali hii hutokea pale mtu anaponyongwa, kukabwa koo, kuteswa kwa kutumbukizwa kichwa kwenye maji (waterboarding), au kupigwa vibaya sana kichwani na kusababisha mfumo wa moyo na upumuaji kusimama.

Mwili na umri wake mdogo haukuweza kuvumilia ukatili wa magereza ya Korea Kaskazini. Ubongo wake ulipoteza seli zote muhimu, na akakaa kwenye koma ya kudumu.

Mwezi Juni 2017, baada ya shinikizo kubwa la kidiplomasia kutoka kwa serikali ya Marekani chini ya Rais Donald Trump, Korea Kaskazini hatimae ilikubali kumwachia Otto kwa "sababu za kiutu."

Usiku wa tarehe 13 Juni 2017, ndege ya jeshi ya Marekani ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Cincinnati, Ohio. Wazazi wa Otto, Fred na Cindy Warmbier, walikuwa wanasubiri kwa hamu na matumaini kumkumbatia mtoto wao.
Milango ya ndege ilipofunguka, hali iliyojitokeza ilikuwa ya kusikitisha mno: Otto hakutoka anatembea. Alitolewa yuko kwenye kitanda cha wagonjwa akiwa amefungwa mipira ya kumsaidia kupumua. Macho yake yalikuwa wazi lakini hayakuwa yanaona wala kutambua chochote, ameuma meno na kutoa sauti za maumivu zisizoeleweka. Alipoteza uwezo wa kuona, kusikia, au kusogea, ubongo wake ulikuwa umekufa kabisa (vegetative state).

"Kijana wetu alirudishwa kwetu akiwa amepooza kabisa, asiyeweza kuongea wala kumtambua mtu yeyote. Korea Kaskazini haikumpiga tu kikatili, bali ilimwangamiza kabisa," alieleza baba yake, Fred Warmbier.

Siku sita tu baada ya kurejeshwa nyumbani Marekani, mnamo tarehe 19 Juni 2017, Otto Warmbier alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 22, akiwa amezungukwa na familia yake iliyokuwa inamlilia.

Kwa nini Otto Warmbier hakunusurika?
1. Mateso na Ukatili wa jeshi: Uchungu*i wa kitatibu ulionyesha kuwa ubongo wake ulipata uharibifu mkubwa kutokana na ukosefu wa hewa ya oksijeni, matokeo ya mateso makali ya kisaikolojia na kimwili mara tu baada ya hukumu yake.
2. Kunyimwa Matibabu: Mfumo wa Korea Kaskazini ulimficha kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kumpa matibabu sahihi ya mfumo wa fahamu, ukisubiri hadi hali yake iwe haina matumaini ndipo umwachie ili asifie gerezani.
3. Kutumiwa K**a Shinikizo la Kisiasa: Korea Kaskazini ilimtumia Otto k**a "kete ya kisiasa" (political pawn) ili kuilazimisha Marekani kufanya mazungumzo, lakini ukatili waliomfanyia ulivuka mipaka ya kibadamu.

Kifo cha Otto Warmbier kilitikisa dunia na kuisukuma Marekani kupiga marufuku raia wake wote kusafiri kwenda Korea Kaskazini k**a watalii, marufuku inayodumu hadi leo..
.................................
Download app hii ili usipitwe na simulizi hizi za kusisimua maana zinapatikana huko zaidi... App hii iko playstore.. Bonyeza link https://dub.sh/Wx9mJtc

01/09/2026

Saa kumi na moja za alfajiri. Ukungu mzito wa baridi kali ulikuwa umetanda juu ya milima ya Mkoa wa Pyongan Kusini, kilo...
31/08/2026

Saa kumi na moja za alfajiri. Ukungu mzito wa baridi kali ulikuwa umetanda juu ya milima ya Mkoa wa Pyongan Kusini, kilomita 80 kaskazini mwa Pyongyang. Nje ya u*io mrefu wa waya za umeme na minara ya walinzi wenye mitutu, dunia haikuwahi kujua k**a kuna hiyo sehemu.

Kwenye ramani za serikali, eneo hili lilikuwa limefutwa kabisa. Hata hivyo, ndani ya u*io huo, eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 200 lilijulikana kwa jina moja tu: Kambi 14 (Kaechon Internment Camp).

Tofauti na magereza mengine duniani, Kambi ya 14 si mahali pa kumrekebisha mhalifu. Ni eneo la "Total Control Zone" mahali ambapo wafungwa wanaingia wakiwa hai, na njia pekee ya kutoka ni kupitia moshi wa tanuru la kuchomea miili.

Mnamo tarehe 19 Novemba 1982, ndani ya kibanda cha matofali ya tope ndani ya Kambi ya 14, alizaliwa mtoto wa kiume aliyeitwa Shin Dong-hyuk.

