InformationTechonology

InformationTechonology karibu tubadilishane mawazo juu ya IT. karibu tueze kubadilishana mawazo juu ya technolojia

Namna Bora ya ku-manage shule Yako.Karibu upate kilichobora na support Bora.Karibu tukue pamoja.Tupigie +255766500144ugo...
15/06/2023

Namna Bora ya ku-manage shule Yako.
Karibu upate kilichobora na support Bora.
Karibu tukue pamoja.

Tupigie
+255766500144
[email protected]

Jifunze Database kwa lugha ya kiswahili na namna rahisi zaidi.https://www.youtube.com/watch?v=0_DrK43gmHQMuendelezo wa h...
02/06/2023

Jifunze Database kwa lugha ya kiswahili na namna rahisi zaidi.

https://www.youtube.com/watch?v=0_DrK43gmHQ

Muendelezo wa hii utakuja karibuni.

Databaseattributesrelationship in databaseentitykwa kiswahili

23/05/2023

Unakutana na mtu mtandaoni, unapiga video call ukihisi ni muhusika kumbe sie.

Tupo kwenye era ya kua makini na tunachokiona na kukisikia.

21/05/2023

One-time password (OTP) ni nini?

Mifumo hutoa namna ya ku login kwa kutumia neno au tarakimu unique ambazo huweza kutumika mara moja kuruhusu ku login au ku approve kitu.

Watu wengi hawajua kuhusu OTP na imekua ipelekea kupoteza Hela au Akaunti zao za mitandao ya kijamii kwa kuwatumia watu wanapowaomba hizo OTP bila kujua wanawapa access kufanya kitu husika.

Matapeli huweza kutumia Akaunti waliyoipata kukutumia message kukuomba OTP uliyopokea kwenye simu Yako au email Yako, ukiwapatia unakua umewapa access na wanaweza kuishikilia Akaunti Yako.

Mifumo mingi sasa hutumia OTP kuruhusu vitu mbali mbali kabla ya kumpatia mtu neno lililofika kwenye simu au email Yako.

Usiamini kila unachokiona na kukisikia kupitia video, images na audio (Deepfake)Deepfake tunaeza itafsiri kiswahili k**a...
21/01/2020

Usiamini kila unachokiona na kukisikia kupitia video, images na audio (Deepfake)

Deepfake tunaeza itafsiri kiswahili k**a kueka taswira ya mtu au kitu katika picha au video ilhali muhusika hakufanya ivyo. Deepfake imekua ikitumia katika Nyanja tofauti ikiwemo kueka sura za mastaa katika p**n videos, kusambaza habari ambazo sio sahihi, au kulipiza kisasi kwa kumchafua mtu.
Kwa kutumia technology hii unaeza amka asubuhi ukakuta video ya mtu mfano raisi anatoa kauli mbaya ukahisi ni yeye kumbe sio au video za mtu mashuhuri chafu kumbe sio yeye. Kukua kwa technology hii kumeeka ugumu wa kutofautisha video au picha halisi na ambayo sio halisi.
Ukaribu wa technology za kusambaza taarifa mfano whatsapp na facebook kunaongeza athari Zaidi kwa kusambaa kwa political propaganda,
Kuna mjadala sasa juu ya kuaminika kwa video, picha au audio na kuendelea k**a ushahidi maak**ani.
Mfano wa deepfake videos
https://www.youtube.com/watch?v=iTTG2AcOLrM

usisahau ku like page na ku share kwa info nyingi zaid.

❀️Like This Video For 3 Years Of Good Luck ❀️ πŸ”” TURN my POST NOTIFICATION ON and become a part of the for a chance to win a shoutout! ↓ ST...

MICROSOFT KUACHA KU SUPPORT WINDOWS 7 KUANZIA 14 JANUARY 2020.Habari za leo,Baada ya tarehe 14 january 2020 microsoft ha...
07/01/2020

MICROSOFT KUACHA KU SUPPORT WINDOWS 7 KUANZIA 14 JANUARY 2020.

Habari za leo,

Baada ya tarehe 14 january 2020 microsoft hawatokua waki support tena windows 7 hii ina maana gani kitaalam.

