¶Elimu na ushauri kwa vijana¶

¶Elimu na ushauri kwa vijana¶ ¶Improving health and life opportunity of the Society ¶
¶ Kutoa elimu na ushauri mbalimbali kwa jamii.

09/02/2026

✍️Mwanaume mwenye busara hutoa nafasi, husikiliza na kuelewa na Utulivu wa mwanaume hujenga amani na heshima katika ndoa🙏 sio kwa binadamu tu bali kwa viumbe vyote

✍️Amani inawezekana tukikubali kuishi pamoja bila kujali tofauti zetu.Sote ni viumbe wa Mungu, tumeumbwa kuishi kwa aman...
30/01/2026

✍️Amani inawezekana tukikubali kuishi pamoja bila kujali tofauti zetu.Sote ni viumbe wa Mungu, tumeumbwa kuishi kwa amani. Upendo hauchagui rangi wala asili🙏

26/01/2026

KIMSINGI OFA HUWA NI MTEGO NA KUNASA HUTEGEMEA AKILI ZAKO MWENYEWE* 🫣

@ *MAISHA*

25/12/2025

Maisha ya kijana ni k**a kiota. Mungu anakupa ndoto, mwelekeo na mustakabali. Lakini si kila anayekuja karibu na wewe anaelewa thamani ya unachokijenga. Wengine huharibu bila hata kujua. Vijana, linda mipaka yako kwa kuzingatia pande zote, chagua marafiki wa hekima, na usiruhusu yeyote akaharibu ndoto za maisha yako pia Maisha yanahitaji uwezo wa kubadilika bila kupoteza mwelekeo.🙏

*Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya*

21/12/2025

Amani na baraka ziwe juu yenu nyote, Nawasalimu kwa upendo na heshima kubwa, nikitambua kuwa tupo pamoja k**a ndugu, kila mmoja akiwa na imani yake, lakini sote tukiongozwa na nia njema ya kufanya yaliyo mema.

Katika safari ya maisha, kumkumbuka Mwenyezi Mungu ni jambo la msingi linalotupa nguvu, hekima na utulivu wa moyo.
Kila mmoja wetu kwa njia yake, ajitahidi kudumisha uhusiano wake na Muumba wake kwa ibada, dua na matendo mema.

Na kwa upendo mkubwa, nawakumbusha tusisite kwenda kusali na kumweka Mungu mbele katika kila jambo, maana sala ni chanzo cha nguvu, mwelekeo na baraka katika maisha yetu ya kila siku. Amina🙏

*SWALI LA LEO*  @22 Jun 25*Kwanini CCTV nyingi hazichukui sauti?*Sababu kuu ni hizi hapa:- 1.  *Sheria na Faragha*Katika...
22/06/2025

*SWALI LA LEO* @22 Jun 25

*Kwanini CCTV nyingi hazichukui sauti?*

Sababu kuu ni hizi hapa:-

1. *Sheria na Faragha*
Katika nchi nyingi (ikiwemo Tanzania), kurekodi sauti bila idhini ya watu walioko kwenye eneo hilo ni kosa la kisheria.
Kwa hiyo, kampuni nyingi za ulinzi au biashara huzima kipengele cha kurekodi sauti ili kuepuka kuvunja sheria za faragha.

2. *Gharama*
CCTV zinazorekodi sauti huwa na gharama kubwa zaidi kwa sababu zinahitaji Microphone ya ubora wa juu, Storage kubwa zaidi kwa sababu sauti huongeza ukubwa wa faili.

3. *Matumizi ya CCTV ni kwa Macho Zaidi*
CCTV zilibuniwa zaidi kwa usalama wa kuona (video surveillance) K**a wizi, uharibifu, au kuingia kwa watu wasiofaa. Sauti si muhimu sana kwa uchunguzi huu, hasa kwenye maeneo ya wazi au yenye kelele.

4. *Changamoto za Kiufundi*
Sauti inaathiriwa na kelele, umbali, upepo, au kuta, hivyo haik**atwi vizuri na kamera za mbali. K**a kamera iko juu au mbali na tukio, sauti haitasikika vizuri, hivyo haiongezi msaada mkubwa.

