13/08/2026
Moja kati ya kumbukumbu zangu nzuri za utotoni, ilikuwa ni kwenda mtoni kila siku jioni mara baada ya kumaliza kuchunga ng'ombe wangu.
Kule kijijini tulikuwa tunaita Kunywesha.
Hapo nilikuwa naenjoy sana utulivu na amani, nikifurahia namna maji yanavyotembea, huku nikiangalia ndege wanavyoruka na kukusanyika kwenye miti.
Wakati huo huo, nilikuwa nikitazama namna miti ya mianzi iliyozunguka pembezoni mwa mto, inavyoinama pale upepo unapokuwa mkali, na kurudi katika hali yake, pale hali inapokuwa shwari.
Nilipata kitu kikubwa sana cha kujifunza.
Ninapokumbuka uwezo huo wa mianzi ile kurudi katika utulivu wake kila baada ya upepo kupita, neno uvumilivu linanijia kichwani.
Ninapojaribu kufananisha na maisha yetu halisi, huu ni uwezo wa kuvumilia Maumivu, depression, au hali nyingine yoyote inayoweza kutuathiri kimwili na kihisia.
Ulishawahi kuhisi ni bora ufe?
Ulishawahi kuhisi k**a kila kitu katika maisha yako kimefika mwisho?
Kumbe leo hii tunaweza kukupongeza kwa sababu uliweza kusurvive ndio maana bado upo.
Bila shaka katika kipindi hicho, ulihisi hauna thamani tena ya kuishi, ulipata hisia zilizoweka hatarini afya yako na watu wanaokuzunguka.
Guess what?
Maisha ndivyo yalivyo.
Yamejaa nyakati nzuri na nyakati ngumu.
Nyakati za Furaha na nyakati za huzuni.
Next time utakapokutana na nyakati ngumu au zilizojaa maumivu, na zikakufanya uanze kufikiria kujitoa uhai au kuhatarisha afya yako...
K**a mti wa muanzi, ruhusu nyakati hizo zipite.
Usiendelee kushikiria mamumivu hayo moyoni.
Utavunjika!
Ruhusu upepo wa hali hiyo upite. Lakini, usipite na wewe jumla jumla.
Jenga matumaini yatayokusaidia kuvuka katika maumivu na nyakati zote ngumu unazozipitia leo.
Ukiwa na matumaini ya kesho iliyobora, Kesho yenye nuru na Furaha, utaweza kushinda.
K**a unapitia nyakati ngumu au maumivu wakati huu, jifunze kutoka kwa mti huu wa muanzi...
Inama, lakini usivunjike!