Mara kwa mara microsoft hupitia windows zao na kujaribu kuziboresha k**a watagundua kuna mianya ambayo inaweza kudhuru security yako hivyo kuongeza ulinzi katika windows yako, kuacha ku support inamaana hawatokua wakiendelea kutafuta mianya na kutoa hotfixes.

Lakini hii haimaanishi kua Windows 7 sio salama tena ilimradi uwe na namna nzuri ya ku mantain security yako. ni kitu cha kukizingatia pia.

usisahau ku like na ku share kwa info nyingi zaidi.πŸ™ƒπŸ™ƒ

05/01/2020

UTABIRI YANGU JUU YA KAZI ZA IT KUANZIA MIAKA KUMI IJAYO.

Najaribu kufikiri nini muelekeo wa IT kwa Tanzania na ni field gani ya IT itakua HOT.

Kuna miaka kadhaa k**a sita au saba iliyopiata watu waliosomea TELECOM walikua deal sana hivyo kushawishi wanafunzi wengi kukimbilia kusomea TELECOM na baadae walipokuja kutoka walikutana na walichokutana nacho, IT Tanzania inakua sana na uhitaji wa watu wenye fani flani hutegemeana na kipindi husika sasa ivi kuna uhitaji Mkubwa sana wa PROGRAMMERS kwasababu taasisi nyingi zina adopt mifuno ya ki IT, je nini kitafuata baada ya uhitajii wa PROGRAMMERS.

Najaribu kushare my simple forecasting k**a unalolote unaweza comment πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚

FIELD BORA YA MIAKA KUMI IJAYO ITAKUA CYBERSECURITY NA DATA SCIENCE, japokua taasisi hazichukulii mkazo now, ila nina sababu zifuatazo kusema hilo.

DATA au taarifa ni kitu muhimu sana kina kusaidia kufanya maamuzi ukishatengeneza mfumo wa kuziifadhi basi kinafuata ni kuzilinda kutokana sababu tofauti tofauti moja ni business competitor wako au taarifa ambayo haitakiwi kua public available, taasisi pia inaezakua na shauku yakutaka kujua usalama wa mifumo yao hapa sasa unakuja umuhimu wa mtu wa CYBERSECURITY, imagine umeamka na taarifa zote za system za chuo zimefutwa na hacker au taarifa za hospital zimeibiwa.

Katika kuanzalia umuhimu wa DATA SCIENTIST kwa baadae, taasisi nyingi zatakua na data then lazima data ziwasaidie kupata taarifa na kuboresha au kuachana na kitu wanachokifanya, lakini vile vile lazima data ikusaidie kujua k**a kua frauds na vitu vingi.

kwasasa tunakusanya data PROGRAMMING IS HOT tukishapata data inabidi tuzilinde CYBERSECURITY IS HOT lakini pia lazima data itusaidie kufanya maamuzi DATA SCIENCE IS HOT.

hiyo ndio forecasting yangu kwa miaka kumi ijayo kwa upande wa kazi za IT kwa Tanzania, karibu kutoa mawazo yako kupitia comment.

asante kwa kupoteza time kusoma usisahu ku like na ku share.

HABARI YA MOTO. ikiwa ni siku chache baada ya marekani kufanya shambulio nimekutana na hii habari wadukuzi wa iran wamew...
05/01/2020

HABARI YA MOTO.

ikiwa ni siku chache baada ya marekani kufanya shambulio nimekutana na hii habari wadukuzi wa iran wameweza kudukua website ya marekani na kupost picha ya trump akitokwa damu. Bado sijafuatilia kwa kina ila source naiamin

MANUNUZI YA BIDHAA MTANDAONI(MASTERCARD) Habari ya muda huu, Leo nataka nigusie kidogo juu ya malipo ya mtandao(online p...
05/01/2020

MANUNUZI YA BIDHAA MTANDAONI(MASTERCARD)

Habari ya muda huu,
Leo nataka nigusie kidogo juu ya malipo ya mtandao(online payment ) lakini nataka niangalie kwa njia ya mastercard au visa.

Hili suala limekua likishika kasi kipind hiki cha karibu katika nchi yetu, hili limejidhihirisha kwa mitandao mikubwa miwili Airtel Tanzania na Vodacom Tanzania kuanzisha huduma kwa wateja wao kuweza kutengeneza virtual mastercard ni kitu kizuri.

