Mchumi Consulting

Mchumi Consulting 🟠Huduma za IT
🟠Masoko mtandaon
🟠Masoko kawaida
🟠Business trainings
🟠Ushauri wa biashara
🟠Semina
(1)

MTEJA HAPIMI BEI PEKEE-FAHAMU TABIA ZA WATEJAKatika biashara kuna somo muhimu unalotakiwa kulifahamu k**a mfanyabiashara...
10/08/2026

MTEJA HAPIMI BEI PEKEE-FAHAMU TABIA ZA WATEJA
Katika biashara kuna somo muhimu unalotakiwa kulifahamu k**a mfanyabiashara ambalo ni “Consumer Behaviour Dynamics.”

Ni somo linalokusaidia kuelewa kwa nini mteja ananunua.

Kwa nini anachagua biashara moja na kuacha nyingine, kwa nini wakati mwingine anakataa bei fulani lakini anakubali kulipa bei kubwa sehemu nyingine, na kwa nini mteja anaweza kubaki mwaminifu kwenye biashara fulani hata k**a kuna sehemu nyingine yenye bei ya chini.

Ukiielewa vizuri tabia ya mteja, utaanza kuangalia biashara kwa macho tofauti.
Utaacha kujiuliza tu, “Niuze kwa bei gani?” na utaanza kujiuliza, “Mteja anaona thamani gani kwenye kile ninachompa?”
Na hapa ndipo wafanyabiashara wengi wanapokosea.

Mfanyabiashara akiona mshindani wake anauza bidhaa kwa bei ya chini, jambo la kwanza analofikiria ni:

“Basi na mimi nishushe bei.”
Na hapo ndipo vita ya bei inaanza.
Mmoja anauza 100,000.
Mwingine anashusha mpaka 95,000.
Mwingine anakuja na 90,000.

Mwisho wa siku, kila mtu anashusha bei, lakini hakuna anayesimama kujiuliza:
“Mteja anachagua biashara kwa sababu ya bei tu?”
Jibu ni hapana.

Bei ni muhimu, lakini siyo kitu pekee ambacho mteja anaangalia.
Mteja anaangalia pia thamani anayopata kwa kile anacholipa.

Hii ndiyo tunaita Perceived Value — kwa lugha rahisi, ni thamani ambayo mteja anaiona na kuihisi kutokana na bidhaa au huduma yako.
Na hapa ndipo mambo yanakuwa interesting.

Fikiria kuna biashara mbili
Tuseme kuna Biashara A na Biashara B.
Biashara A inauza bidhaa kwa:
TZS 100,000
Biashara B inauza bidhaa hiyo hiyo kwa:
TZS 130,000
Kwa kuangalia bei tu, utaona Biashara A ndiyo imeshinda.
Lakini hebu tuangalie upande wa mteja.

Biashara A:
Mteja anasubiri muda mrefu.
Hakuna delivery.
Huduma siyo nzuri sana.
Akipata tatizo baada ya kununua, anapata msaada kwa shida.
Mahali pa biashara siyo rahisi kufika.
Mteja hana uhakika sana na quality.

Biashara B:
Anapata huduma haraka.
Bidhaa inaletwa kwake.
Anaelezewa vizuri kabla ya kununua.
Kuna warranty au support baada ya mauzo.
Malipo ni rahisi.
Anajua akipata tatizo kuna mtu wa kumsaidia.
Anaamini quality ya bidhaa.
Sasa mteja anaweza kusema:

“Ni kweli Biashara A ni rahisi kwa TZS 30,000, lakini Biashara B inanipa vitu ambavyo ni muhimu kwangu.”
Na akaenda Biashara B.
Je, amekosea?

Siyo lazima.
Kwa sababu yeye hakuwa anaangalia TZS 100,000 dhidi ya TZS 130,000 pekee.
Alikuwa anaangalia:
“Kwa hela ninayolipa, ninapata nini?”
Hapo ndipo Perceived Value inapokuja.

MTEJA HAANGALII FEDHA PEKEE
Wakati mwingine sisi wafanyabiashara tunafikiria kwamba gharama ya mteja ni hela anayolipa.
Lakini si hivyo.
Mteja anaweza pia kuangalia:
⏱️ Muda — Nitamaliza huduma kwa muda gani?
😓 Usumbufu — Nitatakiwa kufuatilia mara ngapi?
⚠️ Risk — Nikilipa, nina uhakika nitapata nilichoahidiwa?
🤝 Huduma — Watanihudumiaje?
🚚 Urahisi — Bidhaa itanifikia kwa urahisi?
🔄 Baada ya mauzo — Nikiona tatizo, watanisaidia?
🔐 Uaminifu — Ninaweza kuwaamini?
Kwa hiyo, mteja anaweza kuona bidhaa ya TZS 130,000 ni “nafuu” kwake kuliko bidhaa ya TZS 100,000.
Kwa nini?

Kwa sababu ile ya TZS 100,000 inaweza kumgharimu zaidi kwenye muda, usumbufu, risk na stress.

MFANO MWINGINE: MIGAHWA MIWILI
Hebu fikiria kuna migahawa miwili.

Mgahawa A
Chakula ni TZS 10,000.
Lakini ukifika:
Unasubiri dakika 40.
Mhudumu anachelewa.
Wakati mwingine chakula kiko vizuri, wakati mwingine hakiko vizuri.
Parking ni shida.
Na ukipata tatizo, hakuna anayejali sana.

Mgahawa B
Chakula ni TZS 18,000.
Lakini:
Unaagiza haraka.
Chakula kinatoka kwa muda mzuri.
Quality iko consistent.
Wahudumu wanajua kazi.
Mazingira ni mazuri.
Malipo ni rahisi.
Na ukihitaji msaada, unapata.
Sasa kuna mtu anaweza kusema:
“Kwa nini nilipie 18,000 wakati kuna sehemu ya 10,000?”
Lakini mwingine anaweza kusema:

“Mimi bora nilipie 18,000. Sitaki kupoteza muda wangu na usumbufu.”
Hapo ndipo tunapoona kwamba:
Bei ya chini siyo kila wakati maana yake ni value kubwa.

