08/06/2022
*Kuna uwezekano unajiuliza:*
Napata fedha nyingi kila mwezi, hivi huwa zinaishia wapi?
Nawezaje kulipa deni Kwa wakati au kuepuka kabisa kukopa pesa?
Watu wengi hawatambui kuwa wanatumia zaidi kuliko wanavyopata na polepole kuzama kwenye madeni. Walakini unaweza kutumia utaratibu wa kupanga na kuweka kipaumbele cha matumizi yako na kuelekeza pesa zako kwenye mambo ambayo ni muhimu zaidi kwako.
Mchakato wa kuunda mpango wa kutumia pesa zako. Mpango huo wa matumizi unaitwa bajeti.
Kuunda bajeti hukuruhusu kuamua mapema ikiwa utakuwa na pesa za kutosha kufanya kile unachotaka au unachohitaji kufanya. Kwa maana hiyo, hatua ya kwanza katika mpango wa usimamizi wa matumizi na kufikia malengo unayoitaji ni kupanga bajeti ya fedha zako. Hebu tufafanue bajeti.
*Bajeti ni nini?*
Ni mchakato wa kukadiria mapato na gharama juu ya kipindi fulani cha wakati wa sasa na ujao. Kwa kawaida huandaliwa na kurekebishwa upya kwa mara kwa mara. Bajeti inaweza kufanyika kwa mtu, familia, kundi la watu, biashara, serikali, nchi, au chombo kingine chochote kinachopata na hutumia pesa.
Kutumia bajeti ya kweli kutabiri matumizi yako kwa muda mrefu mfano mwaka mzima kunaweza kukusaidia sana katika upangaji wako wa kifedha wa muda mrefu. hivyo unaweza kufanya makadirio ya kweli kuhusu mapato na gharama zako katika kila mwaka kwa hivyo, utaweza kutabiri ni pesa ya kiasi gani unaweza kuokoa na kupanga malengo ya muda mrefu ya kifedha k**a vile: kuanzisha biashara yako mwenyewe, Kununua gari, kukarabati nyumba yako, kuweka akiba ya dharura, kufanya uwekezaji au kustafu, kwenda likizo n.k
Ungependa kupata MAARIFA zaidi.
Jiunge na kozi ya
*LIFETIME MONEY PLAN*
Utajifunza Nini?
1. Utangulizi wa elimu ya kifedha
2. Kuelewa dhana ya mapato, matumizi, akiba, uwekezaji
3. Benki (akaunti ya akiba)
4. Vita dhidi ya madeni
5. *Kukuza tabia za kifedha zenye tija*
Kwa uwekezaji wa Tshs.5000 badala ya 20,000
Jisajili sasa kwa kutuma jina lako kupitia whatsapp. 0710845978