Shin hakufanya kosa lolote. Wazazi wake walikuwa wafungwa walioruhusiwa kuoana na serikali k**a "zawadi" ya kufanya kazi kwa bidii. Chini ya sheria ya Korea Kaskazini ya "Hatia ya Vizazi Vitatu" (Three Generations of Punishment), ikiwa mtu mmoja atatenda kosa la kisiasa, familia yake yote hadi vizazi vitatu vya baadae lazima viangamizwe gerezani.

Kwa Shin, dunia haikuwa na magari, majengo marefu, intaneti, wala wazo la nchi inayoitwa "Korea Kaskazini."

Dunia yake yote ilikuwa ni u*io wa waya za umeme, matope, viboko vya walinzi, na njaa ya kudumu. Tangu akiwa na umri wa miaka sita, chakula chake kikuu kilikuwa ni supu ya kabichi iliyooza na mchele uliotengenezwa kwa ajili ya wanyama. Ili kuishi, watoto waliwinda panya, panzi, na konokono.

Mwaka 1996, Shin akiwa na umri wa miaka 13, tukio la kutisha lilitokea lililobadilisha maisha yake milele.

Usiku mmoja, akiwa amelala kwenye sakafu ya baridi, alisikia mama yake na kaka yake mkubwa wananong'onezana kwa sauti ya chini sana. Walikuwa wanapanga mpango wa kutoroka kambini.

Tangu akiwa mdogo, masomo pekee aliyofundishwa na walinzi shuleni ni kwamba: "Ukificha kosa la mfungwa mwingine, utauawa." Akiamini kuwa kuripoti mpango huo kungemletea zawadi ya chakula zaidi kutoka kwa walinzi, Shin alikimbia usiku huo na kumwambia mlinzi. Lakini walinzi hawakumpa zawadi.

Saa chache baadae, askari walivamia kibanda chao. Shin alichukuliwa na kutupwa kwenye chumba cha mateso cha chini ya ardhi (underground punishment cell). Kwa miezi saba, mtoto huyu wa miaka 13 alitundikwa kwenye dari huku miguu imefungwa, huku anapiliziwa moto mgongo ili atoe siri za familia yake.

Mwezi Novemba 1996, Shin alitolewa kutoka chumba cha mateso na kupelekwa katikati ya uwanja wa kambi. Maelfu ya wafungwa walilazimishwa kupiga magoti.

Mbele ya macho yake, Shin alishuhudia kaka yake anapigwa risasi ya kichwa na mama yake ananyongwa kwenye mti. Hakuna machozi yaliyotoa siku hiyo, mateso ya kambi yalishapoteza hisia zake zote k**a binadamu wengine, ikamfanya amchukie mama yake kwa kumzalia eneo hilo.

Miaka ilipita. Shin akawa kijana wa kazi ngumu kwenye kiwanda cha nguo na migodi ya makaa ndani ya kambi hiyo. Mwili wake ulikuwa umejaa majeraha: vidole vyake vilikatika kutokana na ajali za mashine, na mgongo wake ulikuwa na makovu makubwa ya moto.

Mnamo mwaka 2004, mfungwa mpya alihamishiwa gerezani hapo. Jina lake Park Yong-chul, mtu aliyeelimika aliyewahi kusafiri nje ya nchi kabla ya kuk**atwa.

Park alianza kumsimulia Shin mambo ambayo Shin hakuwahi kuyawazia maishani:

• Alimsimulia kuhusu miji iliyojaa taa usiku.

• Alimsimulia kuhusu kuku wa kukaanga, nyama ya ng'ombe, na chakula kinachopatikana bila kupigwa viboko.

• Alimwambia kuwa nje ya u*io ule, kuna dunia ambapo watu wanaishi kwa uhuru.

Maneno hayo yalizusha kitu kipya kabisa ndani ya moyo wa Shin: Tamanio la Uhuru.

Siku ya tarehe 2 Januari 2005, baridi kali ya msimu wa baridi ilifunika Kambi ya 14 kwa barafu nzito. Shin na Park walipangiwa kufanya kazi ya kukata kuni karibu na u*io wa mpaka wa kambi kwenye mteremko wa mlima.

Walinzi walipogeuka upande wa pili kwa sekunde chache tu, Park alimuangalia Shin na kunong'ona: "Kimbia!"

Park alikuwa wa kwanza kurukia u*io wa waya zenye umeme. Lakini hapo hapo, umeme mkali ulimpiga Park (electrocution) na akafa hapo hapo, mwili wake ukakauka juu ya waya hizo.

Shin hakusita. Katika kitendo cha kuto kukata tamaa na ujasiri wa ajabu, Shin alitumia mwili wa Park aliyekufa k**a "daraja" au kinga! Alipanda juu ya mwili wa mwenzake ili kuepuka kugusa waya za umeme moja kwa moja.

