Bwabuke Tulia Mwansasu

Bwabuke Tulia Mwansasu ☀️Jipatie nguo za k**e 👗👗na Za kiume👔👔 Kwa bei nzuri
☀️Tunapatikana Kariakoo
0747360347

16/01/2026

NENO LA SIKU.

Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha.

TAREHE 16/01/2026.

SOMO: KUNA MAJARIBU.

Yakobo 1:14 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.”

Yesu wakati anajaribiwa hakutenda dhambi, alishinda jaribu mbele yetu ili nasi tumfuate na tuweze kupata ushindi wa kila siku.
Sote tunajaribiwa na adui huwa anatupitia katika madhaifu yetu. Maeneo tuliyo dhaifu ndiyo shabaha lake!

Ni muhimu kufahamu kuwa majaribu yenyewe si dhambi. Dhambi inaanza pale tunapoanza kuyatenda majaribu au kuyapokea mawazo mabaya katika maisha yetu. Mawazo mabaya yanapokujia, fahamu kwamba wazo hilo halitokani na wewe, bali linatoka kwa adui anayekuletea jaribu, akitegemea utalipokea.

Katika wakati huu, unatakiwa kufanya uamuzi wa kuyakataa majaribu katika Jina la YESU. Unapofanya hivyo, Roho Mtakatifu huja kukusaidia, hukupa nguvu na hekima ya kumpambanua adui.

Yakobo 4:7 “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.”

16/01/2026

NAIBARIKI IJUMAA YANGU.

Nafurahi katika BWANA, maana amenipa KUSHINDA.

Haleluya, YESU ni Mzuri sana.

15/01/2026

NAIBARIKI ALHAMISI YANGU.

BABA yangu wa Mbinguni ni Mpaji wangu; Mimi sitapungukiwa na Kitu. Upendo, Kicheko, Furaha, Karamu, Utele, Chakula vitakuwa pamoja nami.

Haleluya, YESU ni Mzuri.

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bwabuke Tulia Mwansasu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share