17/01/2024
SOMO: *HAKIKA UTASEMA KUNA KUINUKA TENA, KWASABABU YUPO MUNGU AKUINUAYE.*
🙏Roho wa Mungu tunakushukuru kwa kuendelea kuongea na sisi,ni Neema ya ajabu kujua yakwamba upo pamoja nasi mpaka ukamilifu wote,tunaomba utusaidie kulielewa Neno lako na hili Neno likatuvushe Imani hata Imani,utukufu hadi utukufu katika Jina kuu la Yesu Kristo. amen
Ayubu 22:29,30
Imeandikwa
*HAPO WATAKAPO KUANGUSHA, UTASEMA,KUNA KUINUKA TENA;*
*NAYE MNYENYEKEVU MUNGU ATAMUOKOA...NAAM UTAKOLEWA KWASABABU YA USAFI WA MIKONO YAKO*
=maadamu upo Duniani na unaishi lazima ujue wapo wanaosubiri uanguke na watafurahia kuanguka kwako;hata ukiishi k**a mtakatifu au kwa kujitenga kiasi gani watu hawa hawatakosekana kwenye maisha, hata ukiwa mbali nao watakuwazia mawazo ya kukuangusha,watanena maneno ya kukuangusha,na watakaa vikao vya kukuangusha wakisema tuone k**a atafika mbali...nk. kwahiyo uwatarajie wapo.
njema ni kwamba ikiwa tumaini lako nikwa MUNGU ALIYE HAI basi ujue HUTAANGUKA NA HATA UKIANGUKA HUWEZI KUBAKI CHINI,HAKIKA KUNA KUINUKA TENA..Neno la Mungu linatuambua *👆NAYE MNYENYEKEVU MUNGU ATAMUOKOA*
👂👂Lazima tujue kanuni mojawapo ndani ya Ufalme wa Mungu ni haijalishi unapita wapi,iwe ni kwenye shida au iwe ni kwenye raha endelea kunyenyekea chini ya mkono wa Mungu na usitoke kwenye mstari wa kumtii Mungu, na usitoke kwenye mstari wa kutafuta kumpendeza Mungu..
*👆UTAOKOLEWA KWA USAFI WA MIKONO YAKO*
1Petro5:6-7
Imeandikwa
*BASI NYENYEKEENI CHINI YA MKONO WA MUNGU ULIO HODARI, ILI AWAKWEZE KWA WAKATI WAKE.*
*7 HUKU MKITWIKA YEYE FADHAA ZENU ZOTE,KWA MAANA YEYE HUJISHUGHULISHA SANA KWA MAMBO YENU*
👆yupo Mungu awezaye kukuinua,yupo Mungu anayejishughurisha sana na fadhaa zako *zote unazompelekea* tena anashughurika nazo bila kukuchoka,binadamu wanaweza kukuchoka kwa mizigo yako unayowapelekea lakini Mungu peke yake ndio hawezi kukuchoka *👆anajishughurisha sana na mambo yako yote.*
Mithali 24:15,16
Imeandikwa
*EWE MTU MBAYA,USIYAVIZIE MAKAO YAKE MWENYE HAKI; WALA USIPAHARIBU MAHALI PAKE PA KUPUMZIKA 👂KWA MAANA MWENYE HAKI HUANGUKA MARA SABA AKAONDOKA TENA*
=Mungu anatoa ujumbe kwa wabaya wako hawatakiwi kufurahia saana maanguko yako kwasbabu MWENYE HAKI WA MUNGU HATA A