02/07/2023
Nafasi ya Kazi
Webmagic Tanzania inatafuta mfanyakazi wenye shauku ya kujaza nafasi ya Msimamizi wa Ofisi ambaye atafanya kazi za ofisini, mawasiliano na shughuli zinazohusiana na masoko.
Majukumu
1) Kufanya kazi tovuti za ofisi na mteja kila siku,
2) Kutengeneza na kuboresha akaunti za media za kijamii za ofisi na mteja,
3) Kutangaza bidhaa na tovuti za ofisi na za wateja kwenye mitandao ya kijamii + na sehemu nyinginezo
4) Kufanya mawasiliano ya kawaida kupitia barua pepe, WhatsApp, mitandao ya kijamii, SMS, simu kwa ajili ya kuwafanya wateja waendelee kuwa nasi
5) Kufanya kazi nyingine za ofisi k**a atakavyoamriwa na msimamizi wake
6) kuwasilisha ripoti ya kila mwezi kwa msimamizi
Sifa inahitajika
• Kidato cha nne menye ujuzi na uzoefu katika tovuti na majukwaa makubwa ya mitandao ya kijamii
Sifa Zingine Zinazohitajika
1) Awe na tabia ya kujitoa kufanya kazi kwa ubora
2) Awe ni mtu anayewajibika na anayeaminika
3) Awe ni mtu anayependa sana kutengeneza websites na mitandao ya kijamii.
4) Mchapakazi anayeweza kufanya kazi nyingi, kwa ubora na kwa muda uliowekwa
5) Mtu anayejali undani wa kazi na ubora kwa kazi zake zote
6) Awe mtu mwenye hamu na wa haraka kujifunza na kutumia teknolojia mpya kwenye kazi zake
7) Mtu mwenye fikra chanya katika maisha, juu ya wanadamu wengine na maisha kwa ujumla
Mahali pa kazi: Arusha mjini
Awe ni mkazi wa jiji la Arusha
Tuma ombi kabla ya tarehe 1 Agosti 2023:
Watakao tuma mapema watafikiriwa kwanza
Tembelea ana kwa ana au Piga/SMS/WhatsApp: 0755646470 au andika kwa [email protected]
Unaweza kutembelea tovuti yetu kwa https://www.webmagic.co.tz
Waombaji walio na sifa za msingi tu ndio watakaofikiriwa