03/10/2018
Karibuni MABOMA Company. Kila siku Mungu amebaki kuwa mwema kwetu ni matumaini yetu Mungu amebaki hivyo kwako pia.
Sisi tupo, MABOMA Company IPO, na maono tuliyobebeshwa tunaamini lazima yatimie ndiyo Mungu aamue vinginevyo.
Tuko imara, tunajifunza vitu vipya kila siku, tukikosea tunajifunza, tukifanikiwa tunarudisha Sifa na utukufu Kwa Mwenyezi Mungu. Kwani Nani k**a Mungu??
Tunatambua kwa kila anayetufahu, haihitaji kumshawishi ili ashuhudie kuwa tuko VIZURI kwenye suala Zima LA ELIMU ya UJASIRIAMALI, Hapa Mungu kawekeza nguvu kwetu. Tunatambua kuwa Kwa nyakati tofauti tumekuwa tukikumbwa na changamoto kadha Wa kadha katika baadhi huduma zetu. Sisi huwa tunazipokea, tunazifanyia kazi, tunajifunza hatimaye tunasonga mbele kwani Ujasiriamali uliokamilika si jambo LA ajabu kukutana na changamoto.
Sisi ni watanzania, watoto Wa Tanzania, tunaipenda Nchi Tanzania na watu wake. Tutasimama kuwasaidia watanzania Kwa kila talanta tuliyonayo hata k**a vikwazo ni vingi. Tunaamini katika msingi Wa 'HAPA KAZI TU' Tutafanya bila kukata tamaa k**a Amir jeshi wetu MKUU, Mhe. raisi Wa Nchi Dr. John Pombe Magufuri, anavyohimiza. Tuko naye tutafanya kazi Kwa manufaa ya kila mnufsika wetu.
MABOMA Company ina vijana wenye vipaji, wana nguvu na ari ya mafaniko halali, tunaahidi kutumia vipawa hivi kuitengeneza Tanzania.
Tunawajaribisha wote, moto wetu Wa kufanya kazi ni mkali na tunakaribisha ushauri toka Kwa yoyote mwenye nia njema na hii Nchi na MAENDELEO ya watu wake, tutapokea na kufanyia kazi..
Huduma zetu zitakuwa zinaoneka kwenye kurasa zetu kila Mara ili twende pamoja.
Karibuni MABOMA Company Kwa huduma BORA zenye kiwango. Mungu ibariki Tanzania, Bariki watu wake HAPA KAZI TU..