Wakati anaruka upande wa pili wa u*io, miguu yake ya chini iligusa waya za umeme, ukaichoma vibaya sana nyama na ngozi, lakini alifanikiwa kuangukia upande wa pili wa u*io nje ya Kambi 14!

Akiwa anavuja damu mguuni na kutetemeka kwa maumivu makali, Shin alikimbia usiku kucha kupitia milima na barafu, bila kujua anaenda wapi.

Kwa kutumia akili za mtaani, kuiba chakula vijijini, na kuhonga wafanyabiashara wa magendo nchini China kwa nguo na sigara, Shin Dong-hyuk alifanikiwa kuvuka Mto Tumen na kuingia China, na baadae kufika Korea Kusini.

Shin Dong-hyuk anabaki kuwa mwanadamu pekee katika historia anayejulikana, kuzaliwa ndani ya Kambi 14 ya Korea Kaskazini na kufanikiwa kutoroka akiwa hai.

Ushuhuda wake, uliowekwa kwenye kitabu maarufu duniani cha "Escape from Camp 14", uliifungua macho dunia kuhusu uwepo wa kambi hii ya siri ambapo maelfu ya wanadamu bado wanateseka hadi leo. Maisha yake ni ushahidi hai wa ukatili uliokithiri, lakini pia ni ishara ya nguvu ya kipekee ya roho ya mwanadamu kutafuta uhuru hata katikati ya mateso..

31/08/2026

Saa kumi na moja za alfajiri. Upepo wa baridi kali ya mwezi Septemba 1977 ulikuwa unavuma kwenye barabara za vumbi mjini...
29/08/2026

Saa kumi na moja za alfajiri. Upepo wa baridi kali ya mwezi Septemba 1977 ulikuwa unavuma kwenye barabara za vumbi mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini.

Kwenye jengo jeusi la ghorofa la Polisi wa Upelelezi (Security Branch) lililojulikana k**a Sanlam Building, chumba namba 619 kilikuwa kimejaa harufu ya damu, moshi wa sigara, na ukatili usiokuwa na kipimo.

Kwenye sakafu ya zege, alilala kijana mwenye umri wa miaka 30, mrefu na mwenye umbo la kishujaa, akiwa uchi wa mnyama, amefungwa pingu za chuma mikononi na miguuni. Jina lake aliitwa Bantu Stephen Biko muasisi na kiongozi mkuu wa Vuguvugu la Fikra za Mtu Mweusi (Black Consciousness Movement).

Hizi ndizo zilikuwa saa za giza nene kabla ya kifo chake kilichoitikisa serikali ya Makaburu na kubadilisha sura ya mapambano ya Afrika Kusini.

Story ilianzia usiku wa tarehe 18 Agosti 1977. Steve Biko na rafiki yake Peter Jones walikuwa wanarudi mjini King William's Town wakitokea Cape Town kwenye kikao cha siri cha kuunganisha vyama vya mapambano.

Serikali ya Makaburu (Apartheid) ilimmuwekea Biko amri ya kuzuiliwa nyumbani (banning order), ikimkataza kuongea na vyombo vya habari, kuandika vitabu, au kuondoka nje ya eneo lake bila kibali cha polisi.

Walipofika kwenye kizuizi cha barabarani (roadblock) nje kidogo ya mji wa Grahamstown, taa kali za magari ya polisi zililimulika gari lao. Makaburu walipoona sura yake, waligundua mara moja kuwa wamemk**ata "Samaki Mkubwa" waliyekuwa wanamtafuta kwa muda mrefu.

Biko na Jones walitiwa pingu hapo hapo na kupelekwa kwenye Kituo cha Polisi cha Walmer mjini Port Elizabeth.

Mnamo tarehe 6 Septemba 1977, Biko alihamishwa kutoka kituo cha polisi na kupelekwa ghorofa ya sita ya jengo la Sanlam Building. Hapo ndipo alipokutana na kikosi cha makatili kilichoongozwa na Major Harold Snyman na Captain Gideon Nieuwoudt.

Lengo la Makaburu lilikuwa moja tu: Kumtesa Biko kisaikolojia na kimwili ili akiri kuwa anapanga kuipindua serikali kwa silaha.

Lakini Biko hakuwa mfungwa wa kawaida. Wakati walinzi walipojaribu kumpiga na kumdhalilisha, Biko alipigana nao kiume! Alikataa kupiga magoti au kuonyesha hofu, Biko aliwajibu kwa sauti kali:

"K**a mnataka kunipiga, na mimi nitawapiga! Ninyi ni wanadamu k**a mimi, hamna haki ya kunidhalilisha!"

Siku hiyo, makatili hao walimvamia Biko kwa pamoja. Walimpiga kwa fimbo za chuma, wakamgongesha kichwa chake kwa nguvu kwenye ukuta wa zege, na kumpiga ngumi za uso hadi akapoteza fahamu. Pigo hilo la kichwani lilisababisha uvujaji mkubwa wa damu kwenye ubongo (severe brain damage).