5. *Ulinzi wa Biashara au Taasisi*
Wamiliki wa maeneo ya biashara wanapendelea kamera zisizo na sauti ili wafanyakazi au wateja wasijisikie wanavamiwa faragha yao.

*MWISHO*
Kuna kamera za kurekodi sauti ambazo ni za kisasa (hasa za IP au Wi-Fi cameras) ambazo hurekodi video na sauti. Zinaweza kutumika majumbani, ofisini, au maeneo yenye uhitaji maalum.
Lakini zinatakiwa zitumike kwa makubaliano ya kisheria.

Asanteni, By Dr Ema

10/10/2024

Story kutoka kwa MASOUD"

Siku moja nilimununulia baba yangu simu kubwa ya laki 360,000 nilipompelekea akapokea kwa furaha sana kisha akasema mwanangu umewaza vyema kunipa zawadi hii, lakin pia na Mimi ninaombi kwako.
Naomba unipeleke mahali uliponunua hii simu,nikashtuka🤔 mbona hivyo Mzee wangu,akasema si kwa ubaya lakin,nikasema ok twende🚶🚶basi haooo mpaka mjini kwa muuza duka,mara Mzee akaniuliza ndo hapa? Nami Eee ndo hapa niliponunua baba, sawa;
Mzee: kijana habar
Muuzaji: salama tu mzee shikamoo!!
Mzee: Malhaba..kijana wangu niliamuagiza aje kuninunulia cmu kwako,lakin alichokikosea kanunua simu ambayo siwezi kuitumia,kwa unmri wangu ni ngumu sana kui-manage.
Muuzaji: Aaah!! Kwahyo tunafanyaje Mzee wangu maana tayari nishauza na nimeikatia rist.
Mzee: Sipo mbali na wewe,naomba uniangalizie simu ndogo ya kiswaswadu yenye thamani ya elfu 40,000 kisha ukate pesa ya rist ambayo ni sh.10,000 na baada ya yote unirudishie hiyo Baki ya 310,000 unaonaje mwanangu ukifanya hivyo.
Muuzaji: haina shida Mzee wangu.
Kijana akawa amefanya hivyo,kisha akarudisha pesa na tukaanza kurudi nyumban,tulipofika home Mzee akanikabidhi hiyo 310,000 kisha akasema mwanangu Asante sana kwa kuiona thamani yangu,ni watoto wachache sana wenye kukumbuka wazazi wao wa kiume,sasa,nimefanya hivyo sababu!! najua mwanangu mbeleni mapambano makubwa ya kimajukumu yanakusubiri,Nenda kaongezee kwenye biashara yako hii pesa Ili mtaji ukue na siku Moja uweze kuimudu family yko na sisi pia maana uzee ndo huo mwanetu wewe ndo mlezi wetu wa kesho.
Aise!! nilijikuta machozi yakinitoka😭😭
Huwezi Amin pesa ile baada ya kuichanganya kwenye mtaji wangu mpka Leo hapa nilipo daaaaaah hakika mungu wa ajabu sana,kwa miaka 12 ndo zimezaliwa nyumba 3 humo shamba za parachichi hekali 200 na mifugo ya kutosha.
Nyumba mbili nimejenga kwa Mzee wangu Moja nimejenga kwangu,,pia biashara ipo moto sana daaah!!🥹
Asante baba yangu,ushauri wako umanilietea mafanikio makubw. Umejifunza nini kutoka kwenye hiyo story

06/04/2023

Siku moja jamaa mmoja alichinja ng'ombe mnono na akachoma vizuri, baadaye akamwambia mke wake: "NENDA NA KAWAALIKE MARAFIKI NA MAJIRANI ZETU WAJE TULE NYAMA."

Basi mke mtu akatoka nje na kuanza kupiga kelele: "OH JAMANI MOTOO, TUNAOMBA MSAADA! MSAADA !! MOTOOO NYUMBANI KWETU !!!"
Kweli ghafla watu walitoka majumbani kwao lakini wengine walijifanya hawasikii chochote.

