27/04/2026
Kuna taarifa kwamba vijana wawili wamepatikana wakiiba katika area ya Muthaara. Inasemekana wako Grade 10. Mmoja wao alipigwa na wananchi, huku mwenzake akitoroka.
Wameeleza mahali simu ya mama fulani iliyokuwa imeibwa dukani ilipelekwa, na simu hiyo imepatikana. Kwa sasa, wanakijiji wengi wanaendelea kujitokeza wakidai vitu vyao ambavyo vilikuwa vinapotea.
Ni muhimu sana k**a wazazi tushirikiane kuwalea na kuwafunza watoto wetu maadili mema. Wizi ni mbaya na una madhara makubwa kwa jamii.
Mama wa mmoja wa vijana yupo hapo na anaomba msamaha. Inasemekana pia huenda kuna vijana wengine wanaohusika, kwani kijana anaulizwa kuonyesha wanakoishi.
Tuchukue hatua mapema k**a jamii ili kuzuia mambo k**a haya kuendelea.