Kwa siku sita zilizofuata, Biko aliwekwa kwenye sakafu ya baridi akiwa amezimia, akitokwa na povu mdomoni na damu masikioni. Madaktari wawili wa serikali walioenda kumuangalia walitumiwa na polisi kuficha ukweli, wakaripoti kuwa "Biko alikuwa anajifanya mgonjwa!"

Siku ya tarehe 11 Septemba, hali yake ilipozidi kuwa mbaya sana na mwili wake kuanza kupoteza uhai, polisi waliamua kumhamisha kutoka Port Elizabeth kwenda Hospitali ya Jela ya Pretoria.

Badala ya kutumia ndege au ambulance lenye vifaa vya matibabu, walifanya kitendo cha kinyama zaidi: Walimuweka Steve Biko nyuma ya gari la wazi la Land Rover, akiwa uchi kabisa, amefungwa pingu miguuni na mikononi, bila hata blanketi la kumfunika!

Gari hilo lilitembea kwa saa 12 usiku kucha katikati ya baridi kali ya msimu wa baridi, likisafiri umbali wa kilomita 1,200 kwenye rough road kuelekea Pretoria. Kila shimo ambalo gari liligonga, kichwa cha Biko kilikuwa kinajigonga pia.

Asubuhi na mapema ya tarehe 12 Septemba 1977, Land Rover hiyo iliwasili kwenye Jela Kuu ya Pretoria. Steve Biko aliburuzwa hadi kwenye sakafu ya chumba cha jela. Hakukuwa na daktari wala vifaa vya kumsaidia.

Saa chache baadae, akiwa peke yake kwenye sakafu hiyo ya baridi, Bantu Stephen Biko alikata roho. Alikuwa na umri wa miaka 30 tu.

Waziri wa Sheria wa serikali ya Makaburu, Jimmy Kruger, alitoa taarifa ya uongo kwa vyombo vya habari akidai Biko alifariki kutokana na "kugoma kula" (hunger strike). Na hata akaongeza kauli ya kejeli iliyoingia kwenye historia ya ukatili: "Kifo chake kinaniachia baridi tu" (His death leaves me cold).

Uchungu*i wa kujitegemea wa baadae (Autopsy) ulikuja kufichua ukweli: Biko alikuwa na majeraha makubwa matano kwenye ubongo wake, na mwili wake wote ulikuwa umejaa makovu ya vipigo.

Mazishi ya Steve Biko ya tarehe 25 Septemba 1977 yalihudhuriwa na zaidi ya watu 20,000, pamoja na wajumbe kutoka nchi 13 za Magharibi. Kifo cha kikatili cha Biko hakikuua vuguvugu lake. Badala yake, kilikuwa ni kiberiti kilichowasha moto wa mapindu*i. Umoja wa Mataifa (UN) uliuwekea utawala wa Makaburu vikwazo vikali vya silaha, na jina la Steve Biko likawa alama ya kimataifa ya ukombozi na utu wa mtu mweusi.

K**a alivyowahi kusema mwenyewe Steve Biko kabla ya kifo chake:
"Silaha yenye nguvu zaidi mikononi mwa mtawala dhalimu, ni akili ya mtawaliwa. Mkimkomboa fikra zake, mnamng'oa mtawala."...

Chanzo: Mtandao

Jua kali la mwezi Agosti 1974 lilikuwa likiangaza juu ya jiji la Kampala, Uganda. Magari ya jeshi ya Mamlaka ya Ulinzi w...
28/08/2026

Jua kali la mwezi Agosti 1974 lilikuwa likiangaza juu ya jiji la Kampala, Uganda. Magari ya jeshi ya Mamlaka ya Ulinzi wa Taifa (State Research Bureau – SRB) yalikuwa yanatembea kwa kasi barabarani, yakiacha vumbi na hofu kila yalipopita.

Kwenye wodi ya hospitali moja jijini hapo, mwanamke mrembo sana mwenye umri wa miaka 26, aliyekuwa na ngozi laini na macho makubwa ya kipekee, amekaa kitandani anatetemeka. Jina lake aliitwa Kay Adroa Amin mke wa pili wa Rais katili wa Uganda, Field Marshal Idi Amin Dada.

Kay hakujua kuwa saa chache zilizokuwa zinafuata zingekuwa na mwisho wa kutisha na wa kikatili zaidi katika historia ya Uganda.

Story ilianzia miaka ya 1960. Khezia Adroa (anajulikana zaidi k**a Kay Adroa), binti wa mchungaji wa Kanisa la Anglikana kutoka kabila la Lugbara (kaskazini magharibi mwa Uganda), alikuwa msichana mrembo na msomi aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu cha Makerere.