Basi wale walioingia ndani ya fensi ya nyumba hiyo walijikuta mbele ya "ndafu kubwa" ambapo walikula na kunywa hadi wakasaza.

Lakini baadaye yule jamaa alimgeukia mke wake, akamwuliza: "LAKINI MKE WANGU MBONA WALE ULIOWAALIKA SIWAJUI HATA MMOJA, WENGINE HATA SIJAWAHI KUWAONA. WAKO WAPI MARAFIKI NA MAJIRANI ZETU NILIKUAMBIA UWAAALIKE?"

Mke wake alijibu: "HAWA NDIO MAJIRANI NA MARAFIKI ZETU, WALE WALIOTOKA NYUMBANI KWAO KUTUOKOA SISI NA NYUMBA YETU. WANASTAHILI HESHIMA HII KWA SABABU HAWAKUTARAJIA KUPATA CHOCHOTE KWETU."

Chakujifunza: Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki 🙏

14/01/2023

Jinsi ya kufanikiwa katika biashara mbinu ambazo zitapelekea kupata mafanikio katika kuendesha na kukuza biashara yako

1. Katika Biashara Uza Bidhaa Zenye mashiko
Kupata wateja kwenye biashara yako unatakiwa kuwa na kile wanachohitaji. Huwezi kuuza mwavuli msimu ya jua kali kwani hakuna atakayenunua.

K**a mfanyabiashara, ni muhimu kusoma soko lako siku zote na kuwapatia wateja kile wanachohitaji na sio vinginenyo. Ukiwa na biashara yenye bidhaa ambayo uhitaji wake kwenye soko ni mkubwa lazima watu wanunue.

2. Bei za Bidhaa zako ziendane na Uhalisia
Baadhi ya wafanyabiashara wamejikuta wakidorora kutokana na maamuzi yao ya kuuza bidhaa kwa gharama kubwa ambayo asilimia kubwa ya wateja wanashindwa kumudu. Wakati unapangilia bei ya bidhaa katika biashara yako ni vizuri kuweka akilini nani hasa ni soko lako.

Jiulize katika mazingira uliopo utapata wateja wangapi kwa bei hiyo Hakuna mtu atakayetumia kiasi kikubwa cha fedha kupata bidhaa ambayo wafanyabiashara wengine wanauza kwa bei rahisi zaidi.

3. Kuwa Mpambanaji Katika Biashara Yako
K**a unamiliki biashara au unafikiria kuanzisha biashara hupaswi kuwa mzembe Unatakiwa kuwa tayari kutoa huduma bora kwa wateja wako muda wote.

Kuwa tayari kumshauri mteja kumuelekeza pale ambapo anapata wakati mgumu kuelewa na kuwa mtu ambaye yupo tayari kutoa msaada kwa wateja wake pale wanapohitaji. Usiwe mfanyabiashara ambaye anakaa tu dukani akitegemea wateja watamfuata pasipo ushawishi wowote.

4. Geuza Wateja Kuwa Marafiki Katika Biashara
Kujenga mahusiano kwenye biashara kimsingi yatakufaidisha wewe. Ukiwa na wateja wa muda mrefu kwenye biashara yako basi wateja hao hugeuka kuwa marafiki.

Uaminifu wao kwenye bidhaa na huduma zako utawafanya warudi kwako mara zote pale wanapohitaji kitu.

Hili ni jambo zuri kwa mfanyabiashara kwani ni uwanja mzuri wa kupanua soko. Unaweza kuwaomba wateja hao watangaze biashara yako kwa marafiki zao kupitia mitandao ya kijamii na hata wanapokuwa nyumbani.

5. Usikate Tamaa Katika Biashara
Kuna wakati mambo yatakuwa magumu katika biashara na Mipango yako haitoenda k**a unavyotaka na hali hii huenda ikakuvunja moyo na kukufanya ukose motisha ya kufanya kazi kwa bidii.

