BongoNews.co.tz

BongoNews.co.tz Pata habari mbalimbali mahali popote kupitia tovutu yetu ya Bongo News Wasiliana nasi: info@bongonew

ata habari mbalimbali mahali popote kupitia tovutu yetu ya Bongo News Wasiliana nasi: [email protected] Au simu +255719076376

03/12/2024
MRADI WA MAEGESHO CHIMBUYA KULETA UNAFUU KWA WANANCHI, WASAFIRISHAJI Mradi wa ujenzi wa maegesho ya Chimbuya Wilayani Tu...
02/12/2024

MRADI WA MAEGESHO CHIMBUYA KULETA UNAFUU KWA WANANCHI, WASAFIRISHAJI



Mradi wa ujenzi wa maegesho ya Chimbuya Wilayani Tunduma Mkoani Songwe, unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, unatarajiwa kuwa mkombozi kwa wafanyabiashara katika kutatua msongamano wa magari katika barabara ya TANZAM.

Mradi huo ambao ni miongoni mwa miradi iliyofanikiwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia, unahusisha ujenzi wa eneo la Maegesho lenye urefu wa mita 50 na upana wa mita 46, ufungaji wa taa za barabarani kwa urefu wa zaidi ya kilometa tatu, pamoja na ujenzi wa vyoo, bafu, uzio, na ofisi.

Mradi huu ambao utaleta matumaini mapya kwa wasafiri na wafanyabiashara umegharimu Shilingi Bilioni 1.8 na ukarabati wake umefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake.

Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa alitoa mwezi mmoja kwa TANROADS Mkoani Songwe kukamilisha ujenzi wa kituo cha maegesho katika eneo la Chimbuya ili kufikia wiki ya kwanza ya mwezi wa Disemba, maegesho hayo yaanze kutumika kwa kupunguza foleni ya malori kukaa barabarani.

Katika maelekezo hayo pia amemuagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kufunga mizani mitatu inayohamishika (Mobile Weighbridge) ya kudhibiti uzito wa magari katika eneo la Tunduma ili kuongeza kasi ya upimaji wa magari na kupunguza msongamano wa malori yanayosubiria kwa muda mrefu kupima katika mzani mmoja wa Mpemba unaopima Magari yanayoelekea Tunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Kukamilika kwa kituo hicho cha maegesho, kutatoa urahisi kwa Wasafarishaji na wananchi katika eneo hilo kutokana na msongamano wa malori wa muda mrefu na kukwamisha matumizi ya barabara kwa watumiaji wengine.

RAIS SAMIA APONGEZWA KUKUTANA NA WAKAZI WA NGORONGORO Ni kiongozi msikivu, mwenye huruma, asiyependa uonevu  na mwenye k...
02/12/2024

RAIS SAMIA APONGEZWA KUKUTANA NA WAKAZI WA NGORONGORO



Ni kiongozi msikivu, mwenye huruma, asiyependa uonevu na mwenye kutaka haki. Ni Rais Samia Suluhu Hassan ambae tangu aingie madarakani amekuwa akiishi falsafa yake ya 4R.

Falsafa hii inalenga Maridhiano, Ustahimilivu, Maboresho na kujenga upya, kupitia falsafa yake hiyo Desemba 1,2024 Rais Samia alikutana na wakazi wa Ngorongoro.

Hatua hiyo imeonekana kuwavutia wengi na kuamua kumpongeza kwa kuiona haja ya kulimaliza sakata la Ngorongoro kwa njia ya maridhiano.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa amekuwa miongoni mwa watu waliompongeza Rais Samia.

Aidha, Olengurumwa amempongeza Rais kwa hatua ya kukutana na watu wa Ngorongoro, na kusema kuwa, imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa watu hao, na anashukuru angalau sasa amekutana nao.

Rais Samia amesema ataunda tume mbili kuchunguza kinachojiri Ngorongoro na kusababisha kuwapo kwa malalamiko kwa wakazi wa eneo hilo.

Amesema tume moja itachunguza na kutoa mapendekezo kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa Ngorongoro na nyingine itaangalia utekelezaji wa zoezi zima la uhamiaji kwa hiari kutoka eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Rais Samia ameyasema hayo katika Ikulu Ndogo ya Arusha wakati akizungumza na viongozi wa kimila wa jamii ya Kimaasai (Malaigwanani) wanaoishi Ngorogoro.