Na pia:
Bei kubwa siyo kila wakati maana yake ni bidhaa ghali.
K**a mteja anaona anapata thamani inayostahili hela yake, anaweza kulipa.

PERCEIVED VALUE NI NINI HASA?
Kwa lugha rahisi sana:

Perceived Value ni namna mteja anavyoona thamani ya kile unachompa ukilinganisha na kile anachotoa.
Anaweza kutoa:
Pesa
Muda
Juhudi
Uvumilivu
Risk
Stress
Na anatarajia kupata:
Ubora
Urahisi
Usalama
Huduma nzuri
Matokeo mazuri
Comfort
Confidence
Experience nzuri

Kwa hiyo, k**a unataka mteja aone biashara yako ina value, usifikirie tu:
“Tunauza kwa bei gani?”
Anza kufikiria:
“Mteja anapata nini kwa hiyo bei?”

HAPA NDIPO BIASHARA NYINGI ZINAKOSEA
Mfanyabiashara anaweza kusema:
“Bidhaa yangu ni nzuri.”
Sawa.

Lakini mteja anaiona?
Anaelewa kwa nini ni nzuri?
Anaona tofauti yake na bidhaa nyingine?
Anaamini hiyo quality?
Au wewe ndiye unayejua tu kwamba bidhaa yako ni nzuri?
Hili ni jambo muhimu sana.

Value ambayo mteja haioni, haielewi au haiamini, ni vigumu kwake kuithamini.

Kwa hiyo k**a una:
Delivery nzuri — mwambie.
Warranty nzuri — mweleze.
After-sales service — ionyeshe.
Quality nzuri — thibitisha.
Huduma ya haraka — mteja aipate kweli.
Urahisi wa malipo — mweleze.
Uaminifu — ujenge kupitia matendo.
Usifikiri mteja ataona kila kitu mwenyewe.

Wakati mwingine unatakiwa kumsaidia aone value uliyonayo.

KWA NINI MTU ANALIPA ZAIDI?
Hili ni swali ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kujiuliza.

Kwa nini mtu anunue kwangu kwa TZS 150,000 wakati mwingine anauza TZS 120,000?

K**a jibu lako ni:
“Kwa sababu bidhaa yangu ni nzuri.”
Haitoshi.

Jiulize zaidi:
Je, ninampa huduma bora?
Je, ninaokoa muda wake?
Je, ninapunguza risk yake?
Je, ninampa convenience?
Je, anaweza kuniamini?
Je, nikishauza nitakuwa bado niko naye?
Je, experience yake ni nzuri?
Je, bidhaa yangu inampa matokeo bora?
Hizo ndizo sababu zinazoweza kumfanya mteja akubali kulipa zaidi.

USISHINDANE KWA BEI PEKEE
Kuna tofauti kati ya kusema:

“Sisi ni cheap.”
na kusema:
“Sisi tuna value.”
Ukijenga biashara yako kwa bei ya chini pekee, siku mshindani wako akishusha bei zaidi unaweza kuanza kupoteza wateja.

Lakini k**a umejenga biashara ambayo mteja anaiona ina:
Ubora + Uaminifu + Urahisi + Huduma + Experience + Matokeo
mshindani wako akishusha bei kidogo siyo lazima mteja akimbie.
Kwa sababu tayari ana sababu nyingine za kukuchagua.

SWALI LA MUHIMU KWA MFANYABIASHARA
Leo usijiulize tu:
“Bei yetu iko chini kuliko ya mshindani?”
Jiulize:
“Mteja anapata value gani zaidi akija kwetu?”
Na swali lingine ambalo ni muhimu zaidi:

“K**a kesho mshindani wangu atashusha bei kuliko mimi, ni kitu gani kitamfanya mteja wangu bado abaki kwangu?”

K**a una jibu zuri la swali hili, kuna uwezekano mkubwa kwamba una kitu muhimu zaidi ya bei:

UNA THAMANI AMBAYO MTEJA ANAIONA.
Mwisho wa siku, biashara siyo kuhusu nani anauza kwa bei ya chini zaidi.

Ni kuhusu nani anaweza kumpa mteja thamani anayohisi inastahili kile anacholipa.
Mteja haangalii tu bei iliyo kwenye tag. Anaangalia experience nzima.

Na wakati mwingine, TZS 150,000 yenye value inaweza kuonekana nafuu kuliko TZS 100,000 yenye usumbufu.

IMEANDIKWA NA
Paul Chengula
+255 714 260266

Jiunge na channell yetu ya wasap hapo chini kwenye link👇
https://whatsapp.com/channel/0029Va8wXM54dTnFbkbyUv2f

Umewahi kujiuliza kwa nini unafanya kazi kwa bidii kila siku, lakini mwisho wa mwezi faida huioni au biashara imedumaa p...
09/07/2026

Umewahi kujiuliza kwa nini unafanya kazi kwa bidii kila siku, lakini mwisho wa mwezi faida huioni au biashara imedumaa pale pale? Ukweli ni kwamba, kuendesha biashara yenye mafanikio hakuhitaji nguvu nyingi pekee, kunahitaji mbinu sahihi.

K**a unataka kuona mabadiliko ya kweli kwenye kipato chako na unataka kuacha kuendesha biashara kwa mazoea, uko sehemu sahihi.

Nimekuandalia huduma maalum kabisa zitakazokusaidia kuvusha biashara yako hatua inayofuata. Kila huduma nimeifafanua kwa kina hapo chini ili uone jinsi itakavyokusaidia.