Hutakiwi kukata tamaa biashara ni mapambano . asanteni.. Kwa ushauri zaidi tucheki # 0759778666

✍️Ndege pekee mwenye uthubutu wa kumchokoza, kumtishia na kujaribu kumpiga Tai 🦅 ni Kunguru. Huwa anakaa mgongoni mwa Ta...
11/06/2022

✍️Ndege pekee mwenye uthubutu wa kumchokoza, kumtishia na kujaribu kumpiga Tai 🦅 ni Kunguru. Huwa anakaa mgongoni mwa Tai nakuanza kudonoa shingo na kichwa chake. Cha kushangaza Tai huwa hasumbuki kutumia nguvu yake kumjibu au kupigana na Kunguru.Anachokifanya anapaa juu angani, juu zaidi kiasi kwamba kunguru anakosa hewa ya oksijeni anashindwa kupumuwa na anaanguka chini na Tai kuendelea na maisha yake.

FUNZO: Sio kila anayekupinga unapaswa kumjibu, sio kila vita ni ya kupigana, unachopaswa kufanya ni kubadilisha namna unavyoishi na wanaokuchokoza, raise standards zako za maisha. Watesi wako wataanguka chini. Usipoteze muda wako na makunguru sio size yako. ✍️Maadui wanaweza kukukaba shingo yako leo hii lakini muombe mwenyezi Mungu akupandishe kwenye level ambayo wataanguka kwa kukosa hewa.✍️🙏

05/06/2022

😭😪 Ni stori inayoumiza lkn inafundisha pia😭😪 tafadhari soma hadi mwisho💫

*JIKO LA GESI LILIVYOZIMA NDOTO NA UHAI WA FAMILIA YA ABEID FALHUM*
💥Ndugu zangu nataka kuwapa uzoefu na ushuhuda wa kifo Cha jamaa na mdogo wangu Abeid falhum,💥

Asubuhi saa12 ya Tarehe 19, May nimeamka nikashika simu yangu nikakuta Missed Call 08 za Baba yangu. Wakati najiandaa kumpigia nikaona Notification ya msg kuifungua nakuta ujumbe "..abeid na familia yake wamelipukiwa na gesi Jana usiku, wamelazwa Muhimbili.."
Nikampigia Baba, akanambia tu kifupi kuwa taarifa zipo hivyo.
Nikafunga safari muda huo huo kuelekea Muhimbili,
Nikafika Muhimbili haikuwa ngumu Sana kuingia Wodini sababu nilikuwa na kitambulisho kinachonitambulisha kuwa pia ni Medical Personnel.
Mungu wangu naingia wodi ya SEWAHAJI jicho langu linakutana na Ndugu yangu ABEID, ameungua uso wote hauna ngozi, kwa uchungu sana abeid akaanza kulia.
"..akhaa, kaka nimeungua ndugu yangu, nimeungua aisee, niangalie nilivyoungua.." kiukweli Nilishindwa kumkazia Abeid macho yakiwa yamewiva na machozi nikatoka nje ya wodi nikafuta machozi, nilipojiona nipo sawa sawa nikasema sasa naweza kurudi wodini.

Nikamkuta Abeid pia ametulia, nikampa pole kichwani nikasema hapa sina Cha kuongea na Abeid nikatafuta stori ambayo nitazuga nae pale wodini, akatulia! Unajua nilikuwa Nina mawazo na maswali mengi iweje waungue wote watano, nikajisemea hapa Hilo swali ni gumu kuuliza acha akipona atahadithia. Nikamuaga, nikamwambia naomba nikawaangalie pia Watoto, shemeji na Dada wa kazi.. Iko hivi Abeid alikuwa na familia ya watu wanne na yeye watano. Watoto wawili, Mke na Dada wa kazi, Masikini waliungua woteee........

