19/04/2026
UTAMBULISHO WA MUONEKANO RASMI WA BMH MEDIA 🎤📺
Tunayo furaha kuwatambulisha muonekano rasmi (Official Logo) wa BMH Media, kitengo mahususi kinachoshughulika na habari, utangazaji, pamoja na usimamizi wa maudhui ya kidijitali (YouTube & Meta) ndani ya kampuni ya BMH Entertainment.
Chini ya uongozi wa CEO & FoFounde Amos Kiula , BMH Media imejikita katika kuleta mapinduzi ya kitalamu kwenye ulimwengu wa habari na mawasiliano. Lengo letu ni kuhakikisha kila taarifa, tangazo, na kipindi kinachoandaliwa na BMH Media kinabeba alama ya weledi, ukweli, na ubunifu wa hali ya juu.
Logo hii ni ishara ya uthabiti wetu katika kutoa sauti ya uhakika na kuwa daraja la habari kwa jamii.
ILANI YA KISHERIA (Copyright Notice):
© 2026 BMH Entertainment. Haki zote zimehifadhiwa. Alama hii (Logo) ni miliki halali ya BMH Entertainment. Hairuhusiwi kuitumia, kuinakili, au kuisambaza kwa namna yoyote ile kwa madhumuni ya kibiashara au binafsi bila idhini ya maandishi kutoka kwa uongozi wa kampuni. Ukiukwaji wa ilani hii utapelekea hatua kali za kisheria chini ya mamlaka husika (BRELA, TCRA & COSOTA).
KWA WAFUATILIAJI WETU:
Tungependa kusikia kutoka kwako! Je, umeupokeaje muonekano huu mpya wa logo yetu ya BMH Media? Tupe maoni yako hapa chini! 👇✨