1. USHAURI WA KITAALAMU KUHUSU USIMAMIZI WA BIASHARA
Wafanyabiashara wengi wanajua kununua na kuuza, lakini hawajui jinsi ya kusimamia rasilimali zao.

Hapa tutakaa chini na kuangalia mfumo mzima wa biashara yako ili uache kupoteza pesa bila kujua.
👉Uchambuzi wa Biashara Yako: Tutajua wapi unapoingiza pesa zaidi na wapi unapoteza ili kurekebisha makosa haraka.

👉Kuweka Mifumo ya Uendeshaji: Tutakusaidia kuweka utaratibu mzuri hata k**a haupo eneo la kazi, biashara iendelee kujiendesha yenyewe bila wewe kuwepo kila saa.

👉Kupanga Malengo ya Mauzo: Tutapanga mikakati ya wazi ya namna ya kufikia malengo ya faida kila mwezi.

Mfano: K**a una duka la nguo na huwezi kujua duka limeingiza kiasi gani au bidhaa zilizobaki ni zipi, huduma hii itakusaidia kuweka utaratibu wa kujua kila kitu kinachoingia na kutoka

2. NAMNA YA KUTANGAZA BIASHARA YAKO KISASA UPATE WATEJA WENGI
Siku hizi wateja hawatafuti biashara barabarani, wako kwenye simu zao. Usipojua jinsi ya kuwafikia kisasa, utabaki unawaangalia wenzako wakitajirika.

👉Mbinu za Kuvutia Wateja Wapya: Jinsi ya kuandika maneno yanayomfanya mteja atamani kununua bidhaa yako mara moja.
Kujenga Brand Yako: Kukusaidia kufanya biashara yako ionekane ya kipekee na yenye kuaminika ili wateja wasiogope bei zako.

👉Kuwageuza Watazamaji Kuwa Wateja: Mbinu za kuongea na watu wanaouliza "bei gani" ili mwisho wa siku wanunue kweli na wasikimbie.

Mfano: Badala ya kupost picha ya bidhaa tu na kuandika "Njoeni mnunue," tutakufundisha jinsi ya kueleza jinsi bidhaa hiyo inavyotatua shida ya mteja ili avutiwe kukupigia simu mwenyewe.

3. NAMNA YA KUTUNZA MAHESABU KWA AJILI YA KODI NA MIKOPO BENKI
K**a unataka kukua, lazima uache kutunza hesabu kichwani au kwenye vikaratasi vinavyopotea. Benki haziwezi kukupa mkopo mkubwa k**a huna kumbukumbu nzuri za kifedha.

✍️Uwekaji wa Kumbukumbu za Kila Siku: Tutakufundisha au kukuwekea mfumo rahisi wa kuandika kila shilingi inayoingia na inayotoka.

✍️Maandalizi ya Ripoti za Fedha: Kutengeneza taarifa zinazoonyesha mzunguko wako wa pesa kwa usahihi kabisa.

✍️Maandalizi ya Kodi na Mikopo: Kukusaidia kuwa salama na mamlaka za kodi na kukuandalia hesabu zinazokubalika na benki yoyote kubwa pindi unapohitaji mtaji wa kukuzia biashara yako.

Mfano: Unapotaka mkopo wa milioni 20 ili kuongeza mzigo, tutahakikisha una vitabu safi vinavyoonyesha benki kuwa biashara yako inalipa na una uwezo wa kurudisha mkopo huo bila shida.

4. NAMNA YA KUTUMIA MIFUMO YA AI KUPATA WATEJA NA KUONGEZA MAUZO
Teknolojia imerahisisha mambo sana. Siku hizi unaweza kutumia mifumo ya AI (Artificial Intelligence) kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi sana na bila gharama kubwa.

✍️Kutengeneza Maudhui ya Biashara kwa AI: Jinsi ya kutumia AI kuandika makala, meseji za wateja, au kupata mawazo mapya ya biashara yako.

✍️Uchambuzi wa Soko kwa AI: Kutumia mifumo kujua wateja wako wanapenda nini kwa wakati huo na bidhaa gani itauza zaidi.
Mifumo ya Kujibu Wateja: Jinsi ya kuweka mifumo inayoweza kuwajibu wateja wako maswali ya kawaida hata ukiwa umelala au ukiwa busy.

Mfano: Unaweza kutumia mifumo hii kupata mawazo 10 tofauti ya jinsi ya kupromote saluni au mgahawa wako ndani ya sekunde chache, jambo ambalo lingekuchukua siku nzima kufikiria.

5. MAFUNZO YA KUFANYA MATANGAZO YA MTANDAONI YENYE KULETA WATEJA
Kuweka picha tu WhatsApp au Instagram haitoshi. Unatakiwa kulipia matangazo yanayomfikia mtu sahihi anayehitaji huduma yako kwa wakati huo.

✍️Kuset Matangazo ya Kulipia (Sponsored Ads): Jinsi ya kurun matangazo ya Instagram, Facebook, au Google yanayoenda moja kwa moja kwa watu wenye pesa na nia ya kununua.

✍️Kuchagua Walengo Sahihi (Targeting): Kujifunza jinsi ya kuchagua umri wa wateja unaowataka, jinsia zao, na maeneo wanayoishi (kwa mfano Dar es Salaam pekee).

✍️Kupima Matokeo ya Tangazo: Kujua tangazo gani limeleta wateja wengi na lipi limepoteza pesa ili uboreshe zaidi.

Mfano: K**a unauza bidhaa za urembo, tutakufundisha jinsi ya kuwasha tangazo ambalo litaonekana tu kwa wanawake waliopo Dar es Salaam wenye umri wa miaka 20 hadi 40 wanaopenda urembo, badala ya kupoteza pesa kuonyesha tangazo hilo kwa wanaume au watoto.