Kwahiyo kwa sasa ukiwa Umetengeneza mastercard yako unaeza fanya malipo dunia nzima kwa kupitia simu yako hii imeondoa usumbufu wa awali ambapo ilikua kueza kuifanya card yako ya benki kuweza kulipa kua na process ndefu hii ni hatua kubwa kwetu.

K**a picha ya payments options inavyoinyesha sehemu nyingi huwa unaeza lipia bidhaa either kwa PayPal au moja kwa moja kwa kujaza details za umuhimu zinazopatikana kwenye card yako.

Unapetengeneza mastercard/visa card yako ina details kuu tatu za umuhimu ambazo mtu unayemlipa ndo hizitumia hizi kutoa hela kwenye card yako nazo ni mwaka na mwezi wa card ku expire, card number na cvs(hivi ni vinamba vitatu).

K**a tunavyojua intenet ni mjumuiko wa watu wenye nia nzuri na mbaya pia, mtu wenye nia nzuri anapozipata hizo namba tatu huwa atachukua kinachomstahili na kuondoka zake bila kuhangaika na details za card yako, ila aina ya pili ya watu huweza kujaribu kutoa hela zaidi na mara kwa mara kiasi kupelekea kupoteza pesa zako. Hizi taarifa tatu kwenye card yako ni zakua nazo makini sana.

Unapochagua option ya kueka details za card yako directly hii ni sawa na kucheza pata potea au unauhakika na store unayonunulia vitu ni watu salama.

Option ya kulipa kwa PayPal inaaminika kua salama zaidi kwani huweki wazi details za card yako kwa mtu unayemlipa lakini pia inaongeza gharama kidogo kwani lazima uwalipe paypal cha udalali kidogo lakini pia inakusaidia maana unapata sehemu yakulalamika na kudai maana PayPal ni organization kubwa.

Option ya PayPal inashauriwa zaidi lakini itakubidi utengeneze akaunti PayPal ambayo utakua unaitumia hiyo kufanya malipo yako.

Tukijaribu kuangalia makampuni haya mawili yaliyotuletea huduma yamejipangaje kutusaidia tusikua na uzoefu na huduma hii na wizi wa kimtandao nina wapa big up kwatenganisha main account ya m-pesa na account kwaajili ya malipo ya mastercard unapotaka kufanya mlipo ya online unaeka kiwango unachotaka tuu kwenye account kwaajili ya mastercard.

Suala la malipo online ni kubwa ngoja tuishie hapo tutaendelea siku nyingine πŸ˜‰πŸ˜‰.

Usisahau ku like na ku share kwa info nyingi zaidi.

Wale tunaoeka mwaka wetu wa kuzaliwa au wa mama au wa mpenzi au mwaka wa kumaliza chuo au  mwaka wa kuzaliwa wa mpenzi w...
21/10/2019

Wale tunaoeka mwaka wetu wa kuzaliwa au wa mama au wa mpenzi au mwaka wa kumaliza chuo au mwaka wa kuzaliwa wa mpenzi wetu wa kwanza,tupo katika hatari zaidi ya password zetu kudukuliwa kirahisi hacker anaweza fanya social engineering (Kukusoma) na kujaribu kuhisi neno lako la siri.

Brute force password cracking - kuna application zinazoweza kutumika kukisia password yako ndo maana mara nyingi unashau...
21/10/2019

Brute force password cracking - kuna application zinazoweza kutumika kukisia password yako ndo maana mara nyingi unashauriiwa kutengeneza password ya mchanganyiko wa number na herufi. hii ni list ya muda ambao izo app zinaweza kutumia kukisia password yako kulingana na mchanganyiko uliofanya.
Usisahau ku like na ku share uwajuze wengine zaidi..πŸ™ƒπŸ™ƒ

Nataka nitenge mda wangu wa ziada kusaidia vijana wenzagu walio na interest za kujua kutengeneza web systems, idadi ya i...
27/05/2019

Nataka nitenge mda wangu wa ziada kusaidia vijana wenzagu walio na interest za kujua kutengeneza web systems, idadi ya inbox itanifanya niamue k**a naweza fanya ivyo au nisuburi, so k**a uko teyari ni inbox

Address

Kimara
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when InformationTechonology posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to InformationTechonology:

Share

Category