20/06/2024
MUHIMU! MUHIMU 🚩🚩*
Habari, kumekuwa na ongezeko kubwa la utapeli mtandaoni hivi karibuni, na malalamiko mengi kutoka kwa watu waliotapeliwa na watu wanaotumia jina la Digital Maarifa Marketing Agency
Sisi, timu ya Digital Maarifa Marketing Agency, tunataka kuweka wazi kuwa hatuhusiki kabisa na shughuli hizi za ulaghai. Sisi ni kampuni halali ya masoko ya kidijitali lililojitolea kutoa huduma bora kwa wateja wetu.
Tunawajulisha umma kuwa hatuhusiki na biashara yoyote inayolipa watu kwa kulike, kutoa maoni, au kushiriki maudhui mtandaoni. Hii ni mbinu ya kawaida inayotumiwa na matapeli, na tunataka kujitenga na vitendo hivyo.
Pia, hatuna magroup yoyote ya Telegram au WhatsApp. Namba yetu rasmi ni +255713606808, ambayo ni namba ya Tanzania. Hatutumii namba za nje.
Ikiwa utapokea ujumbe au ofa yoyote isiyo ya kawaida ikidai kutoka Digital Maarifa, tunakuhimiza uwasiliane nasi mara moja kwa namba iliyotolewa. Tumejitolea kulinda wateja wetu na umma kutoka kwa utapeli huu.
Tushirikiane kutokomeza utapeli na kudumisha uadilifu katika tasnia ya masoko ya kidijitali. Ikiwa una wasiwasi au maswali yoyote, tafadhali usisite kuwasiliana nasi.