19/03/2026
Huyu mubaba kazi yake ni kuendesha boda-boda hapa mtaani kwetu Mimi natokea Nairobi. Alikuwa mtu wa kawaida tu, anatafuta maisha yake ya kila siku. Sasa siku moja, k**a ilivyo kawaida, alimpakia abiria — ambaye Alikuwa ni mwanafunzi wa shule. Akampeleka mpaka shule salama kabisa.
Lakini hapo ndipo mambo yalianza kubadilika kidogo kidogo.
Yule mwanafunzi akaanza kumzoea. Kila siku akimkuta, anapewa lifti bure. Mara nyingine anapewa hata hela ya kununua chakula. Mwanzoni ilionekana k**a msaada tu wa kawaida, mtu mzima kumjali mtoto. Lakini yule mbaba moyoni alikuwa na nia nyingine kabisa.
Siku moja akamwambia yule mtoto, “Leo twende sehemu nzuri, tukale vizuri.” Yule mwanafunzi, kwa sababu bado mdogo na hajui mengi, akakubali. Wakenda kwenye gesti. Wakakaa, wakala, wakanywa soda, maisha yakawa laini. Yule mtoto akaanza kunogewa na ile hali.
Kuanzia hapo, mambo yakaharibika kabisa.
Yule mwanafunzi akaanza kuacha shule taratibu. Asubuhi anavaa nguo za shule, anajifanya anaenda shule, lakini anaishia gesti kwa yule mbaba. Wiki ikapita nzima hajakanyaga shule.
Sasa kuna mwalimu mmoja, siku moja Alikuwa na yeye ameenda gesti kufanya yake kwenye ile gesti Alikuwa na gari yake. Kwa macho ya haraka haraka, akahisi k**a amemwona mwanafunzi wake akiingia pale. Hakuchukulia poa. Akaamua kuchunguza kimya kimya.
Kesho yake akaenda shule, akapiga hesabu ya wanafunzi — kumbe yule mtoto hayupo kabisa siku kadhaa. Akaenda kwa wazazi wake kuwauliza, nao wakasema, “Kila siku anaenda shule.” Hapo mwalimu akajua kuna kitu hakipo sawa.
Basi akaamua kufuatilia mpaka mwisho.
Siku moja akaenda moja kwa moja kwenye ile gesti. Akaingia ghafla. Alipofika ndani, akamkuta yule mwanafunzi yupo pamoja na yule mbaba wa boda-boda.
Hasira zikampanda mwalimu.
Akamwambia yule jamaa, “Hii haiwezekani! Unaishi na mwanafunzi? Hii ni kosa kubwa. Nitaita polisi sasa hivi!”
Yule mbaba akaanza kutetemeka. Akajua kabisa hapa mambo yameharibika. Akaanza kuomba msamaha, “Nisamehe, ukinipeleka polisi nitafungwa miaka mingi…”
Mwalimu akamwangalia kwa ukali, kisha akasema, “Sikukupeleka kwa wazazi, wala sijaita polisi bado. Lakini nataka haki ifanyike. Huyu mtoto mwenyewe lazima akushtaki. Asipofanya hivyo, mimi nitakushtaki mwenyewe.”
Basi yule mwanafunzi, akaambia akawaambia wazazi wake kilichomkuta
Lakini cha ajabu…
Baada ya tukio hilo, yule mwanafunzi akatoweka ghafla. Mpaka leo hajulikani alipo. Wazazi wakaanza wasiwasi, watu wakaanza kujiuliza, “Ameenda wapi?”
Sasa na yule mubaba mwenyewe kakimbia afu na yule mwalimu hajamwambia mtu Siri imebaki ya watu watatu tu