📌GHARAMA NA JINSI YA KUPATA HUDUMA HIZI
Uzuri ni kwamba huduma hizi zote hazihitaji uwe na mamilioni ya pesa. Bei zetu ni nafuu sana na zinalenga kumsaidia kila mfanyabiashara mdogo na mkubwa.

GHARAMA zetu zinaanza kuanzia Tzs 10,000 hadi Tzs 120,000 tu! Inategemea na ukubwa wa huduma unayochagua.
Usisite, kila siku unayopoteza bila kubadilisha mfumo wako wa biashara unazidi kupoteza wateja na pesa. Chukua hatua sasa hivi!

📞 Wasiliana nami moja kwa moja kupitia simu namba:
0714 260266
0769 218125

AU unaweza kubonyeza link hii hapa chini uje moja kwa moja WhatsApp kwangu tuongee: 👇👉https://wa.me/message/4336JBHTUPKEN1

Tupo Dar es Salaam. Karibu sana tujenge biashara yako ifike kileleni!

TUNATOA HUDUMA ZIFUATAZO​✍️ Ushauri wa kitaalamu kuhusu usimamizi wa biashara​✍️ Namna ya kuitangaza biashara yako kisas...
07/07/2026

TUNATOA HUDUMA ZIFUATAZO
​✍️ Ushauri wa kitaalamu kuhusu usimamizi wa biashara
​✍️ Namna ya kuitangaza biashara yako kisasa upate wateja wengi
​✍️ Namna ya kutunza mahesabu kwa ajili ya kodi na Mikopo Benki
​✍️ Namna ya kutumia mifumo ya AI kupata wateja na kuongeza mauzo
​✍️ Mafunzo ya kufanya matangazo mtandaoni yenye kuleta wateja
​📍 DARESSALAAM
Call: 0714 260266

FAHAMU ZAIDI👇
https://wa.me/message/4336JBHTUPKEN1

"Kukopa sio dhambi, dhambi ni kushindwa kulipa." Lakini je, kauli hii bado ina ukweli kwa uchumi wa Tanzania sasa hivi m...
16/06/2026

"Kukopa sio dhambi, dhambi ni kushindwa kulipa." Lakini je, kauli hii bado ina ukweli kwa uchumi wa Tanzania sasa hivi mwaka 2026?

Ukweli ni kwamba, namba za deni la taifa letu zinatajwa karibia TZS 114 Trilioni (karibu USD 50 Billion),ukuaji wa deni letu umekua kwa 8.97% lazima ujiulize mara mbili mbili kuwa hii kitu ni nini hasa ipo hivi.

Lakini kabla hatujaanza kupata hofu ya kufilisika k**a nchi zingine za ukanda huu, hebu tulitazame hili kwa jicho la kiuchumi kupitia kitu kinachoitwa Debt-to-GDP Ratio (Uwiano wa Deni dhidi ya Pato la Taifa).

K**a mfanyabiashara, chukulia hii k**a kulinganisha jumla ya mikopo ya biashara yako dhidi ya mauzo yako ya mwaka mzima (turnover).
Maana yake ni Debt to-GDP Ratio yetu ni 48.8% mpaka sasa.

Hivi sasa, mashirika ya kimataifa k**a IMF yanaweka ukomo wa 55% hadi 60% k**a "danger zone" kwa nchi zinazoendelea,sisi Tanzania mpaka sasa tupo around 48.8% bado tupo vizuri,kwakua ukivuka hapo, sifa yako ya kukopesheka inashuka.

Nchi zilizoendelea k**a Marekani au Japan zinaweza kubeba hata zaidi ya 120% kwa sababu wana uchumi mkubwa na wanakopa kwa sarafu zao, lakini sisi hatuna anasa hiyo.

Ukiangalia ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kusini hivi sasa mwaka 2026:
-Zambia ilishafikia hatua ya kushindwa kulipa (default) ikiwa juu ya 85%.

-Kenya inapitia presha kubwa ya kifedha ikiwa kwenye 68% - 70%.

-Tanzania tuko wapi? Nominal debt yetu ipo kwenye 48.8%, lakini tukiangalia Thamani ya Sasa ya Deni baada ya punguzo la masharti nafuu (Present Value), tuko vizuri kabisa kwenye 40.6%.

Kwanini nasema Deni letu bado ni Stahimilivu (Sustainable)?

✅ Mikopo ya Bei Ndogo (Concessional Loans): Zaidi ya 58% ya deni letu la nje linatoka Benki ya Dunia na AfDB. Hii ni mikopo yenye riba ya chini ya 1% na muda mrefu wa neema (grace period).

✅ Uchumi wetu unakua: Uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi nzuri ya 6.0% hadi 6.4% kwa mwaka huu. Uchumi ukikuwa kwa kasi kuliko madeni mapya, uwezo wa kulipa unaongezeka.

✅ Pesa Imeenda Kwenye Kazi: Fedha zetu zimeenda kwenye "vifaa kazi" vya kimkakati k**a SGR na Bwawa la Nyerere, ambavyo vikianza kazi kamili vitachochea uzalishaji na kuokoa fedha za kigeni.

✍ Hata hivyo, wapi tunapaswa kuchukua tahadhari?
Presha kubwa iliyopo sasa ni ya ukwasi wa haraka (liquidity risk). Shilingi yetu inaposhuka thamani dhidi ya Dola, tunalazimika kutumia mapato mengi ya ndani ya kodi (TRA) kununua dola ghali ili kuhudumia deni la nje.

✍ Nini Kifanyike?
Ili tusiteleze, lazima tupunguze kabisa mikopo ya kibiashara (Commercial loans) yenye riba kubwa na badala yake tuhamie kwenye mifumo ya Public-Private Partnerships (PPP) ili sekta binafsi ijenge miundombinu.

