Elohim BOOKS Distributors.

Elohim  BOOKS Distributors. We are here for you

03/05/2022

Anaitwa .

Jana J2 alihubiri kwenye hema ya Nabii Mkuu Mheshimiwa GeorDavie iliyoko Kisongo Arusha....Na alihubiri kwa dakika kadhaa kumtangulia Nabii huyo ambaye inawezekana walipangana mapema ya kuhubiri.

Kwenye Mahubiri yake alisema "hakuna sababu ya kuhubiri ukitaja mitume na manabii k**a Petro au Yuda ambao hatujawaona kwa macho wala hatujui sura zao."

Alisema yeye ameamua kuhubiri kuhusu Nabii Mkuu GeoDavie na atamtangaza kwa nguvu zake zote na yuko tayari kufa akitangaza jina la GeorDavie Nabii Mkuu na siyo Yesu.

Alidai aliwahienda South Africa alialikwa k**a mwimbaji.....sasa ili aheahimiwe akadanganya yeye ni Nabii mkuu sana kutoka Tanzania, na alipopewa madhabahu kuhubiri akaletewa kiwete akamwombea k**a watumishi wengine wanavyoomba (akimaanisha kwa jina la Yesu) lakini kilema hakupona, mwisho akakumbuka Ngurumo ya Upako na Mungu wa GeorDavie.

Akaanza kuonba kwa jina la ngurumo mungu wa GeorDavie, yule kiwete kupitia mungu wa GeorDavie akapona. Akasema nilipokuja hapa Kuna watu walitegemea nihubiri acha uzinzi, akasema hapana nimekuja kumhubiri Nabii mkuu maana ndiye aliyechagua kumhubiri......Ndiye ampaye kula na kulipa Kodi ya nyumba na atamtangaza Kila mahali maana kumtangaza yeye ni kupata promotion.

Halafu Nabii akawa nyuma na anatikisa kichwa....anagurahia sifa anazozipata kutoka kwa kiumbe k**a yeye. Akamzawadia milioni 2 na kumpa mil 1 Kila mwezi kwa miezi 10.

Inasikitisha sana😭😭😭😭
Kwa upande wangu nikimsikia mtu anashuhudia na kunisifu vile, nitazima maiki na kularua mavazi yangu nibaki uchi ili watu wanione ni mtu k**a wao na sina sehemu Yoyote kugusa utukufu wa Bwana hata robo.

Najiuliza tu neno moja, Huyu Nabii mkuu au bashando hajajua Bado sauti ya Neno hili na uzito wake? “Mimi ni Bwana; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu.” Is 42:8

Matebdo 14
Makutano walipoona miujiza aliyoifanya Paulo wakapaza sauti zao, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu. Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng'ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano kumpa Paulo na Barnabas. Barnaba na Paulo, waliposikia wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya (mnataka kutukosanisha na Mungu?) Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo.....sasa mbona mnatusujudia na kutusifu sisi?

Mitume wa kabisa la kwanza walikuwa ni wanyenyekevu sana......baada ya Petro na yohana kumnyanyua kiwete watu wakaanza kuwatazama wao......“Hata Petro alipoyaona haya akawajibu wale watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi?” Mat 3:12

Walikuwa wanajua kumpa Bwana utukufu afanyaye yote hayo......Hata Roho mtakatifu Yesu alisema hatanena kwa shauri lake mwenyewe Bali yote atayatoa kwangu na atanishuhudia Mimi......INAKUWAJE NINYI MNAMSHUHUDIA MTU NA KUMWINUA YEYE😠

By
Kuhani Mwakalambo

Kinasambazwa popote ndani ya Tanzania.
26/12/2021

Kinasambazwa popote ndani ya Tanzania.

We invite you to our educative books, contact us and get you're books.Jipatie vitabu vfuatavyo upate maarifa mapya. Kita...
22/10/2017

We invite you to our educative books, contact us and get you're books.

Jipatie vitabu vfuatavyo upate maarifa mapya.

Kitabu cha "METHALI 170 NA MAANA ZAKE" kina wafaa watu wote mfano waandishi wa vitabu,majarida, makala, watangazaji, wanafunzi wate, watafiti, walimu, na yeyeto anayependa kujua methali kwa kina.

Kitabu cha "FIKRA NI LANGO LA MAFANIKIO" kina mfaa kila mtu ili kuongeza uelewa kuhusu fikra na namna ya kuzitumia ili kuganikiwa katika maisha.

Kitabu cha "MUNGU ANAKUSUDI KUKUPITISHA SHULENI" kina toa siri za kufanikiwa darasani huku ukiwa na MAFANIKIO mazuri ya kiroho na Mungu.

Nyote karibuni.

Address

Elieza. Elisha@yahoo. Com
Dar Es Salaam
1990

Telephone

+255768281975

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Elohim BOOKS Distributors. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share