Kesho nikarudi kumjulia hali mara hii Abeid Wala Hakulia tukawa tunapiga stori pale wodini katikati ya stori bila ya kumuuliza akaanza kunihathia
"...ilikuwa mida ya saa1 usiku (jumatano) nipo nyumbn wife akiwa jikoni akaniita jiko linasumbua kuwaka ni jiko lile la plate, basi nikaenda jikoni na mwanangu wa mwisho akanifata, nilipofika jikoni Bali kujali harufu ya Gesi nika'switch jiko, kaka! kiasi cha sekunde *0* wote tukawa tunaogelea kwny moto, nikamshika mtoto kukimbia nae nje sabb mlango ulikuwa umerudishwa tu, wote tukiwa tunawaka nikambwaga mtoto nje, ndani zimejaa kelele nikarudi tena ndani, sebule imelipuka pia lkn mtoto mwngn alikuwa chumbani (chumba Cha watoto) nikaingia huko kote kunawaka mwanangu anawaka nikamvuta akiwa analia huku anaungua nikakimbia nae nje, Hilo tukio lote la kuungua ninalokuelezea ni ndani hata dakk 5 hazifiki aisee, Moto mkali nikamtupa mtoto nje, nikawa nimewabakiza Mke na mfanyakazi ndani nikiwa naungua nikaona zoezi la kuingia na kutoka ni gumu nikaenda jikoni sabb jiko na sebule ni karibu, nikaushika mtungi wa Gesi nauburuza kuelekea nje (huku nawaka moto) nikautupa nje. Nikarudi tena ndani moto umepungua nasikia harufu ya ngozi yangu namna inanuka kwa kuungua na moto, Mke wangu na msichana wa kazi wote wameungua sabb ya uoga walikuwa wanagalagala huku wanaungua, nikawavuta nje, Wote tukalala nje tunasubiri msaada wa majirani, wengine wakawa wanatufunika na kutuzima moto wengine wanajaribu kuudhibiti moto kuunguza Nyumba.."

Anamalizia "...braza toa Gesi nje ndugu yangu ni hatari sana, hatari mnoo!!

Baada ya kumaliza kuongea na Abeid, nikamuaga kutembelea SEWAHAJI wanawake kumuangalia Mke wa Abeid na Dada wa kazi, wameungua aisee ingawa wanaongea macho wanaona lakini moto wa Gesi umeunguza miili Yao vibaya sana..

Tarehe 23 Alfajiri mtoto wa Abeid wa miaka miwili Akafariki dunia haraka Saa7 mchana wa siku hiyo hiyo tukamzika, tarehe 24 ikawa ni siku tunayomfariji Abeid huku tukiwa tumemficha taarifa za kifo Cha mtoto wake,
Tarehe 25 alfajiri Abeid Akafariki, tukasafirisha kuelekea Moshi- Usangi kumhifadhi Abeid, tupo njiani tarehe 26 May alfajiri tukapigiwa simu Dada wa kazi ambae amelazwa Muhimbili amefariki, tukazika haraka Ili tuwahi taratibu za kumhifadhi dada wa kazi, ikawa ni lazima tusafirishe Mwili wa Dada wa kazi maana ni Mkazi wa Masasi...
Tukasafirisha tukazika tukarudi Dar.

Mind you wodini amebaki Mke wa Abeid, na mtoto wa miaka mitano.
Tarehe 31 May Mke wa Abeid Akafariki.

Familia ya watu watano, wanne wamefariki imebaki na Mtoto mmoja tu, Tunamuombea Mwenyezi ampe Ahueni.

Abeid alipokuwa kitandani NENO ambalo alikuwa akisisitiza tuwe makini na Gesi, tufanye namna Gesi hata ikivuja na kulipuka haiwezi kuleta madhara kiasi kile.

🙇‍♂️Linda afya yako kwanza mengine yatafuata ( afya yako ndio mtaji wako )🙋‍♂️💯🙋
01/06/2022

🙇‍♂️Linda afya yako kwanza mengine yatafuata ( afya yako ndio mtaji wako )🙋‍♂️💯🙋

Address

Manuelalex177@gmail. Com
Dar Es Salaam

Telephone

0759778666

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ¶Elimu na ushauri kwa vijana¶ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share