Kubwa zaidi, tuongeze nguvu kwenye agro-processing na utalii ili kuingiza dola nyingi za kigeni (Exports).

Tuko salama, lakini tunahitaji umakini mkubwa sana kwa sasa.

IMEANDIKWA NA
Paul Chengula
+266 714 260266

FAHAMU ZAIDI KUHUSU PAUL 👇
https://linktr.ee/paulmchumi

Kila mwaka tunaposikia kuhusu Bajeti ya Serikali, wengi wetu huwa tunaona k**a ni mambo magumu ya namba na maneno ya kit...
13/06/2026

Kila mwaka tunaposikia kuhusu Bajeti ya Serikali, wengi wetu huwa tunaona k**a ni mambo magumu ya namba na maneno ya kitalamu yasiyotuhusu kabisa.

Lakini ukweli ni kwamba, bajeti ndio dira ya mifuko yetu kwa mwaka mzima,kuanzia bei ya mafuta ya kupikia sokoni, gharama za vifurushi vya simu, hadi jinsi biashara zetu zitakavyolipa kodi.

K**a mdau wa uchumi na mtu anayependa kuona tukikua pamoja, nimekaa chini na kuchambua kwa kina mabadiliko makubwa ya kodi na tozo yaliyotangazwa kwenye Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Lengo langu ni kuyaweka mambo haya kwa lugha nyepesi na rahisi kabisa kueleweka, ili ujue fursa zako na wapi pa kujipanga vizuri.
Tuingie kwenye mambo yenyewe hatua kwa hatua:

1. Taswira Kuu ya Bajeti (The Big Picture)
Mwaka huu nchi yetu inaingia na bajeti ya kishindo ya TSH Trilioni 62.33. Hili ni ongezeko la 10.3% kutoka bajeti ya mwaka jana (2025/26) ambayo ilikuwa Trilioni 56.49.

Serikali inalenga kuongeza mapato ya ndani hadi 17.1% ya GDP (pato la taifa) na mapato ya kodi kufikia 13.7% ya GDP.

Malengo makuu hapa yako wazi kabisa: kuongeza makusanyo, kupunguza matumizi ya fedha taslimu (cash), kuvutia uwekezaji, na kikubwa zaidi ni kufuta kero za kodi zilizokuwa zinasumbua wafanyabiashara wetu.

2. Misamaha na Motisha Mpya (Habari Njema kwa Wafanyabiashara)
Kwenye upande wa motisha na unafuu wa kodi, kuna mambo ya kufurahisha sana kiuchumi yaliyowekwa safari hii:

👉Wafanyabiashara Wapya: Ukifungua biashara mpya na kupata namba ya TIN, unapewa mwaka mmoja mzima bila kulipa kodi ya mapato. Hii ni fursa ya dhahabu kwa vijana na wajasiriamali kukuza biashara kwanza kabla ya kuanza kukatwa kodi.

👉Mafuta ya Kula ya Ndani: Ili kulinda mifuko yetu tunapoenda sokoni, kodi ya VAT imeendelea kusamehewa kwenye mafuta ya kula yanayozalishwa hapa nchini kwa mwaka mmoja zaidi. Lengo ni kuhakikisha bei ya mafuta inashuka au inatulia.

👉Nguo na Mavazi (Pamba ya Tanzania): K**a unajihusisha na viwanda vya nguo vinavyotumia pamba yetu ya Kitanzania, kodi ya VAT imesamehewa. Hii itasaidia kupunguza bei ya nguo za ndani na kukuza viwanda vyetu.

👉Akiba kwa Serikali (VAT Refunds): Serikali imetenga TSH Bilioni 6.3 kwa ajili ya kurudisha kodi (refunds) kwa wale wanaostahili, jambo linaloongeza mzunguko wa pesa kwa wafanyabiashara.

3. Misamaha Iliyofutwa (Maeneo Yanayobaniwa)
Ili kukuza uchumi na kulinda uzalishaji wa ndani, kuna misamaha ya kodi (VAT) imefutwa kwenye baadhi ya bidhaa zinazotoka nje ya nchi:

👉Nyavu za Kuvulia Samaki: Misamaha ya VAT imefutwa kwa nyavu zinazoagizwa kutoka nje ili kuhamasisha viwanda vya ndani vizalishe nyavu hizi.

👉Chakula cha Mbwa na Paka: K**a unafuga na unaagiza chakula hiki kutoka nje, kodi ya VAT sasa itahusika. Hatua hii inatarajiwa kuingizia serikali mapato ya ziada ya TSH Bilioni 2.55.

4. Ongezeko la Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty)
Hapa sasa ndipo tunapopaswa kuangalia kwa umakini. Kuna ongezeko la 8% la ushuru kwenye bidhaa zifuatazo kwa mwaka 2026/27:
Sigara, Vinywaji vinavyotozwa ushuru (k**a pombe na vinywaji vikali), na bidhaa zingine maalum. Serikali inatarajia kukusanya TSH Bilioni 251.54 kupitia ongezeko hili.

🫵Habari Njema: Mafuta ya petroli hayajahusishwa kwenye ongezeko hili ili kuzuia kupanda kwa gharama za usafiri na bidhaa kutokana na bei ya soko la dunia.

5. Uchumi wa Kidijitali – Malipo ya Lazima Yanaanza
Hili ni eneo kubwa sana la mabadiliko. Serikali sasa inahamia kikamilifu kwenye mifumo ya kidijitali ili kupunguza matumizi ya "cash" na kuziba mianya ya upotevu wa fedha. Malipo ya kidijitali sasa yanalazimishwa kwenye maeneo haya:

Hoteli na Migahawa, Shule na Vyuo, Usafiri wa Ndege na Reli, Usafiri wa Mabasi, Vituo vya Mafuta, Shopping Malls, na ununuzi wa ardhi au nyumba.

