Makutano Tv

Makutano Tv To educate, inform, entertain and inspire community through the power of online content.

Mama"s Day runners 2026
12/05/2026

Mama"s Day runners 2026

Mama"s Day runners 2026
12/05/2026

Mama"s Day runners 2026

09/05/2026

Jaribu kuvaa viatu vya mzazi wa mtoto mwenye hali ya usonji ....... UNADHANI NI RAHISI KIASI GANI KUPOKEA TAARIFA YA HALI HIYO KWA MTOTO WAKO?

JE UNADHANI NINI KIFANYIKE KUSAIDIA WAZAZI KUWEZA KUPOKEA NA KUSAIDIA MAISHA JUMUISHI KWA MTOTO ?
Msikilize Dkt Miriam Elisha mtaalamu na mtafiti elimu jumuishi.


-MMMAM

*When Flames Took Everything, Compassion Helped Rebuild Their Future*Pemba Island. A devastating fire at Fidel Castro Se...
05/05/2026

*When Flames Took Everything, Compassion Helped Rebuild Their Future*

Pemba Island.
A devastating fire at Fidel Castro Secondary School in Chake Chake District, Pemba Island, destroyed the girls’ hostel and left 167 students without essential belongings. While no lives were lost, the fire consumed bedding, school uniforms, books, and personal items, disrupting both daily life and learning.

Beyond material loss, the emotional impact was significant. With exams approaching, many students faced uncertainty and distress, affecting their ability to focus and continue their education.
In response, the Family Strengthening Programme in Pemba Island provided immediate humanitarian support. All affected students received essential supplies, including school uniforms, learning materials, and basic personal items such as plates, basins, and cups.
These items helped restore a sense of normalcy, dignity, and readiness to return to school.

The support was officially handed over in collaboration with local authorities, led by the District Commissioner of Chake Chake District, Her Excellency Mrs. Zuhura Mgeni Othman, who commended the timely intervention.
This joint effort highlights the power of partnership in times of crisis, turning loss into recovery and helping students regain hope and continue their education.

Wadau wakutana Mto wa Mbu kujadili utekelezaji wa mradi wa Arusha Standard Project.Semina ya wadau imeanza jana katika e...
05/05/2026

Wadau wakutana Mto wa Mbu kujadili utekelezaji wa mradi wa Arusha Standard Project.

Semina ya wadau imeanza jana katika eneo la Mto wa Mbu, wilayani Monduli, mkoani Arusha, ikiwaleta pamoja viongozi na wataalamu kutoka ngazi mbalimbali kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi wa Arusha Standard Project. Semina hiyo ya siku tatu inatarajiwa kuhitimishwa kesho.

Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa, wawakilishi kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi, Maafisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya, pamoja na Maafisa Maendeleo wa Wilaya, Kata na Watendaji wa Vijiji. Ushiriki wao unalenga kuhakikisha kunakuwa na uelewa wa pamoja na ushirikiano madhubuti katika utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina, mmoja wa washiriki alieleza kuwa semina hiyo ni muhimu katika kujenga mshikamano kati ya wadau na kuweka mikakati itakayosaidia kufanikisha malengo ya mradi huo, hususan katika kuimarisha ustawi wa jamii na maendeleo ya wananchi.

Katika siku ya kwanza, washiriki wamejadili majukumu ya kila mdau, changamoto zinazoweza kujitokeza pamoja na njia bora za kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli za mradi. Aidha, matarajio ni kuwa siku zinazofuata zitahusisha upangaji wa mikakati ya utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ili kuhakikisha mradi unaleta matokeo chanya kwa jamii.

Mkutano huo unatarajiwa kuhitimishwa kesho kwa azimio la pamoja litakaloweka msingi imara wa utekelezaji wa Arusha Standard Project katika ngazi zote husika.

*SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA DINI KUIMARISHA AMANI NA MAADILI NCHINI*_▪︎ Asema dini ni nguzo muhimu ya...
03/05/2026

*SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA DINI KUIMARISHA AMANI NA MAADILI NCHINI*

_▪︎ Asema dini ni nguzo muhimu ya malezi na mshikamano wa Taifa_
_▪︎ Asisitiza jamii kuendelea kuombea na kulinda amani ya nchi_

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na taasisi za dini nchini ili kuimarisha maadili, mshikamano wa kijamii na kudumisha amani ambayo ni msingi wa maendeleo endelevu ya Taifa.

Amesema hayo leo Jumapili, Mei 3, 2026, aliposhiriki ibada katika Kanisa Kuu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mufindi, lililopo Mafinga Mjini, mkoani Iringa.

Akizungumza na waumini, Dkt. Nchemba amesema taasisi za dini zina mchango mkubwa katika kujenga jamii yenye maadili mema, inayozingatia misingi ya haki na uwajibikaji.

“Serikali inaendelea kusisitiza Watanzania wote kuwa wadau wa kuombea na kusimamia amani ya nchi yetu,” amesema.

Ameongeza kuwa mafanikio ya mipango ya maendeleo ya Taifa yanategemea uwepo wa amani.

“Pasipokuwa na amani, hata malengo binafsi ya mtu mmoja mmoja ya Mtanzania mmoja mmoja hayawezi kufikiwa,” amesema.

Waziri Mkuu pia ameeleza mabadiliko ya mazingira ya dunia na changamoto zinazoweza kujitokeza.

“Kuna aina mpya ya mapambano, na mapambano hayo ni ya rasilimali na kila palipo na rasilimali mara nyingi huwa kunavutia maadui na hupenda kupitia migawanyiko ya raia wa nchi hizo husika,” amesema.

Katika hatua nyingine, amepongeza juhudi za Kanisa katika malezi ya watoto na vijana.

“Maandalizi ya watoto hivi si tu manufaa kwa Kanisa, ni manufaa pia kwa Taifa tunalolitaka,” amesema.

Kwa upande wake, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mufindi, Dkt. Anthony Kipangula, ameipongeza Serikali kwa kazi ya kuwahudumia wananchi na kusisitiza kuwa ziara za Waziri Mkuu zimeonesha uongozi unaowagusa wananchi moja kwa moja.

“Nimeona juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuwajali wananchi mtu wa ngazi yako kushuka mpaka kusikiliza kesi ya mwananchi na kumruhusu ajieleze, niliona ni maajabu kabisa,” amesema.

Ameongeza kuwa Kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha maadili mema, kutoa ushauri na kuliombea Taifa ili kudumisha amani na ustawi wa jamii.

02/05/2026

SERIKALI IMESEMA INAONA MATOKEO CHANYA YA KAZI YA SOS KWA VIJANA RIKA BALEHE.

Shirika la SOS Children's Villages Tanzania limeendelea na Utekelezaji wa Programu ya Afya ya Uzazi na Jinsia kwa Vijana hapa Iringa.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Dkt. Linda Salekwa amekiri wazi kwamba kazi ya SOS katika utekelezaji wa afua za Afya ya Uzazi na Jinsia (SRH) chini ya mradi wa Initiatives for Empowering Adolescents (IEA) unaotekelezwa Wilayani humo kwamba ubafanyika kwa ufanisi na unaleta matokeo na unasaidia juhudi za Serikali katika kutatua changamoto za kundi hilo muhimu katika jamii.

Kupitia mradi wa IEA, SOS Children’s Villages Tanzania inaendelea kuimarisha upatikanaji wa taarifa sahihi za SRH, kuhamasisha mabadiliko chanya ya tabia, na kujenga uwezo wa watoa huduma na wadau mbalimbali katika kuhakikisha vijana wanapata huduma rafiki za afya ndani ya jamii.

Address

Iringa
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Makutano Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share