02/08/2020
UJUMBE WA LEO: HIZI NDIO MBINU KUU ZINAZOWEZA KUKUSAIDIA KUUPATA UTAJIRI
1. Epuka kampani na watu wasio na malengo wala mawazo mapya kimaendeleo.
Ili kufanikiwa katika maisha inabidi ukae na watu makini wenye PLAN na idea za kimaendeleo ili uweze kuongeza mbinu na maarifa katika kuongeza kipato, usipende kukaa na watu wenye story za michezo, mizaha,utani, muziki, umbea, siasa, mapenzi na porojo nyingine maana huto gain kitu.
2. Okoa muda
Usipende kuwa mtu wa kupoteza muda kwenye mambo yasiyosaidia kuongeza kipato chako, usipende kupumzika kupita kiasi fanya kazi k**a mtumwa ili uje uishi k**a mfalme. Hakikisha kila inapopita siku unapiga hesabu umefanya lipi la maana na limekuingizia kiasi gani katika maendeleo yako.
3. Kuwa na mipango ya uhakika.
K**a una nia kweli ya kutoka kweli kwenye umaskini ulionao, hakikisha pia una mipango ya uhakika ya kukutoa pale ulipo. K**a unataka kufanya kitu fulani, tafuta njia itakayokutoa na hasa tafuta mtu mwingine aliyewahi kufanikisha jambo hilo unalotaka kulifanya.
Weka mipango ya uhakika na inayowezekana kwako kuifikia. Jifunze haya yote kwa wale waliofanikiwa zaidi yako. Unapokuwa na mipango ya uhakika inakuwa ni rahisi sana kwako kuifatilia na kiutekeleza. Acha kupanga mipango yako bila ya kuifatilia, ipange mipango yako kisha uifatile. Ikiwa huwezi kufatilia mipango yako nani ataifatilia?
4. Jifunze kutokukata tamaa mapema.
Hii ni njia muhimu sana kwako ya kukufanya wewe kuwa tajiri na kukutoa kwenye umaskini ulionao. Ukiwa na uwezo wa kupambana na vikwazo, ndicho kitu kitakachokufanya ufanikiwe zaidi, na si kukata tamaa na kuacha. Kila safari ya mafanikio ina changamoto zake na vikwazo vyake, hivyo inabidi kukabiliana navyo.
Utaweza kufika kule unakotaka , ikiwa utakuwa uko tayari kupambana na vikwazo vitakavyotokea njiani. Vikwazo vyote ni nafasi ya kufanikiwa k**a utajifunza kitu kwenye hivyo vikwazo au matatizo yanayokuzunguka.
5. Jifunze kufanyia kazi ndoto zako kila siku.
Hii iko wazi kabisa ikiwa utaendelea kufikiria tu, unalofikiria litaendelea milele kubaki kwenye fikra zako na si zaidi. Ni lazima ufanye mambo kwa vitendo ili uweze kujikwamua na umaskini. Unatakiwa kuanzia mahali fulani hasa pale ulipo.
Mpaka utakapoanza ndipo utakapopata matokeo yatakayokusaidia kuweka misingi bora na mwelekeo wako. Ndege ni lazima ianze kwa kuruka inapofika hewani huanza kujiweka sawa ili upate mwelekeo mzuri wa kule inakokwenda.
Ni lazima uanze na mahala fulani popote, si lazima iwe mahala maalumu k**a unavyofikiri, wewe anza tu kufanyia kazi ndoto zako mambo mengine yatajipanga mbele ya safari. Acha kusita sita fanyia kazi ndoto zako ili ufanikishe kile unacholenga.
6. Jifunze kuwa na bajeti maalumu katika maisha yako.
Unapokuwa na bajeti hii itakusaidia wewe kuwa na taarifa nyingi za matumizi na mapato ya pesa zako binafsi na za biashara zako. Ikiwa kila siku unaishi maisha ya kutoweka kumbukumbu hiyo itakusababishia kutojua wakati unapopoteza fedha bila ya sababu hadi hali yako itakapokuwa mbaya zaidi.
Jijengee utaratibu wa kujiwekea bajeti hii itakufanya hautatumia pesa hovyo na hizo pesa utakazozotunza zitakusaidia sana katika kuwekeza pale zitakapokuwa nyingi na hatimaye zitakutoa kwenye umaskini.
7. Jijengee tabia ya kijiendeleza zaidi.
Ni watu wachache sana ambao huwa na tabia ya kujiendeleza kwa kujisomea mara baada ya kumaliza masomo. K**a unataka kuondokana na umaskini hakikisha unasoma mambo mengi na mapya ili kukabiliana na changamoto zaidi za dunia ya sasa.
Bahati mbaya sana mfumo wetu wa elimu tulionao sasa hautusaidii sana kuhusiana na hali halisi ya maisha yetu, hivyo usifikirie kwamba kwa vile umefika chuoni, basi una kila nyenzo ya kukufanya ufanikiwe. Unatakiwa kuendelea kujifunza, watu wenye mafanikio ni watu wakujifunza sana katika maisha yao yote.
Kumbuka ukitaka kufika hadi kwenye kilele cha mafanikio unaweza endapo tu utaamua mwenyewe, hizo ndizo njia muhimu unazoweza kuzitumia kukutoa kwenye umaskini ulionao......
8. Chunguza na kuzifanyia kazi fursa zinazopatikana mahali na wakati husika.
Siku zote fursa zinazojitokeza katika eneo huihitaji uchunguzi wa kina ili kuzibaini, jitahidi kufanya utafiti ujue ni fursa gani katika eneo ulilopo au popote na unaeza ukaitumia vipi kujiendeleza kisha ifanyie kazi. Usiwe mtu wa kuzubaa na kushangaa shangaa, you must be flexible
9. Epuka mapenzi na utani katika kazi
Ni ngumu mno kufanikiwa k**a umeendekeza mambo ya masihara na utani mwingi pamoja na ngono, utapoteza muda wako na rasilimali ikiwemo fedha hatimaye utajiri utabaki kuwa ndoto tu katika maisha yako. Hamna kupe wabaya wanaorudisha watu nyuma kimaendeleo k**a michepuko na wachuna mabuzi yaani wao kila ukigeuka wanakupiga mizinga bajeti yako inakua mara mia.
10. Jitahidi kusoma vitabu na historia ya watu waliofanikiwa kimaendeleo ujue walifanya vipi uongeze maarifa, omba ushauri kwa waliofanikiwa pale inapobidi usijifanye unajua kila kitu, mawazo ya wengine yaweza kukuongezea idea mpya katika kukabili changamoto zingine zitakazo jitokeza katika harakati zako kimaisha na kimaendeleo unazopitia kila siku.
Usipoteze muda wako kuangalia series na season za kikorea, Usipoteze muda wako kujadili maisha ya watu, epuka kupoteza muda kufuatilia umbea na udaku fuatilia fursa na mijadala ya kijasiriamali.
11. Mtangulize Mwenyezi Mungu katika kazi zako Na Mipango yako
Pasipo uwepo wa Mungu katika mipango na kazi zako shetani aeza pata nafasi na kufanikisha mipango yake miovu dhidi yako na kukusababishia anguko, kufilisika, maradhi au kifo na hivyo kukwamisha maendeleo yako. Zipo hila chafu katika kazi mfano chuma ulete katika biashara ambapo washirikina hutumia nguvu za giza kukwamisha watu hivyo ni muhimu kuomba ulinzi wa Mungu siku zote katika harakati zako kimaisha na kimaendeleo.
C&P