Mabadiliko Muhimu ya Kadi na Leseni: Vocha za kukwangua (scratch cards) za muda wa maongezi sasa zinaondolewa maeneo ya mijini. Pia, matumizi ya Lipa Namba na TANQR yatakuwa ni masharti ya lazima ya leseni ya biashara.

Sekta Nyingine: Malipo ya kidijitali ya rejea yatakuwa ya lazima pia kwenye sekta za madini, mifugo, mazao, mbao, uvuvi, na uhamishaji wa mali k**a ardhi, majengo na magari.

6. Tozo za Halmashauri na Uwezeshaji wa Makundi Maalum
Tozo za Halmashauri: Kutakuwa na mwongozo wa kitaifa wa viwango vinavyokubalika kitaifa ili kuzuia halmashauri kujipangia tozo kiholela na kuondoa kero kwa wafanyabiashara na wananchi.

Mikopo ya Halmashauri: Hapa kuna habari nzuri sana kwa vikundi! Ile mikopo inayotolewa na Halmashauri imeongezwa kutoka 10% hadi 15%. Ndani ya asilimia hizi, 10% itaenda kwa Wanawake, Vijana na Wenye Ulemavu, na 5% itatengwa mahususi kwa ajili ya Ujenzi wa Masoko na Maeneo ya Biashara ili kutengeneza mazingira mazuri.

7. Mabadiliko haya yanaanza lini?
K**a mchumi, naona mabadiliko haya yakileta mambo makubwa matano kwenye uchumi wetu:
Kuongezeka kwa uwekezaji wa ndani na nje.
Kukuza viwanda vya ndani na uzalishaji wa bidhaa zetu wenyewe.

Kupana kwa wigo wa walipakodi, jambo linalomaanisha serikali itakuwa na pesa zaidi za miradi ya maendeleo.

Kupungua kwa matumizi ya fedha taslimu (cash) na kuimarika kwa uchumi wa kidijitali.
Kuimarisha ukuaji wa uchumi na kutengenezwa kwa ajira mpya kwa vijana wetu.
Kumbuka, mabadiliko haya yote ya kodi na tozo yanaanza kutumika rasmi tarehe 1 Julai 2026.

IMEADNDIKWA NA
Paul Chengula (Paul Mchumi)
+255 714260266

KUHUSU PAUL👇
https://linktr.ee/paulmchumi

Just imagine mtu kaja ofisini kwangu,lakini bado haniheshimu,ananitania...Geof kusoma na wewe na kunijua nje na ndani is...
07/06/2026

Just imagine mtu kaja ofisini kwangu,lakini bado haniheshimu,ananitania...

Geof kusoma na wewe na kunijua nje na ndani isiwe sababu ya kunikosea heshima😒😀😀

Paul
Whatsapp👉0714 260 266

Eid al-Adha Mubarak! Tunawatakia Waislamu wote furaha na baraka tele.” 🌸
27/05/2026

Eid al-Adha Mubarak!
Tunawatakia Waislamu wote furaha na baraka tele.” 🌸

17/05/2026

Kufanya kazi kwa bidii kila siku kuna maana pale tu tunapoelekeza nguvu zetu sehemu sahihi ili kufikia malengo.

Ili biashara ipate matokeo makubwa, haihitaji tu mipango mizuri ya karatasi, bali inahitaji watu wenye ari ya kufanya kazi.

Mkakati wa biashara unatupa mwelekeo wa wapi tunakwenda, lakini utamaduni mzuri wa mazingira ya kazi ndio unaowapa watu hamu ya kufika huko. Mipango pekee bila mazingira yanayochochea furaha, ushirikiano, na motisha hupoteza nguvu haraka.

Mchanganyiko wa mkakati thabiti na mazingira bora ya kazi ndio siri kubwa ya ukuaji wa kudumu

Paul

KANUNI 6 AMBAZO ULITAKIWA UZIFAHAMU KABLA YA KUANZISHA BIASHARA YAKOJe, unajua siri ya kwanini mitaani kwetu kumejaa "ma...
03/05/2026

KANUNI 6 AMBAZO ULITAKIWA UZIFAHAMU KABLA YA KUANZISHA BIASHARA YAKO

Je, unajua siri ya kwanini mitaani kwetu kumejaa "makaburi" ya biashara zilizozikwa zikiwa bado changa? Tatizo kubwa ni kwamba wengi hupoteza muda mwingi kusubiri "muujiza" wa mamilioni ndipo wathubutu, lakini wakishaanza, unakuta ule mtaji wa jasho unayeyuka k**a barafu ndani ya miezi sita pekee.

Biashara siyo kubatisha; ni sayansi inayohitaji ramani. Kabla ya kufungua mlango wa fremu yako mpya, hizi hapa ni kanuni 6 za kijasusi ambazo zitakulinda usipoteze mtaji wako:

1. Mtaji siyo "Pesa" Pekee
Kosa kubwa la kifikra ni kudhani kuwa mtaji ni pesa taslimu pekee. Katika uchumi wa kisasa, fedha ni matokeo ya mitaji mingine mitatu:

-Mtaji Maarifa: Unajua nini ambacho wengine hawajui? Maarifa ya kutatua matatizo ndiyo yenye thamani kuliko cheti.
-Mtaji Jamii: Hii ni "Nguvu ya Uhusiano" na uaminifu unaokupa taarifa na fursa.
-Mtaji Muda: Jinsi unavyotumia masaa 24 ndiyo huamua k**a utatengeneza utajiri au utabaki maskini.

2. Business Plan siyo Mapambo, ni GPS
Business Plan siyo madaftari marefu ya Kiingereza kwa ajili ya benki pekee; ni ramani ya biashara yako. Bila ramani, utapotea hata k**a una mabilioni.