Mnamo mwaka 1966, Idi Amin wakati huo akiwa Mkuu wa Majeshi ya Uganda alivutiwa sana na urembo na elimu ya Kay. Alimuoa na kumfanya kuwa mke wake wa pili, kulingana na mila na sheria za Kiislamu zilizomruhusu kuwa na wake wengi.

Kwa miaka kadhaa, Kay alikuwa "Sura ya Upole" ya utawala wa Idi Amin. Alimzalia watoto wanne na kuwa naye bega kwa bega wakati Amin alipofanya mapindu*i ya kijeshi mwaka 1971 na kumng'oa Rais Milton Obote.

Lakini Amin alipozidi kupata madaraka, ukatili na mashaka yake (paranoia) viliongezeka. Kila mtu kwake alikuwa msaliti. Mapema mwaka 1974, Amin alimshutumu Kay kuwa anajihusisha na watu wa familia yake waliokuwa wanampinga Rais, na kwa hasira kubwa, alimtaliki rasmi mwezi Machi 1974, akamfukuza Ikulu na kumwamuru aishi chini ya ulinzi mkali wa majasusi wa SRB.

Baada ya kupewa talaka, Kay alibaki mpweke na aliyekatishwa tamaa, akaishi kwenye nyumba moja iliyotengwa jijini Kampala. Akiwa katika hali hiyo ya msongo wa mawazo na kutengwa, Kay alianza uhusiano wa siri na daktari mmoja handsome na msomi wa masuala ya wanawake (Gynecologist) aliyefanya kazi katika Hospitali ya Mulago, Dr. Peter Mbalu Mukasa. Miezi michache baadae, Kay aligundua kuwa ana mimba!

Katika nchi inayotawaliwa na Idi Amin, kuwa na mimba ya mwanaume mwingine ukiwa mke wa zamani wa Rais ilikuwa ni hukumu ya kifo ya moja kwa moja sio tu kwa Kay, bali pia kwa Dr. Mukasa na familia zao zote. Amin alikuwa mtu mwenye wivu mkubwa sana na hakukubali kuaibishwa.

Siku ya tarehe 13 Agosti 1974, Kay na Dr. Mukasa waliamua kufanya upasuaji wa siri wa kutoa mimba hiyo (abortion) kwenye kliniki binafsi ya daktari huyo ili kufuta ushahidi kabla Amin hajagundua. Lakini oparesheni hiyo ya siri ilienda mrama.

Katikati ya upasuaji huo, Kay alianza kuvuja damu nyingi sana kwa ndani (internal hemorrhage). Dr. Mukasa alijaribu kwa kila namna kuokoa maisha yake, lakini juhudi zake ziligonga mwamba. Kay Adroa Amin alipoteza maisha akiwa kwenye kitanda cha upasuaji.

Akiwa amepatwa na kiwewe na hofu ya kile kitakachomtokea mikononi mwa majasusi wa Idi Amin, Dr. Mukasa alikimbia nyumbani kwake. Saa chache baadae, daktari huyo alikunywa sumu na kujiua, akiiacha familia yake na watoto wake wakiwa kwenye mshtuko. Mwili wa Kay ulibaki peke yake ndani ya kliniki hiyo.

Walinzi na majasusi wa SRB walipogundua kuwa Kay amefariki, walitoa taarifa haraka sana kwa Idi Amin. Amin, aliyekuwa anatawaliwa na ghadhabu za wivu, hasira ya kuaibishwa, na imani za kishirikina, aliamuru mwili wa Kay upelekwe mochwari ya Hospitali ya Mulago chini ya ulinzi wa wanajeshi wake maalum. Hapo ndipo kitendo cha kinyama zaidi kilipofanyika.

Siku iliyofuata, tarehe 14 Agosti 1974, Idi Amin aliamuru madaktari wa jeshi na makomandoo wake waufanyie mwili wa Kay unyama uliomshtua kila aliyekuwepo.

Ili "kutoa fundisho" kwa wake zake wengine waliobaki na raia wa Uganda, Amin aliamuru mwili wa Kay ukatwe vipande vipande! Mikono na miguu yake vilitenganishwa na kiwiliwili.

Kisha, Amin aliamuru madaktari waushone tena mwili huo kwa u*i mweusi, lakini wakibadilisha nafasi zao: mikono yake ilishonwa sehemu ya miguu, na miguu yake ikashonwa sehemu ya mikono!

Baadae, Amin aliamuru watoto wake wote aliozaa na Kay, pamoja na wake zake wengine (akiwemo Mama Atyat na Sarah Kyolaba), wapelekwe mochwari.

