28/05/2020
SIRI: Jinsi Ya Kuhakikisha Una Afya Nzuri Ya Mwili Na Akili Maisha ni Mwako
Je, unajua uhusiano uliopo baina ya Akili yako na Mwili wako?
Uhusiano uliopo baina ya akili na mwili ni wa karibu mno. Moja inapoumizwa, nyingine husononeka.
Hali ya akili huathiri afya kwa kiasi kikubwa kuliko tunavyoelewa. Magonjwa mengi yawakabiliyo wanadamu leo ni matokeo ya fadhaa kiakili.
Huzuni, wasiwasi, kutoridhika, hasira, hatia,
kutokuamini, yote hudhoofisha nguvu za uhai,
na kuleta uchakavu na kifo.
Ugonjwa unaletwa, na kuendelezwa zaidi, kupitia mawazo yetu. Wengi ni dhaifu maishani mwao mwote ambao wangalikuwa wazima endapo wangaliwaza hivyo.
Ujasiri, tumaini, imani, huruma, upendo
husaidia kuleta afya na maisha marefu. Akili
tulivu iliyoridhika, roho yenye uchangamfu, ni
afya kwa mwili na NGUVU kwa roho.
Shukurani, uchangamfu, ukarimu, kutumainia
upendo na ulinzi wa Mungu---hizi ni KINGA
bora za afya.
Nguvu ya nia na umuhimu wa kujitawala nafsi, yote katika uhifadhi na urejeshaji wa afya, fadhaa na uangamivu utokanao na hasira, kulalamika, uchoyo au unajisi, na kwa upande mwingine, nguvu tele ya ajabu itokanayo na tabasamu, ukarimu, shukurani, vyapaswa kuoneshwa.
Thoughts from the Mount of blessings