Mpango wa biashara unakusaidia kuona makosa kwenye karatasi kabla hujaingia mtaani na kupoteza pesa halisi.
Ni bora ugundue kwenye karatasi kuwa biashara haitalipa, kuliko ufungue duka na kugundua hilo baada ya kulipa kodi ya mwaka mzima.

3. Eneo la Biashara ni "Injini" ya Mauzo
Wafanyabiashara wengi hukurupuka kupanga fremu kisa pango ni nafuu, bila kujua kuwa "unafuu" huo unaweza kuwa gharama kubwa ya kukosa mauzo.

Eneo (Location) linaweza kuwa rafiki yako mkubwa au adui yako wa kifo.
Kabla ya kupanga, fanya "Street Audit": Angalia nani anapita hapo, mzunguko wa nyakati (peak hours), na k**a eneo linafikika kwa urahisi (accessibility).

4. Tenganisha "Pesa ya chakula" na "Pesa ya Biashara"
Huu ndio ugonjwa mkuu wa wafanyabiashara wa Tanzania: Kuwa na droo moja.
Pesa ya mauzo, mtaji, na matumizi ya nyumbani zisikae mfuko mmoja.

Wewe ni mwajiriwa wa biashara yako; jilipe mshahara (fixed salary) kulingana na mahitaji yako ya chini na uishi ndani ya kiwango hicho. Ukichota hela ya mboga kwenye mauzo, unaitafuna biashara yako ukiwa hai.

5. Cash Flow ndiyo "Pumzi" ya Biashara
Faida ni makadirio ya kwenye makaratasi, lakini Cash Flow (mzunguko wa pesa) ndiyo uhalisia wa biashara kuishi.
Unaweza kuwa na faida kubwa kwenye karatasi lakini ukashindwa kulipa pango kisa pesa yako imekwama mikononi mwa wateja.
Dhibiti mzunguko wa mzigo (inventory turnover) na punguza kukopesha hovyo ili biashara isikose "oxygen" ya kifedha.

6. Jenga Mifumo, Siyo "One-Man Show"
Ikiwa biashara inasimama au inakufa pale unapougua au kusafiri, basi huna biashara—una kazi uliyojitengenezea mwenewe.

Lengo lako liwe ni kujenga mifumo (systems) na timu inayoweza kuendesha kazi bila uwepo wako wa saa 24.
Tumia "Standard Operating Procedures" (SOPs) ili kila mfanyakazi ajue nini cha kufanya hata ukiwa haupo.

Neno la mwisho: Kuanza biashara ni ujasiri, lakini kuifanya idumu ni utaalamu. Linda mbegu yako leo ili uwe na msitu kesho.
K**a umelipenda andiko langu hapo juu,fanya ku-like,save,comment halafu share kwa wenzio ili nao wajifunze pia

IMEANDIKWA NA
Paul Chengula (Paul Mchumi)
0714 260 266
FAHAMU ZAIDI KUHUSU MIMI NA HUDUMA ZETU HAPA
👇👇👇👇
https://linktr.ee/paulmchumi

Kwa mafunzo ya Biashara,Uchumi,Masoko,na Uwekezaji
Book Now: 0714 260 266

TAZAMA YALIYOMO NDANI YA KITABU CHA:KUZA UCHUMI WAKO-HATUA 18 ZA KUSIMAMIA BIASHARA NA KUKUZA UCHUMI WAKO👇👇1.Hakimiliki ...
29/04/2026

TAZAMA YALIYOMO NDANI YA KITABU CHA:KUZA UCHUMI WAKO-HATUA 18 ZA KUSIMAMIA BIASHARA NA KUKUZA UCHUMI WAKO
👇👇
1.Hakimiliki (Copyright)
2.Utangulizi wa Mwandishi
3.Shukrani (Acknowledgements)
4.Utangulizi

SURA YA 1: Mtego wa “Sina Mtaji” na Uchumi wa Mtaani
1.1 Mtaji ni nini hasa?
1.2 Mbinu za “Bootstrapping”
1.3 Uchumi wa Mtaani: Ugavi na Mahitaji
1.4 Mzunguko wa Pesa

SURA YA 2: Business Plan Inayozungumza na Pesa
2.1 Maana Halisi ya Business Plan
2.2 Vipengele Muhimu vya Business Plan
2.3 Hatua ya Kurudisha Gharama
2.4 Mahesabu ya Mzunguko wa Pesa
2.5 Mpango wa Urithi
2.6 Mfano wa Duka la Vifaa vya Ujenzi

SURA YA 3: Uchaguzi wa Eneo na Gharama za Fursa
3.1 Mtego wa “Pango Nafuu”
3.2 Kusoma “Traffic” na Tabia za Watu
3.3 Foot Traffic dhidi ya Quality Traffic
3.4 Mkataba wa Pango na Hatari za Kisheria
3.5 Miundombinu na Ufikikaji
3.6 Mtego wa Eneo la “Kisasa”

SURA YA 4: Mahesabu ya Biashara – Pesa ya Mboga dhidi ya Pesa ya Biashara
4.1 Kifo cha Biashara: Mtego wa “Droo Moja”
4.2 Jinsi ya Kujilipa Mshahara
4.3 Tofauti kati ya Mauzo na Faida
4.4 Daftari la Mapato na Matumizi
4.5 Usimamizi wa Mzunguko wa Pesa
4.6 Umuhimu wa Akiba ya Biashara

SURA YA 5: Cash Flow – Pumzi ya Biashara Yako
5.1 Cash Flow ni nini hasa?
5.2 Mtego wa Mauzo ya Mikopo
5.3 Kusimamia Gharama za Uendeshaji
5.4 Mzunguko wa Mzigo
5.5 Mfano wa Mama Ntilie
5.6 Siri ya Akiba ya Dharura