Picha ya kutisha ilitokea pale milango ya mochwari ilipofunguka: Amin alisimama juu ya meza ya chuma huku akionyesha mwili wa Kay uliokatwa na kushonwa vibaya, damu ikiwa bado mbichi, na kuwaambia watoto na wake zake kwa sauti ya ukali:

"Tazameni nini kitatokea pale mke anapomsaliti Rais wake! Hii ndiyo hatima ya mwanamke yeyote atakayethubutu kunitenga au kuwa na mwanaume mwingine!"

Watoto walipiga kelele kwa hofu na kulia vibaya sana. Tukio hilo lilikuwa zito kisaikolojia na liliwaacha na makovu ya maisha yasiyofutika.

Baada ya onyesho hilo la kutisha, mwili wa Kay uliwekwa kwenye jeneza na kusafirishwa chini ya ulinzi mkali wa vifaru vya jeshi kuelekea kijijini kwao West Nile kwa ajili ya ku*ikwa kwa siri usiku wa manane. Raia walipigwa marufuku kulia au kuonyesha msiba...

____________________________
Unaweza ku download app hii playstore ili usipitwe na Simulizi nyingi kuhusu matukio yaliyotikisa dunia.. Link hii hapa https://dub.sh/Wx9mJtc

Kwenye jumba la kifalme la udongo na chuma lililozungukwa na miili ya simba na mamba waliokaushwa, aliishi mwanamume mmo...
27/08/2026

Kwenye jumba la kifalme la udongo na chuma lililozungukwa na miili ya simba na mamba waliokaushwa, aliishi mwanamume mmoja aliyetawaliwa na woga na wivu mkubwa wa madaraka. Alikuwa amevaa vazi la dhahabu lililonakshiwa na taji ya almasi yenye thamani ya mamilioni ya dola. Jina lake aliitwa Jean-Bédel Bokassa aliyejikweza kuwa "Mtawala Mkuu (Emperor) Bokassa I".

Bokassa aliamini kuwa alikuwa Mungu mdogo duniani. Lakini hakujua kuwa kwenye jiji la Paris, Ufaransa, na kwenye vituo vya kijeshi vya siri vya makomandoo wa Kifaransa, saa yake ya kuanguka ilikuwa imeshaanza kuhesabiwa.

Cheche iliyoleta mwisho wake ilianza mwezi Januari 1979. Bokassa, akiwa amefilisika kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma, alipitisha sheria ya kinyama: Watoto wote wa shule nchini humo walilazimishwa kununua na kuvaa sare za shule zilizotengenezwa na kiwanda kinachomilikiwa na mke wake tu! Sare hizo zilikuwa na bei ghali sana kiasi kwamba wazazi wengi walishindwa ku*imudu.

Mwezi Aprili 1979, maelfu ya wanafunzi wadogo na vijana waliingia mitaani jijini Bangui kupinga sheria hiyo. Bokassa alikasirika kupita kiasi. Aliamuru jeshi lake kuwak**ata zaidi ya watoto 100 waliokuwa na umri kati ya miaka 8 hadi 16 na kuwafunga Jela ya Ngaragba.

Usiku wa tarehe 19 Aprili 1979, Bokassa mwenyewe aliitembelea jela hiyo akiwa amelewa na kushika bakora nene ya chuma yenye ncha ya pembe ya ndovu.

Mbele ya walinzi wake, Bokassa alishiriki kikamilifu kuwapiga watoto wale viboko vya kichwa na kuwakanyaga-kanyaga kwa viatu vya jeshi hadi wengi wao wakavuja damu na kupoteza maisha. Watoto zaidi ya 80 walichinjwa na kuuawa usiku huo mmoja.

Ukatili huu wa kutisha ulipovuja kupitia mashirika ya Haki za Binadamu, Rais wa Ufaransa wa wakati huo, Valéry Giscard d'Estaing ambaye awali alikuwa rafiki mkubwa wa Bokassa aligundua kuwa Bokassa amekuwa mzigo mkubwa kisiasa na doa kwa Ufaransa.

Ufaransa iliamua kumng'oa kwa nguvu. Plan ilipangwa kwa siri kubwa chini ya jina la "Operation Caban" na "Operation Barracuda".

Mnamo tarehe 19 Septemba 1979, Bokassa alitoka nchini kwake na kusafiri kwenda Libya kukutana na Muammar Gaddafi ili kuomba msaada wa fedha. Ufaransa ilitumia fursa hiyo ya Bokassa kutokuwepo nchini.

Saa 6:00 usiku wa tarehe 20 Septemba 1979, ndege ya jeshi la Ufaransa aina ya Transall C-160 ilitua kwa siri kubwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Bangui.

Ndani ya ndege hiyo kulikuwa na makomandoo 83 wa kikosi maalum cha jeshi la Ufaransa (1er RPIMa), wakiongozwa na majasusi wa siri wa DGSE. Pamoja nao alikuwepo David Dacko, rais wa zamani aliyepinduliwa na Bokassa miaka 13 nyuma.