Taarifa iliyotolewa kwa umma na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais-Ikulu ilieleza kuwa mkutano huo ulifanyika kwa lengo la kuwasikiliza viongozi hao kufuatia kuwapo malalamiko dhidi ya baadhi ya uamuzi wa serikali unaohusu eneo la Ngorongoro.

Hata hivyo Rais Samia amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuimarisha utendaji kazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya serikali na jamii hiyo.

Vilevile, amesisitiza ulazima wa wananchi kushirikishwa ipasavyo katika upangaji na utekelezaji miradi inayopita kwenye maeneo yao.

Ameongeza kuwa, Tanzania ni nchi inayojivunia umoja wa kitaifa na yenye serikali inayowahudumia Watanzania wote. Hivyo, akaitaka Ofisi ya Rais - TAMISEMI kushughulikia changamoto zinazojitokeza ikiwamo kukosekana kwa baadhi ya huduma za msingi za kijamii katika eneo la Ngorongoro.

RAIS SAMIA AWAONGOZA WATANZANIA KUMUAGA DKT. NDUGULILE Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Desemba 2, 2024 ameshiriki Ibada ya...
02/12/2024

RAIS SAMIA AWAONGOZA WATANZANIA KUMUAGA DKT. NDUGULILE



Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Desemba 2, 2024 ameshiriki Ibada ya kuuaga mwili wa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya duniani (WHO) kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile.

Shughuli ya kumuaga mwanasiasa huyo imefanyika kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam na Rais Dkt. Samia pia amesaini kitabu cha Maombolezo.

UTENDAJI WA RAIS SAMIA WAPUNGUZA KASI YA VIJANA KUKIMBILIA MJINI Maendeleo yanayopelekwa vijijini na Serikali ya Rais Sa...
30/11/2024

UTENDAJI WA RAIS SAMIA WAPUNGUZA KASI YA VIJANA KUKIMBILIA MJINI



Maendeleo yanayopelekwa vijijini na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan yamesaidia kupunguza kasi ya vijana wengi kukimbilia mjini kutafuta maisha.

Kusambazwa kwa umeme, maji, barabara na huduma nyengine muhimu kwenye miji, vijiji na vitongoji, pamoja na kuwepo kwa mikopo isiyo na masharti inayotolewa na Rais Samia kumewahamasisha vijana kubaki huko waliko na kuanzisha biashara zinazowaingizia vipato.

Katika Mjadala wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambao wako jijini Arusha kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya hiyo, Rais Samia amesema kwa Tanzania sasa wimbi la vijana kutoka vijijini kuja mjini limepungua.

Amesema hiyo imesababishwa na kupelekwa kwa maendeleo yanayopatikana mijini kule vijijini waliko.

"Wimbi la kuja mjini limepungua kwa sababu kule walipo wanapata yote ambayo mjini yanapatikana, kila kitu walichokuwa wakikifuata mjini sasa wanakipata kule waliko.” amesema Rais Samia.

β€œTanzania tumejitahidi kusambaza umeme katika Vijiji vyote japokuwa sio kila mtu ana umeme ila tunaendelea kuwasambazia wananchi na tunataka umeme ufike kote.

Akizungumzia masuala ya mabadiliko ya tabianchi amesema yana gharimu nchi na akatolea mfano Tanzania inatumia asilimia 4 mpaka 5 ya pato la Taifa kwenye masuala ya kupambana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema moja ya njia ya kukabiliana na hali hiyo ni kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa, badala yake serikali inahakikisha Nishati ya gesi inafika katika maeneo mengi ya nchi na lengo ni kuwaondoa akina mama kwenye matumizi ya kuni na mkaa.

SERIKALI YA SAMIA YATAKA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA SEKTA YA MAJI YALINDWE Utendaji kazi wa kiwango cha juu wa Rais Samia ...
30/11/2024

SERIKALI YA SAMIA YATAKA MAFANIKIO YALIYOPATIKANA SEKTA YA MAJI YALINDWE



Utendaji kazi wa kiwango cha juu wa Rais Samia Suluhu Hassan, umewezesha eneo kubwa la nchi kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama kwa mijini na vijijini hali iliyoifanya Serikali kutaka mafanikio hayo yalindwe.

Ikumbukwe kuwa hadi kufikia Februari 2024, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ilifikia asilimia 79.6 ikilinganishwa na asilimia 77 Februari, 2023.

Kwa upande wa mijini upatikanaji wa maji umefikia asilimia 90 ikilinganishwa na asilimia 88 Februari 2023.

Mafanikio hayo ni makubwa na ndio yamempa nguvu Kaibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuwataka watumishi wa Sekta ya Maji kuhakikisha wanalinda mafanikio yaliyofikiwa katika utekelezaji wa majukumu ya sekta hiyo.

Mhandisi Mwajuma ametoa agizo hilo katika kikao chake na watumishi wa Wizara hiyo jijini Dodoma.

Ikumbukwe kuwa Serikali ya Rais Samia, kupitia Wizara ya Maji, imeweka malengo makubwa ya kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa uhakika wa maji safi na salama kwa wananchi wote nchini.

Malengo haya ni sehemu ya juhudi za kufikia Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kwa mujibu wa mpango wa serikali ni kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inawafikiwa asilimia 95% ya wakazi wa mijini ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wa wananchi wa Vijijini asilimia 85 wawe wanapata huduma ya maji safi na salama ifikapo mwaka 2025.

Malengo hayo yanategemewa kufanikishwa na miradi mbalimbali k**a Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP), ambayo inalenga kuboresha miundombinu ya maji na kuongeza upatikanaji wa maji vijijini na mijini.

Serikali pia inashirikiana na sekta binafsi na mashirika ya kimataifa ili kufanikisha malengo haya.

MSAADA WA KISHERIA WA RAIS SAMIA WAFANIKISHA WANANCHI 2,775 RITA Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia umesaidia w...
26/11/2024

MSAADA WA KISHERIA WA RAIS SAMIA WAFANIKISHA WANANCHI 2,775 RITA



Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia umesaidia wananchi 2,775 kupata vyeti vya kuzaliwa kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).

Msaada wa kisheria wa Mama Samia umekuwa ni chachu ya kuhamasisha wananchi kuujua umuhimu wa kuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Kati ya wananchi 2,775 walionufaika na kampeni hiyo Wanaume ni 1,258 na Wanawake 1,517.

Zoezi la uhamasishaji na kutoa elimu ya umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa liliwafikia wananchi 14,156, anbapo RITA ilihamasisha watu kufanya Usajili wa Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na umuhimu wa kuandika wosia.

Elimu ya uhamasisha bado inaendeleo kutolewa ili kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanafikiwa.

πŸ›‘πŸ›‘ *MAKUYUNI WILDLIFE PARK KUFUNGUA NJIA YA MAFURIKO YA WATALII*πŸ“ *Bodi ya TAWA yaridhishwa na uboreshaji wa miundombinu...
26/11/2024

πŸ›‘πŸ›‘ *MAKUYUNI WILDLIFE PARK KUFUNGUA NJIA YA MAFURIKO YA WATALII*

πŸ“ *Bodi ya TAWA yaridhishwa na uboreshaji wa miundombinu ya utalii*

Na Beatus Maganja, Arusha.

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeanza rasmi utekelezaji wa mikakati ya kuiendeleza na kuiandaa Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park iliyopo Mkoani Arusha Kwa ajili ya kupokea wageni wengi zaidi kwa kuongeza mindombinu ya utalii hususani barabara, ujenzi wa mabwawa ya maji Kwa ajili ya wanyamapori na kuondoa mimea vamizi ndani ya eneo hilo.

Hayo yamesemwa Novemba 24, 2024 na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Dkt. Simon Mduma katika ziara ya wajumbe wa Bodi hiyo ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na TAWA ndani ya Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park.

"Hifadhi hii ni mpya ilikabidhiwa takribani mwaka mmoja uliopita na katika mchakato wakuiendeleza na kuiandaa Kwa ajili ya kupokea wageni kulikuwa na umuhimu wa kuongeza barabara kwenye maeneo haya ili wageni watakaokuwa wanatembelea eneo hili wawe na wigo mpana wa kuiona mandhari nzuri sana ya eneo hili lakini vilevile kutoa nafasi kubwa ya kuona vivutio ambavyo vipo kwenye hifadhi hii" amesema Dkt. Mduma

"leo tumezunguka na tumeona maendeleo ya ujenzi wa barabara, ni kazi ambayo inaridhisha, ni nzuri na ratiba ambayo ipo kwa makubaliano kwenye mikataba Kazi ya ujenzi wa barabara inaendelea vizuri sana hilo tumeridhika nalo" ameongeza" Mduma.

