23/12/2021
China yaufunga mji wakati visa vya Covid vikiongezeka kote ulimwenguni
China leo imeufunga mji wa wakaazi milioni 13 katika jaribio la kutuliza mripuko mdogo wa Covid-19, wakati mataifa mengine kote ulimwenguni yakipambana na ongezeko kubwa la maambukizi yanayosababishwa na kirusi kipya cha Omicron.
Mji wa Xi'an kaskazini mwa China umefungwa baada ya kutokea visa vya mamia kadhaa ya maambukizi.
Hata hivyo tafiti za awali kutoka Afrika Kusini na Uingereza zimetoa matumaini, kwa kuonyesha kuwa maambukizi ya Omicron yanaonekana kusababisha idadi ndogo ya wagonjwa wanaolazwa hospitali ikilinganishwa na kirusi cha Delta.
Ulaya imeathirika pakubwa na wimbi linaloongezeka, kwa kurekodi asilimia 60 ya visa vyote ulimwenguni kwa wiki moja iliyopita.