Bila risasi hata moja kufyatuliwa, makomandoo wa Ufaransa waliutwaa uwanja wa ndege, vituo vya redio, na Ikulu ya Bangui. Saa 6:30 usiku, David Dacko alitangaza kwenye redio ya taifa kuwa utawala wa Bokassa umeanguka na ufalme wake umevunjwa.

Wakati wanajeshi walipovamia Majumba ya Kifalme ya Bokassa huko Villa Kolongo na Berengo, walikutana na ushahidi uliowashtua makomandoo hao waliokomaa kivita:
• Ndani ya majokofu makubwa ya Ikulu (freezers), walikuta viungo na nyama za wanadamu zikiwa zimehifadhiwa k**a nyama ya ng'ombe!

• Mashahidi na wapishi wa Ikulu walikiri kuwa Bokassa alikuwa na tabia ya kula nyama ya wanadamu (cannibalism) na kuwalisha wageni wake wa kimataifa bila wao kujua.

• Miili ya wapinzani wake kisiasa ilikutwa ikiwa imetupwa kwenye mabwawa ya mamba aliokuwa akiwafuga kwake.

Bokassa alipogundua akiwa nchini Libya kuwa amepinduliwa na hana tena nchi, alijaribu kutorokea Ufaransa lakini alikataliwa. Alilazimishwa kuishi ukimbizini nchini Ivory Coast na baadae Ufaransa kwa miaka kadhaa kabla ya kufanya kosa kubwa la kurudi nchini kwake mwaka 1986, akiamini wananchi bado wanampenda.

Mara tu alipotua Bangui, alik**atwa hapo hapo na kufikishwa mahak**ani kwa makosa ya Mauaji ya Kimbari, Utesaji, Utekaji Nyara, na Kula Nyama za Wanadamu.

Mahak**a ilimuhukumu adhabu ya kifo, lakini baadae adhabu hiyo ilipunguzwa na kuwa kifungo cha maisha jela kabla ya kuachiwa huru mnamo mwaka 1993 kutokana na msamaha wa rais.

Tarehe 3 Novemba 1996, Jean-Bédel Bokassa alifariki dunia kwa shambulio la moyo jijini Bangui akiwa maskini wa kutupwa, aliyetengwa na dunia na kukumbukwa tu k**a mmoja wa viongozi makatili zaidi waliowahi kuitawala Afrika...
_______________________________________________________
Simulizi zaidi za Enzi zinapatikana kwenye App ya ndugu Syaga James ambaye ameomba kuwa partner wetu.. Hivyo unaweza ku download app hii playstore ili usipitwe na Simulizi nyingi kuhusu matukio yaliyotikisa dunia.. Link hii hapa https://dub.sh/Wx9mJtc

Saa sita za usiku. Baridi ya mwezi Novemba mwaka 1985 ilikuwa inatawala kwenye mitaa ya jiji la Accra, Ghana.Kwenye nyum...
26/08/2026

Saa sita za usiku. Baridi ya mwezi Novemba mwaka 1985 ilikuwa inatawala kwenye mitaa ya jiji la Accra, Ghana.

Kwenye nyumba moja ya siri iliyopo Airport Residential Area, mwanamke mmoja mrembo raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 35 aliyeitwa Sharon Scranage alikuwa amekaa kitandani anatetemeka. Sharon alikuwa mtaalamu wa mawasiliano wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) aliyekuwa ametumwa kufanya kazi kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Ghana.

Mbele yake alisimama mwanamume mrefu, mtanashati, aliyeitwa Michael Soussoudis, binamu wa damu wa Kiongozi wa Mapindu*i na Rais wa Ghana, Jerry John Rawlings.

Sharon hakujua kuwa uhusiano wao wa kimapenzi wa miezi kadhaa ulisuka mtego mbaya zaidi wa kijasusi uliokuwa unaenda kulipua bomu kati ya Washington na Accra, na kuweka wazi siri zote za CIA barani Afrika.

Story ilianzia mwaka 1983. Baada ya Kapteni Jerry Rawlings kuchukua madaraka nchini Ghana kupitia mapindu*i ya kijeshi mwaka 1981, serikali ya Marekani na CIA zilikua na wasiwasi mkubwa kuwa Rawlings alikuwa anaelekea kwenye mfumo wa Kikomunisti na kushirikiana na Cuba na Libya.

CIA ilituma kikosi chake cha siri cha majasusi jijini Accra ili kufanya operesheni za kuipindua au kuidhibiti serikali ya Rawlings.

Ili kufanikisha hili, CIA ilimfanya Sharon Scranage ku*ifikia faili zote za siri za shirika hilo nchini Ghana. Lakini idara ya usalama wa taifa ya Ghana (Bureau of National Investigations – BNI), chini ya uratibu wa Michael Soussoudis, iligundua uwepo wa Sharon.

