09/07/2024
K**a umepambana sana kusimamisha biashara yako mtandaoni bila mafanikio, umefanya matangazo ya kulipia na kupoteza pesa bure, ,umetumia hadi wataalamu wa masoko ya mtandao na bado umefeli;
Basi upo karibu kugundua KOSA ambalo umekuwa ukilifanya muda mrefu…
Kosa ambalo limekufanya kuishi kwenye madeni makubwa.
Kukosa amani, na kudharauliwa mpaka na familia yako.
Ingawa umefanya mambo yote ya muhimu kabla ya kufungua biashara…
• Umechagua wazo zuri sana la biashara
• Umepanga biashara yako kwa umakini mkubwa
• Umefungua tovuti na mitandao ya kijamii na unapost kila siku
Lakini
WATEJA HAKUNA.
Mitandao yako imejaa picha nyingi sana na video ambazo hazisaidii kitu….
Zimekuwa k**a album tu.
Wafanyabiashara 9 kati ya 10 wameshindwa kugundua kuwa KOSA wanalofanya kwenye biashara zao mtandaoni ni kwenye MANENO.
Maneno Huuza
Unatumia maneno gani kuongea na mteja wako?
Jifunze kutumia maneno sahihi umpe mteja wako sababu ya kununua biashara yako.