Gotoa page

Gotoa page Ukurasa huu ni jukwaa la habari za kitaifa na kimataifa sanjari na burudanie,uelimishaji na matangazo

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imefanikiwa kufikia asilimia 64.88 ya lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka...
20/02/2026

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imefanikiwa kufikia asilimia 64.88 ya lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2025/26 hadi kufikia Desemba 2025.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha makisio ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya, Afisa Mipango wa halmashauri hiyo, Ndugu Bilali, amesema Halmashauri iliidhinishiwa kukusanya jumla ya shilingi 22,243,578,000 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani.

Aidha Bilali amesema kuwa hadi kufikia Desemba 2025, Halmashauri ilikuwa imekusanya shilingi 14,432,648,867.45, sawa na asilimia 64.88 ya lengo la mwaka.

Kwa mujibu wa Afisa Mipango amesema miongoni mwa vyanzo vya mapato vilivyochangia mafanikio hayo ni kodi ya ukumbi, ushuru wa mawe, kokoto, mchanga na kifusi, ada za maegesho ya malori, adhabu na tozo mbalimbali, vibali vya ngoma na sherehe, pamoja na matangazo ya redio.

Vile vile amebainisha kuwa Halmashauri inaendelea kuimarisha mikakati ya ukusanyaji wa mapato ili kuhakikisha lengo lililobaki linafikiwa kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na kilihudhuriwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi

Address

Mawasiliano
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Gotoa page posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Gotoa page:

Shortcuts

Share