Soussoudis alitumia mbinu ya kijasusi inayojulikana k**a "Honeytrap" (mtego wa mahaba). Alimkaribia Sharon, akamfanya ampende kwa dhati, na kisha kuanza kumuomba siri ndogo ndogo za ubalozi k**a ishara ya "upendo."

Sharon, akiwa amezama kwenye mahaba na bila kujua anachezewa mchezo wa kijasusi, alianza kumvujishia Soussoudis taarifa za siri za CIA!

Taarifa alizovujisha Sharon zilikuwa dhahabu safi kwa serikali ya Ghana:

1. Orodha ya Majasusi: Alitoa majina na anwani za raia wote wa Ghana waliokuwa wanafanya kazi kwa siri k**a majasusi na watoa taarifa wa CIA ndani ya Jeshi na Serikali ya Ghana.

2. Mipango ya Mapindu*i: Alivujisha maelezo ya operesheni za siri zilizokuwa zinapangwa na CIA ili kumpindua Jerry Rawlings.

3. Mifumo ya Mawasiliano: Alitoa Code na njia za siri za mawasiliano zilizotumiwa na Ubalozi wa Marekani na Washington.

Mara tu BNI ilipopata orodha hiyo, serikali ya Rawlings ilifanya msako wa kimya kimya usiku wa manane. Majasusi wote wa Ghana waliokuwa wanafanya kazi na CIA walik**atwa mmoja baada ya mwingine na kutupwa kwenye magereza ya siri, huku wengine wakikutana na hukumu ya kifo kwa kosa la usaliti wa taifa.

Mnamo Mei 1985, Sharon Scranage alipomaliza muda wake wa kazi nchini Ghana, alirudi Makao Makuu ya CIA mjini Langley, Virginia.

Lakini makao makuu ya CIA walikuwa tayari wameanza kushtukia kuwa mtandao wao wote nchini Ghana umeanguka ghafla. Idara ya Usalama ya Ndani ya CIA na FBI walimfanyia Sharon vipimo vya mashine ya kubaini uongo (polygraph test).

Sharon alishindwa mtihani huo vibaya sana. Akiwa anatokwa na machozi ya hofu, alikiri kila kitu: "Nilifanya kwa sababu nilimpenda Michael..."

FBI walimtumia Sharon kumwekea mtego Soussoudis. Sharon alimpigia simu Soussoudis na kumshawishi asafiri kwenda Marekani kukutana nae kwenye hoteli moja huko Virginia. Mnamo tarehe 17 Julai 1985, Soussoudis alipotua nchini Marekani na kuingia hotelini, mak**andoo wa FBI walivunja mlango na kumk**ata hapo hapo.. Mjumbe wa familia ya Rais wa Ghana akak**atwa Marekani kwa makosa ya ujasusi!

Kuk**atwa kwa Soussoudis kuliziweka serikali za Marekani na Ghana kwenye mgogoro mkubwa wa kidiplomasia. Rawlings alitishia kuwanyonga majasusi wote wa Kighana waliokuwa wanawafanyia kazi CIA ikiwa Soussoudis asingerudishwa nyumbani.

Katika kitendo kisicho cha kawaida katika historia ya Vita Baridi barani Afrika, serikali ya Marekani na Ghana ziliingia kwenye makubaliano ya siri ya Mabadilishano ya Wafungwa (Spy Swap):

• Mnamo Novemba 1985, Marekani ilimwachia Michael Soussoudis kutoka jela na kumrejesha Accra.

• Kwa upande wa Ghana, Rawlings aliwaachia huru majasusi 8 wa Kighana waliokuwa wakiifanyia kazi CIA, akawapokonya uraia wao wa Ghana, na kuwasafirisha kwenye ndege kuelekea Marekani.

Sharon Scranage alihukumiwa miaka mitano jela nchini Marekani kwa kosa la kutoa siri za usalama wa taifa (ingawa adhabu yake ilipunguzwa baadaye).

Kashfa hii, iliyojulikana k**a "The Scranage-Soussoudis Affair", inabaki kuwa moja ya matukio makubwa na ya kustaajabisha zaidi ya kijasusi katika historia ya Afrika. Ilionyesha jinsi hisia za badamu na mbinu za mapenzi zinavyoweza kuangusha mtandao mzima wa shirika lenye nguvu zaidi la ujasusi duniani, na kuilazimisha Marekani kufanya biashara ya kubadilishana majasusi katikati ya Afrika...

_______________________________________________________
Simulizi zaidi za Enzi zinapatikana kwenye App ya ndugu Syaga James ambaye ameomba kuwa partner wetu.. Hivyo unaweza ku download app hii playstore ili usipitwe na Simulizi nyingi kuhusu matukio yaliyotikisa dunia.. Link hii hapa https://dub.sh/Wx9mJtc

Address

Koinange
Nairobi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Connect posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share