25/10/2017
Biashara
Utangulizi
Sekta ya Viwanda na Biashara hutoa ajira kwa asilimia 62 ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam lina jumla ya wakazi 4,364,541 kati yao watu wenye umri wa kufanya kazi (miaka 15 hadi 64) ni asilimia 66.3 (2,893,691); wengi wao wanafanya kazi za biashara na ajira viwandani.
AINA ZA BIASHARA
Kuna aina tatu za biashara zinazotambuliwa
Biashara ya jumla
Biashara ya rejareja
Biashara ya Kimataifa: - Uagizaji bidhaa toka nje (Import) na Uuzaji bidhaa kwenda nje (Export)
(a) BIASHARA YA JUMLA
Katika Jiji la Dar es Salaam kuna bidhaa za aina mbalimbali pamoja na huduma zinazouzwa kwa kiwango kikubwa na kupelekwa nje ya Mkoa. Bidhaa hizo ni pamoja na zinazozalishwa katika viwanda viliyopo hapa Mkoani na zile zinazoagizwa toka nje ya nchi.
(b) BIASHARA YA REJAREJA
Hii ni biashara inayofanywa kwa kuuza bidhaa zilizonunuliwa jumla na kuuzwa kidogo kidogo kwa mlaji wa mwisho. Bidhaa hizi ni za aina nyingi sana zikiwemo vyakula, vifaa vya ujenzi, mavazi na bidhaa zingine zote za matumizi mbalimbali. Biashara hizi hupatikana katika masoko, maduka na maeneo mbalimbali yaliyotengwa kwa ajili hiyo.
(c) BIASHARA YA KIMATAIFA
Biashara hii inafanyika katika Nchi yetu na nchi za nje ambapo kuna aina: Uagizaji bidhaa toka Nchi za nje (Import) na Uuzaji bidhaa kwenda Nchi za nje (Export)
Uagizaji bidhaa toka Nchi za nje (Import)
Kuna makampuni mbalimbali yanayoagiza bidhaa toka nje ya nchi na kuzisambaza mikoani. Bidhaa zinazoagiza nje ni pamoja na nguo, vifaa vya ujenzi kwa mfano mabati, magari, vipuri vya magari, vipuri vya mashine, baiskeli, pikipiki.
Uuzaji wa bidhaa Nchi za nje (Export)
Bidhaa zinazouzwa nje ya nchi ni pamoja na mazao ya kilimo kwa mfano kahawa, katani, tumbaku, majani ya chai, korosho, karanga na maua. Uagizaji wa bidhaa na uuzaji wa bidhaa nchi za nje unasimamiwa na Taasisi ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tanzania Trade Development Authority (TANTRADE).
MADUKA MAKUBWA
Kuna maduka makubwa yanayouza bidhaa jumla na rejareja na kuagiza bidhaa toka nje. Maduka hayo ni:-
Nakumatt
Shoppers Plaza
Quality Centre
Mlimani City
Imalaseko
Hidary Plaza
J. Mall n.k.
MASOKO
Katika Jiji la Dar es Salaam idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa haraka kutokana na vivutio vya shughuli za biashara na viwanda. Wakazi hawa hupata mahitaji yao kwa kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwenye Masoko. Kuna jumla ya masoko 61 yanayosimamiwa na Halmashauri za Manispaa na moja linasimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Temeke 17
Ilala 24
Kinondoni 19
Halmashauri ya Jiji 1 (Machinga Complex)
Kati ya Masoko ambayo idadi yake imeoneshwa hapo juu, masoko makubwa ni Kariakoo, Tegeta, Buguruni, Temeke Sterio, Kawe, Ilala, Tazara (Veteririnary) na Feri. Serikali imejenga soko kubwa (Machinga Complex) linaloweza kuchukua wafanyabiashara/wajasiriamali 6,000 lakini jengo hili halijatumika/halijachukua wajasiriamali wengi k**a ilivyotarajiwa.
HUDUMA ZA BIASHARA
Kuna huduma za biashara zinazotolewa na Taasisi mbalimbali.