SURA YA 6: Masoko na Branding – Kutengeneza Jina Linalouza
6.1 Tofauti kati ya Masoko na Branding
6.2 Kujenga USP
6.3 Saikolojia ya Mauzo
6.4 Kufunga Mauzo
6.5 Masoko ya Kidijitali
6.6 Personal Branding
6.7 Huduma kwa Wateja
6.8 Ufungaji wa Bidhaa
6.9 Mfano wa Brand ya Matunda

SURA YA 7: Usimamizi wa Watu na Mifumo – Biashara Inayojiendesha
7.1 Mtego wa “Hakuna wa Kumuamini”
7.2 Siri ya Kuajiri Tabia
7.3 Udhibiti wa Ndani
7.4 Taratibu za Kawaida (SOPs)
7.5 Motisha na Nidhamu
7.6 Mfano wa Hardware ya Juma

SURA YA 8: Changamoto na Hatari
8.1 Hatari ya Soko na Ushindani
8.2 Hatari ya Udhibiti na Sheria
8.3 Hatari ya Uendeshaji na Majanga
8.4 Hatari ya Ukwasi na Madeni Sugu
8.5 Mkakati wa Pivot
8.6 Ustahimilivu wa Kisaikolojia
8.7 Mfano wa Duka la Vifaa

SURA YA 9: Mikakati ya Kutanua Biashara
9.1 Ukuaji dhidi ya Kupanuka
9.2 Mitaji ya Kutanua Biashara
9.3 Msingi wa Kupanuka
9.4 Mikakati ya Upanuzi
9.5 Changamoto za Scaling

SURA YA 10: Kodi na Sheria – Serikali K**a Mshirika
10.1 Aina za Kodi
10.2 Tax Avoidance dhidi ya Tax Evasion
10.3 Utunzaji wa Rekodi
10.4 Matumizi ya EFD
10.5 Ukaguzi wa Kodi
10.6 Leseni na Vibali

SURA YA 11: Usimamizi wa Madeni na Mikopo
11.1 Deni Zuri dhidi ya Deni Baya
11.2 Siri ya Leverage
11.3 Uwezo wa Mikopo
11.4 Mbinu za Kupata Mkopo
11.5 Usimamizi wa Mauzo kwa Mkopo
11.6 Uhusiano na Benki
11.7 Mfano wa Saidi dhidi ya Hamisi
11.8 Mbinu za Kudai Madeni Sugu

SURA YA 12: Akili ya Ushindi
12.1 Kushinda Hofu ya Kufeli
12.2 Nidhamu ya Kujitawala
12.3 Upweke wa Uongozi
12.4 Ustahimilivu
12.5 Kuachana na Matamanio ya Haraka
12.6 Fikra za Maono
12.7 Ujasiri wa Kusema “Hapana”

SURA YA 13: Siri ya Mzunguko wa Pesa
13.1 Faida dhidi ya Mzunguko wa Pesa
13.2 Upotevu wa Cash Flow
13.3 Mikakati ya Kupunguza Gharama
13.4 Mbinu za Kudhibiti Cash Flow
13.5 Mfano wa Juma dhidi ya Amos
13.6 Teknolojia katika Cash Flow
13.7 Saikolojia ya Pesa

SURA YA 14: Teknolojia na AI katika Biashara
14.1 AI k**a Mshauri
14.2 Masoko ya Kidijitali
14.3 Ufanisi wa Uendeshaji
14.4 Faida ya Teknolojia
14.5 Mfano wa Huduma
14.6 Maadili ya Kidijitali

SURA YA 15: Uongozi na Utamaduni wa Biashara
15.1 Kutoka Bosi kwenda Kiongozi
15.2 Falsafa ya Ajira
15.3 Utoaji wa Majukumu
15.4 Utamaduni wa Shirika
15.5 Motisha Isiyo ya Kifedha
15.6 Utendaji Unaotegemea Takwimu
15.7 Migogoro na Maamuzi Magumu

SURA YA 16: Uwekezaji Nje ya Biashara Yako
16.1 Kuzalisha dhidi ya Kulinda
16.2 Hisa na Unit Trusts
16.3 Dhamana za Serikali
16.4 Mkakati wa Mali Isiyohamishika
16.5 Utoaji wa Uwekezaji
16.6 Kuvuna Faida
16.7 Uwekezaji katika Nafsi

SURA YA 17: Ulinzi wa Biashara, Sheria na Urithi
17.1 Uelewa wa Umiliki wa Kisheria
17.2 Aina za Kodi
17.3 Mikakati ya Mipango ya Kodi
17.4 Ulinzi wa Haki Miliki
17.5 Mikataba ya Maandishi
17.6 Mpango wa Urithi
17.7 Usimamizi wa Hatari
17.8 Uzingatiaji wa Sheria

SURA YA 18: Upeo wa Kiuchumi na Fedha
18.1 Viashiria vya Uchumi
18.2 Ustahimilivu wa Kodi

___________________________________

BEI YA KITABU NI ELFU TATU(3,000)
Lipia kwa namba ya malipo yetu ya Tigopesa (Mixx) hapo chini,kisha njoo Whatsapp tukutumie

Kumbuka: Kitabu ni softcopy(pdf) tunakutumia kwenye Whatsapp au Email yako

📌 👇👇👇👇👇
LIPIA KITABU HIKI SASA

📌NAMBA YA MALIPO
(Mix by Yass/Tigopesa)
👇👇
0775004955 (Jina Paulo Ignas Chengula)

____________________________________

KISHA bonyeza link hapo chini ili kuja Whatsapp tukutumie kitabu hiki sasa
👇👇👇
https://wa.me/message/4336JBHTUPKEN1
https://wa.me/message/4336JBHTUPKEN1

Address

Mbeya
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00

Telephone

+255714260266

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mchumi Consulting posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mchumi Consulting:

Shortcuts

Share