31/03/2022
WAZUNGU NA MAHESABU YA HELA, WAAFRIKA NA UKALI WA VITABUNI
Ukiwa mfanyabiashara, unaambiwa hata uwezo wako wa kufikiria utumie kwenye kufikiria ni kwa namna gani utaweza kuingiza pesa zaidi ya unavyoingiza kipindi hicho. Yeah! Ndiyo maana halisi ya kuwa mfanyabiashara mkubwa.
Jana nilikuwa naangalia muvi ya Death On The Nile. Hii ni sehemu ya pili ya ile muvi iitwayo Murder On Orient Express ambayo niliipenda idea yake ilifanana kwa kiasi fulani na kitabu changu cha Baa Katikati ya Jiji.
Nilichokigundua kwenye maisha ya filamu hasa kwa wenzetu ni namna ya kupiga pesa. Wanapiga sana pesa kupitia waandishi. Yaani mtu anakuja na kukwambia nitungie kitabu kikali cha kipelelezi, anatungiwa halafu akikisoma na kuridhika nacho, anakwambia kiuze sasa, unakiuza, unapata pesa k**a mwandishi halafu naye anakuja kukinunua kwako kwa mamilioni ya pesa, halafu kukifanyia filamu.
Hapo mwandishi umepata faida mara mbili. Moja ni zile kopi milioni moja ulizouza halafu la pili ni pesa kutoka kwa mtu huyo wa kampuni fulani.
Baada ya hapo, muvi ikiwa imefanya poa sana, anakufuata na kukaa tena mezani na kukuuliza k**a unaweza kuandika kingine, kiwe muendelezo wake, ukimwambia sawa, anakwambia andika, ananunua tena na kwenda kutengeneza muvi, inakuwa ni muendelezo.
Hao hawakwambii tuandikie muvi, wanakwambia andika kitabu kwa kuwa mwandishi anapoandika kitabu cha simulizi akili yake hutulia sana kuliko yule ambaye huandika muvi moja kwa moja kupitia script.
Kwa sasa Wazungu wanapenda sana kutengeneza muvi za vitabuni. Unajua kwa nini? Watu wanaumiza sana vichwa kuandika vitabu vya simulizi, wanaweka matukio makubwa na ya kuvutia, si ajabu ukaona mwandishi akatumia mwaka ama miaka miwili kukiandika kitabu ambacho kitakuja kuigizwa muvi kwa muda wa miezi tisa tu.
Kuna watu wanashangaa! Ndiyo! Muvi za wenzetu now zinatengenezwa kwa miezi tisa tu, inakamilika na kubakia kazi ya watu wa kuedit kufanya kazi yao. Dunia imekua sana, sasa hivi hakuna ile kutengeneza muvi kwa miaka minne ama mitano, watu ndani ya miezi kadhaa, muvi imeigizwa, wanakamilisha vitu vidogo kisha mzigo kuachiwa.
K**a unakumbuka, mwaka 2020 mwezi k**a wa tisa ndipo wahusika wakaanza kukusanywa kwenda kuigiza muvi ya Spiderman: Nowhere Home ambapo watu walipiga picha na kusema Andrew Garfield na Tobie Maguire watakuwepo, kwa maana hiyo kungekuwa na Spiderman watatu, na kweli muvi ilivyotoka mwaka 2021 mwishoni, wawili hao walikuwepo.
Vuta picha, tangu walipoanza kushuti na kutolewa, imechukua muda gani? Miezi k**a miwili iliyopita, picha za kwanza za Chris akiwa location zimeonekana akishuti muvi ya Extraction 2, na mwaka huu mwishoni ama mwaka kesho mwanzoni mzigo unatoka.
Hapo nilitaka kukwambia now watu wanaigiza kwa kipindi kifupi si k**a zamani. Muvi k**a Moonlight iliigizwa kwa siku 25 tu. Just imagine, siku 25, watu wamemaliza mzigo, watu wa kuedit wakafanya kazi yao na mzigo kutoka, kubwa zaidi, ikashinda Tuzo kubwa za Oscar mwaka 2017 kipengele cha picha bora.
Ukiachana na hiyo, hata muvi ya Birdman nayo iliigizwa kwa siku 23 japo vyanzo vingine vinasema ilishutiwa kwa miezi miwili tu. Hapa nimewaambia hivi ili mjue kwamba siku hizi muvi zinaigizwa kwa siku chache tu halafu baada ya hapo, editing inachukua miezi kadhaa na mzigo kutoka. Tusiwacheke sana Bongo Muvi.
Okay! Nilikuwa nasema nini vileeeeee!
Ni kwamba waandishi wanakula shavu sana sasa hivi. Muvi nyingi za Wazungu ni za kutoka vitabuni, tena zinakuwa kali kishenzi. Yaani unasoma kitabu, halafu baada ya hapo unaitazama muvi yake. Raha iliyoje!
Jamaa walimfuata mwandishi Agatha Christie na kumwambia aandike kitabu, humo amuweke mpelelezi hatari, amuite kwa jina la Poirot. Agatha akaingia kazini na kuandika kitabu cha Murder On The Orient Express. Muvi ilipoigizwa na kutoka, ikapendwa na hivyo kumpa tena shavu la kuandika muendelezo ambao aliugusia mwishoni kwenye hii, akaandika cha Death On The Nile.
Bado Waafrika tunatumia nguvu kubwa sana kutengeneza muvi kwa watu wasiokuwa na uandishi wa kutosha. Mtu anasema mimi mwandishi, nipeni stori niandike, mnampa, anaandika script moja kwa moja, hiyo muvi haiwezi kuwa nzuri hata kidogo.
Tunasema Bongo hatuna muvi nzuri, ni kwa sababu hawapewi nafasi waandishi husika. Waandishi tuna vitabu vingi, si jambo la kutaka kutungiwa hadithi mpya, leo ukinifuata na kuniambia Nyemo niandikie muvi, nitakwambia chukua Kitabu cha Muuaji Mwenye Tai Nyekundu kakitengenezee muvi.
Au kampuni ya kimataifa ije na kuhitaji niwaandikie muvi, nitawaambia tu chukueni kitabu cha Dili la Dola Bilioni Nne kaiwekeni kwenye muvi. Unapoandika muvi mpya tena kwa kuunganisha kwa script lazima ufeli tu kwa kuwa kuna vingi utakuwa unavipita na akili haitokuwa kwenye utulivu unaotakiwa.
Muvi k**a Harry Potter, vile ni vitabu, na wanasoma mashuleni nchini Uingereza, hizo comic na nyingine nyingi, vyote ni vitabu. Ila kwa Afrika, bado kabisa hatujaanza kuigiza filamu kupitia vitabu vya waandishi.
Wakati nasoma kitabu cha Beka kiitwacho Mzee Beka kile cha kwanza, nilijisemea βHiki kitabu kikiwekwa kwenye muvi, kikapata waigizaji, ni bonge moja la muvi. Kitabadilisha kila kitu.β
Ila hakuna kampuni inayojali kwenye hilo.
K**a kweli Bongo Muvi wakitaka kupiga hatua, ni lazima waanze kuigiza muvi za vitabu vya waandishi wa Kitanzania, kuna vitabu vikali sana, soma kitabu k**a cha Damu ya Mwanamwali cha Ally Katalambula, Ombaomba Aliyeuza Wanaye cha Boniface Ngumije, soma kitabu cha Muuza Mihogo cha Stallone, Mkimbizi cha Hussein Tuwa, Kifo Ni Haki Yangu cha Eric Shigongo, utagundua kuna muvi kali sana kwenye hivyo vitabu, bahati mbaya sana, kampuni za kutengeneza muvi hazijajua hilo.
Majuzi nimeona kitabu cha Vuta Nβkuvute kikitengenezewa filamu, najua na nina uhakika wa 100% itakuwa muvi nzuri sana. Kwa Marekani, kuna mwandishi fulani, dizaini k**a role model wangu anaitwa Nicolas Spark aliyeandika vitabu k**a Notebook, A Walk To Remember, The Vow, The Last Song, Before You na vingine, jamaa vitabu vyake vyote kaviweka kwenye muvi, na muvi zote hizo ni kali.
Leo tunaweza kuwachukulia poa waandishi ila baada ya miaka 30 mbele wakati watoto wetu watakapoona Bongo Muvi inazingua na kusoma vitabu vyetu, watajiuliza why hawakupata nafasi? Kwa nini watu hawa waliachwa, hakutokuwa na nafasi nyingine ya kuwapata kwa kuwa hawatokuwepo, mbaya zaidi kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele, vipaji vinazidi kupungua.
Kwa waandishi hapa kuna mambo mawili ya kufanya. Nitakwambia ila jua kwamba duniani kuna waigizaji wengiiii ila waandishi wachache. Hivyo, ili utoke na vitabu vyako vionekane kwa televisheni, cha kwanza fanya juu chini uonane na kampuni za kutengeneza muvi na kupeleka mawazo yako, ukishindwa kabisa, kuwa k**a Tyler Perry. Yaani tafuta pesa na utengeneze kampuni yako ya filamu.
Siku Filamu ya Baa Katikati ya Jiji itakapokaribia kutoka, nitawajuza, nadhani itakuwa mwaka huu ama mwaka kesho mapema.
Mnisamehe kwa kuandika sana! Hope haijawachosha kusoma.