Benki
Kuna Benki za Biashara zipatazo 34 kati ya hizo ni:
CRDB
National Bank of Commerce
Standard Chartered
National Microfinance
Bank of Baroda
Kenya Commercial Bank
International Commercial Bank
FBME Bank
Equity Bank (Tanzania)
Taasisi za Fedha
Kuna taasisi zinazotoa huduma za fedha katika Jiji la Dar es Salaam zikiwa ni pamoja na zifuatazo:-
Efatha
Finca Tanzania Ltd
Maendeleo Bank
Anzania Investment Bank
Tanzania Mongange Refinance Bank
Twiga Barcorp Ltd
Uchumi Commercial Bank Ltd
Convenant Bank for Women
Exim Bank
Maduka ya fedha (Bureau de change)
Maduka hayo huuza fedha za ndani na za kigeni. Maduka hayo ni mengi na yamesambaa katika maeneo mengi ya Jiji.
Majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania
Maduka ya Madawa
Kuna maduka makubwa ya madawa yanayotoa huduma ya kuuza madawa kwa jumla na rejareja.
Salama Phamaceticals Ltd
JB Phamacy etc.
VIWANDA
Sekta ya viwanda ni sehemu muhimu katika uchumi wa Taifa. Mkoa wa Dar es Salaam una viwanda vingi vya aina mbalimbali kufuatana na bidhaa zinazozalishwa.
(a) Viwanda vya nguo viko 36 kati ya hivyo ni:
Karibu Textile Mills Ltd
Tanzania China Friendship Textile
Nida Textile Mills (t) Ltd
21 st Century Textile
Tanzania Uniform and Clothing Corporation Ltd
Quality Textile
Tanzania clothing Co. Ltd
Textile Manufacturers Association
Textile Manufacturers (T) Ltd
Tex Age Tanzania Ltd
Traditional Textiles (T)
Tanganyika Textiles Industries Ltd
Tanzania Knitwear Co. Ltd
Tradenet International Ltd
Varieties Textile Merchant
Viraj Textile
Afri Care
Blanket Textiles Manufacturers Ltd
Blanket & Textile Ltd
Congolin & Co. Ltd
Fomoka Trading and Industry Co. Ltd
J.V. Textile & Cryarments Ltd
K.H. Khimji & Sons
Kilimanjaro Textile Corporation
Fashion Fabric Textile etc
(b) Viwanda vya Kusindika Vyakula
Dyestuffs, Chemicals & Food Colors
Msk Solutions
Olan Tanzania
Power Food Industries
Bakhresa Group
Noble Azania n.k.
Fishmeal and Animal Protein
(c) Viwanda vya Vinywaji
Tanzania Breweries Ltd
Serengeti Breweries Ltd
Cocacola Kwanza Ltd
SBC (Pepsicola)
Chibuku
Tanzania Distritaries
(d) Viwanda vya Kutengeneza Kemikali
Quality Plastics Ltd
Polypet Industries
Mansoor Daya Chemicals Ltd
Plasco Ltd
Twiga Chemical Industries (T) Ltd
Abcom Chemicals Ltd
Afro Chemicals Ltd
Bio-Chemicals Laboratory Supplies Ltd
VIWANDA VIDOGO
Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO) linatoa mafunzo kwa wajasiriamali na kuanzisha viwanda vidogo vidogo k**a vile:-
Utengenezaji wa samani mfano Keko Furniture Works
Utengenezaji wa vyakul vya mifugo (Temeke Growers Meal)
Aluminium Scrap
Mkono Arts & Crafts
Confectionary & Beverages
Wine Products
Gifts, Crafts & Home Decorations
Poultry, Farming Equipments
EPZA (Export Processing Zone Authority)
Hii ni Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji bidhaa kwa ajili ya mauzo ya Nje. Inashughulikia maeneo yaliyotolewa na kuendelezwa kwa ajili ya kuvutia na kutoa fursa kwa wawekezaji wa ndani na nje. Maeneo haya huzalisha bidhaa kwa ajili ya kuuza nje tu (exports). Maeneo ya EPZA kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni:
Benjamin Mkapa Export Processing Zone
Millennium Business Park (Ubungo)
Hifadhi Economic Processing Zone (Ubungo)
Manzava Fabries Co. Ltd
Kurasini Export Processing Zone. Hili eneo bado linajengwa na litahusika sana na mazao ya kilimo.
VITEGA UCHUMI VIKUBWA VYA AINA YA PEKEE
Mkoa wa Dar es Salaam una vitega uchumi vikubwa vya aina ya pekee kwa ukubwa na huongeza mapato Kitaifa. Vitege uchumi hivyo ni:-
Bandari ya Dar es Salaam
Viwanja vya Maonyesho vya Mwalimu J.K. Nyerere
Uwanja wa Taifa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere
Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere