NCHI YETU TV

NCHI YETU TV Media

Dodoma | Serikali imejipanga kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo ya Polio ili kuendelea kuilinda Tanzania dhidi ya ugon...
27/08/2026

Dodoma | Serikali imejipanga kuhakikisha watoto wanapatiwa chanjo ya Polio ili kuendelea kuilinda Tanzania dhidi ya ugonjwa huo, licha ya nchi kutokuwa na mgonjwa wa Polio kwa sasa.

Hayo aliyasema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaj Jabir Shekimweri katika hafla fupi ya ufunguzi wa kampeni ya utoaji chanjo ya Polio iliyofanyika katika Shule ya Msingi Nkuhungu, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Alhaj Shekimweri alisema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali chini ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha afya za watoto nchini, akieleza kuwa watoto wamekuwa sehemu muhimu ya programu mbalimbali za afya zinazotekelezwa na serikali.

Aliongeza kuwa k**a Wilaya ya Dodoma imepewea lengo la kuwafikia watoto 207,096 katika zoezi hilo, ikiwa ni sehemu ya jumla ya watoto 1,003,061 katika Mkoa wa Dodoma wanaolengwa katika maeneo husika.

“Viongozi, watendaji wa serikali, shule, k**ati na bodi za shule wamehamasishwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo, ikiwamo kuwafikishia wazazi ujumbe kuhusu umuhimu wa kuwapeleka watoto kupata chanjo ingawa hatuna changamoto ya mgonjwa wa Polio nchini, ni muhimu kujihami kwa kuwakinga watoto wetu,” alisema Alhaj Shekimweri.

Kwa upande wake, mkazi wa Dodoma, Rosmith Mkoko aliishukuru serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa chanjo hiyo, akiwataka wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo.

“Chanjo ni muhimu katika kuwalinda watoto dhidi ya magonjwa na kwamba wazazi wanapaswa kutumia fursa hii kuhakikisha watoto wao wanapata kinga. Nawashauri wazazi wawalete watoto wapate chanjo hizi ili ziweze kuwalinda,” alisema Mkoko.

Zoezi hilo linatarajiwa kuendelea hadi tarehe 30 Agosti, 2026 kwa kushirikisha jamii, hususani wazazi na walezi, ili kuhakikisha watoto wote waliolengwa wanapata chanjo kwa wakati.

Ruvuma | Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limeungana na wananchi katika kuadhimisha Miaka 20 ya Polisi Jamii kwa kutembele...
27/08/2026

Ruvuma | Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limeungana na wananchi katika kuadhimisha Miaka 20 ya Polisi Jamii kwa kutembelea Shule ya Sekondari Kigonsera iliyopo Wilaya ya Mbinga, ambapo limefanya zoezi la upandaji miti kwa kushirikiana na wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo.

Zoezi hilo lililofanyika Agosti 26, 2026, limekuwa sehemu ya kuweka kumbukumbu ya waasisi na viongozi mbalimbali waliowahi kusoma katika shule hiyo, sambamba na kuhamasisha utunzaji wa mazingira na umuhimu wa kuacha urithi wa kudumu kwa vizazi vijavyo.

Akizungumza katika zoezi hilo akiwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Polisi Ramia Mganga, ametoa elimu kuhusu Polisi Jamii kwa kusisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya ulinzi na usalama, ikiwemo kutoa taarifa za matukio ya uhalifu na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia uhalifu.

Amesema ushirikiano wa karibu kati ya Jeshi la Polisi na wananchi ni msingi wa kujenga jamii yenye amani, usalama na mshik**ano, huku akiwataka wananchi na wanafunzi kuendelea kuwa mabalozi wa amani na utunzaji wa mazingira.

Maadhimisho hayo ya Miaka 20 ya Polisi Jamii yanaendelea kuimarisha mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Dar es salaam | Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoketi Agosti 26, 2026, chini ya Mwenyekiti wa Chama hic...
26/08/2026

Dar es salaam | Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoketi Agosti 26, 2026, chini ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imependekeza jina la Waziri wa Nishati, Deo Ndejembi, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Uamuzi huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha Rose Migiro, baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa utaratibu wa kikatiba, jina la Ndejembi linatarajiwa kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge, hatua inayolenga kukamilisha mchakato wa kumuidhinisha kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Ndejembi ambaye kwa sasa anahudumu k**a Waziri wa Nishati, iwapo atapitishwa na Bunge, atachukua nafasi hiyo kufuatia mchakato ulioanzishwa na Chama Cha Mapinduzi.

Mwanza | Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amewaagiza Maafisa wa Polisi Jamii, wakiwemo waratibu ...
26/08/2026

Mwanza | Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amewaagiza Maafisa wa Polisi Jamii, wakiwemo waratibu wa Polisi Jamii wilaya, Wakaguzi na Polisi Kata, kuendelea kutoa elimu kwa vikundi vya ulinzi shirikishi wakiwemo Sungusungu ili kuimarisha usalama na kuzuia wananchi kujichukulia sheria mikononi.

DCP Mutafungwa amesema maofisa hao wanapaswa kuhakikisha wanatoa elimu kwa makundi hayo juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria.

Kamanda Mutafungwa ametoa maelekezo hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 20 ya Polisi Jamii, yaliyofanyika kimkoa wilayani Kwimba, DCP Mutafungwa amesema vikundi vya Sungusungu vina nafasi muhimu katika ulinzi wa jamii, lakini vinapaswa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria na kuzingatia utu na haki za binadamu.

Kwa mujibu wa Kamanda Mutafungwa, Mkoa wa Mwanza umeweka Wakaguzi na Polisi Kata katika kata zote 191 za mkoa huo kwa lengo la kusogeza huduma za ulinzi karibu na wananchi.

Dodoma | Katibu Mkuu Kiongozi ametoa barua ya kuthibitisha kupokelewa na kushughulikiwa kwa ombi la Makamu wa Rais kuhus...
25/08/2026

Dodoma | Katibu Mkuu Kiongozi ametoa barua ya kuthibitisha kupokelewa na kushughulikiwa kwa ombi la Makamu wa Rais kuhusu kujiuzulu kutoka katika nafasi yake.

Barua hiyo imeeleza rasmi hatua iliyochukuliwa kuhusu ombi hilo, huku taratibu za kikatiba na kiutawala zikitarajiwa kuendelea kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazohusika.

Taarifa zaidi kuhusu hatua zitakazofuata pamoja na hatma ya nafasi hiyo zinatarajiwa kutolewa na mamlaka husika.

Dodoma | Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Umakamu wa Rais wa Jamhu...
25/08/2026

Dodoma | Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Septemba 4, 2026, akisema uamuzi huo umetokana na utekelezaji wa Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika barua aliyoiwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Nchimbi amesema amefanya uamuzi huo kwa heshima na uaminifu, huku akieleza kuwa ataendelea kumuunga mkono Rais na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Nchimbi amesema katika kipindi chote alichohudumu katika utumishi wa umma, amepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Watanzania na viongozi mbalimbali, akiwashukuru kwa imani na ushirikiano waliompa.

Aidha, ameahidi kuendelea kuwa raia mwema wa Tanzania na kutumia nafasi na uwezo wake kuendelea kulitumikia taifa kwa namna nyingine.

Uamuzi huo umeelezwa kupitia taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, huku ikisisitizwa kuwa taarifa rasmi kuhusu hatua hiyo itatolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

24/08/2026

Tanga | Katika Kilele cha Hitimisho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Dokta Mwigulu Nchemba amepongeza jitihada za Chuo hicho na amejionea bunifu za Kisasa zinazotatua Changamoto za Jamii kupitia Tafiti wasifanyazo Wasomi wa Chuo hicho.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Said Ally Vuai akizungumza mbele ya Waziri Mkuu amesema Chuo hicho kwa Sasa kinaendelea Kupiga hatua kwa kuwa na Kozi Muhimu zenye Kuleta mabadiliko Katika Jamii.

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Kimeshiriki Maonyesho ya Wiki ya Elimu ,Ujuzi na Ubunifu Toka August 15 Jijini Tanga ,Maonyesho yaliyoshirikisha Wadau mbalimbali wa Sekta ya Elimu na kuhitikimishwa August 24 Mwaka huu.

24/08/2026

Tanga | Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametembelea banda la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Agosti 24, 2026, jijini Tanga, na kupongeza ubunifu mbalimbali unaofanywa na chuo hicho katika kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu amepata fursa ya kuona bunifu mbalimbali zilizowasilishwa na NIT, ikiwemo mfumo uliobuniwa kwa lengo la kupunguza foleni pamoja na muda wa kusubiri kwa abiria wanaotumia usafiri wa mwendokasi katika vituo.

Dkt. Mwigulu amempongeza mbunifu wa mfumo huo kwa kazi hiyo, akieleza umuhimu wa ubunifu na matumizi ya teknolojia katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuongeza ufanisi katika huduma za usafiri.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuibua na kuendeleza bunifu zinazolenga kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi, huku akiwataka wabunifu kuendelea kutumia fursa za elimu na teknolojia katika kuboresha huduma nchini.

24/08/2026

Mwanza | Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii nchini, CP Alex Mk**a amewataka maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa Jeshi la Polisi kuendelea kuzingatia maadili na kudumisha nidhamu wanapotekelezaji wa majukumu yao ili kujenga uhusiano mzuri na jamii.

CP Mk**a ametoa maagizo hayo , wakati wa maadhimisho ya miaka 15 ya utumishi wa umoja wa askari wa Jeshi la Polisi waliohitimu depo mwaka 2011/2012 (GH Tanzania) huku akidokeza kuwa wananchi wamekuwa wakilalamikia maadili ya baadhi ya maafisa wakaguzi na askari.

Amesema Wananchi wamekuwa wakilalamikia maadili ya baadhi ya maafisa wakaguzi na askari, hivyo ili wawe na mahusiano mazuri na wananchi lazima maadili yawe mazuri.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza, SACP Ndagile Makubi amesema maboresho yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi yanaonekana kupitia ushirikiano wa askari katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Tanga | CRDB Bank imeshiriki katika kilele cha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, kinachofanyika Jijini Ta...
24/08/2026

Tanga | CRDB Bank imeshiriki katika kilele cha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026, kinachofanyika Jijini Tanga, ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa wadau mbalimbali kutoka sekta ya umma na binafsi katika maadhimisho hayo.

Ushiriki wa CRDB Bank unaendelea kuakisi nafasi ya sekta ya fedha katika kuchangia jitihada zinazolenga kuimarisha elimu, ujuzi na ubunifu k**a nyenzo muhimu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Pichani: John Mtani, Meneja Mwandamizi wa Biashara za Serikali, CRDB Bank, akishiriki katika kilele cha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu 2026 jijini Tanga, pamoja watumishi, viongozi mbalimbali na wananchi waliotembelea Banda la CRDB Benki.

Address

DODOMA
Dodoma
0255

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NCHI YETU TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category