21/08/2025
Mimi ni mama wa mtoto mmoja, nilikua naishi kwa dada yangui nikaanzisha mahusiano na shemeji yangu, ananipenda na mimi nampenda. Baada ya dada yangu kujua shemeji aliondoka na tukaanza kuishi pamoja, dada alienda mahak**ani kudai talaka. Wamesumbuana mahak**ani mpaka talaka imepatikana, shida kaka inakuja katika mali za Shemeji ambazo ni yeye alichuma kwani Dada hakua na kazi.
Baada ya kupeana talaka mwaka jana mali zilikua na majina ya watoto kwahiyo hawakugawana. Waliambiwa wabaki kuzisimamia mpaka watoto waatakapofikisha miaka 18 na ambaye alitakiwa kusimamia ni mume wangu. Mwaka huu ndiyo mtoto wake mkubwa kafikisha miaka 18, nyumba hii tunayoishi ina jina lake na hiyo nyingine ambayo anaishi Dada yangu ina jina lake pia na majina ya wadogo zake wawili.
Sasa shida inakuja tu baada ya kufikisha miaka 18 anataka tuondoke kwenye hii nyumba kwani ni nyumba yake, yaani ndiyo kafikisha juzi tarehe 4 anataka kutufukuza. Mimi najua ni wivu wa Dada ndiyo unamsumbua kwakua yehe hapendwi, lakini shida inakuja kuwa huyu mtoto alipokuja kudai alimtukana sana Baba yake, mume wangu ana presha hivyo alipotukanwa ilipanda na kapata kitu k**a strock kalazwa hospitalini.
Nashindwa kuelewa dada kaja na mtoto wake wakati mume wangu yuko hospitalini katoa vitu vyetu kaweka wapangaji, mimi sina kazi, nasina pakwenda, nahofia kumuambia mume wangu kuwa tushafukuzwa kwani hali yake si nzuri naomba suahuri wako kwani kitu pekee chenye jina lake ni kiwanja tu ana kazi sawa lakini nahofia tutaishi wapi kwani nyumba ndiyo tushafukuzwa naomba ushauri kisheria hapa inakuaje?. https://youtu.be/lzMJsBYu1d0?si=tQ1L0Nan2KzMzHlF