Dkt. Mduma amesema kutokana na eneo la Makuyuni kukumbwa na changamoto ya ukame wakati wa kiangazi kiasi cha kusababisha wanyamapori kutoka nje ya hifadhi hiyo na kwenda kwenye makazi.ya watu, Bodi ya TAWA iliona umuhimu wa kujenga bwawa la kukusanyia maji Kwa ajili ya wanyamapori, hivyo Bodi hiyo imefanya ukaguzi wa eneo litakapochimbwa bwawa hilo na kuridhishwa nalo, na hivyo ujenzi wake utaanza hivi karibuni kwakuwa mikataba imekwisha sainiwa tayari Kwa kuanza kazi hiyo.

Kwa upande wake mjumbe wa Bodi hiyo Profesa Suzanne Augustino ameipongeza Menejimenti ya TAWA na watumishi wote Kwa jitihada kubwa wanayoifanya kuboresha mazingira ya Makuyuni Wildlife Park ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi ushauri na maelekezo yanayotolewa na Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis R. Semfuko.

Aidha Profesa Suzanne ametanabaisha kuwa kutokana na kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Balozi wa utalii wa nchi yetu na uwekezaji wa miundombinu ya utalii unaofanywa na TAWA, Makuyuni Wildlife Park ya miaka mitano ijayo haitakuwa k**a inayoonekana leo badala yake itakuwa Makuyuni yenye mabadiliko makubwa ambayo inafungua njia kwa watalii wengi zaidi lakini pia Makuyuni yenye utofauti mkubwa na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii.

Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ambaye pia ni Kaimu Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini ya TAWA Privatus Kasisi amesema Kitendo cha Serikali kuiamini TAWA na kuikabidhi eneo hilo muhimu kumeipa chachu na nguvu ya kuliendeleza na kulisimamia kwa ukamilifu ili kulifanya liwe bora kwa manufaa ya wakazi wa Mkoa wa Arusha na Taifa Kwa ujumla.

Aidha Kasisi amesisitiza kuwa TAWA itahakikisha inaongeza kasi ya uboreshaji wa miundombinu ya eneo hilo ili kupata watalii wengi na mapato kwa muda mfupi hasa katika mashindano ya AFCON ya mwaka 2027 ambapo Tanzania inatarajia kupokea wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali na Arusha ni moja ya miji ambayo itapokea wageni hao.

Katika hatua nyingine, Kamanda wa eneo la Makuyuni Wildlife Park Andrew Kishe amesema miradi yote inayotekelezwa na TAWA ndani ya Hifadhi hiyo inagharimu zaidi TZS Billioni moja ambayo inajumuisha barabara atakazopewa mkandarasi na zile zinazotengenezwa Kwa kutumia vitendea kazi vya taasisi huku akibainisha kuwa barabara zinazofunguliwa zina mrefu wa Kilometa 18.

Vilevile miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa geti kubwa la kisasa la watalii na bwawa la maji Kwa ajili ya wanyamapori ambapo ujenzi wa miradi yote hiyo inatokana na fedha za ndani ya taasisi ya TAWA.

RAIS SAMIA KIONGOZI MWENYE IMANI THABITI Imani ni moja ya mambo yanayowashinda wengi, kiongozi mwenye imani thabiti ya d...
26/11/2024

RAIS SAMIA KIONGOZI MWENYE IMANI THABITI



Imani ni moja ya mambo yanayowashinda wengi, kiongozi mwenye imani thabiti ya dini huwa na huruma na mwenye kujali.

Hivyo ndivyo alivyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake, amekuwa mstari wa mbele katika kuthamini dini na viongozi wa dini.

Hulka yake hiyo inamfanya kukubalika na viongozi wa dini zote nchini hadi kufikia hatua ya kupewa jukumu la kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Msikiti k**a alivyofanya Novemba 25,2024 mkoni Morogoro.

Rais Dkt. Samia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti wa Al Ghaith uliopo eneo la Kilakala Flats, Mkoani Morogoro.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Msikiti huo, Rais Samia amewasisitiza waumini wa dini ya Kiislami kujenga madrasa nyingi zaidi ili kuwapatia watoto mafunzo ya kiimani ambayo yatawawezesha kuwa na jamii zenye maadili.

26/11/2024

Address

Ohio
Dar Es Salaam
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BongoNews.co.tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to BongoNews.co.tz:

Share