Karatu Online TV

Karatu Online TV The Official
We shoot • We edit • We Publish • Documentary Karatu Tv

07/09/2026

TAARIFA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi akitangaza taarifa ya kifo cha Mhe. Hafidh Ameir Hassan ambaye ni mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani

04/09/2026

DC DKT. LAMECK KARANGA ATOA TAHADHARI KWA WANANCHI KUJIANDAA NA MVUA KUBWA
Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Dkt. Lameck Karanga, ametoa tahadhari kwa wananchi kuhusu uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba hadi Januari.
Dkt. Karanga ametoa tahadhari hiyo leo, Septemba 4, 2026, wakati akizungumza na watendaji wa kata na vijiji kuhusu umuhimu wa kujiandaa na kujipanga kimkakati kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
Aidha, Mhe. Dkt. Lameck Karanga amewataka watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wanawafikishia wananchi elimu na taarifa muhimu kuhusu namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya maafa yanayoweza kusababishwa na mvua kubwa.
Amesisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema ili kupunguza madhara kwa wananchi, mali na miundombinu

04/09/2026
DC KARATU ATOA WITO KWA WANANCHI KUTUMIA NYARAKA HALALI KUPATA VITAMBULISHO VYA NIDA Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Dkt....
02/09/2026

DC KARATU ATOA WITO KWA WANANCHI KUTUMIA NYARAKA HALALI KUPATA VITAMBULISHO VYA NIDA Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mhe. Dkt. Lameck Karanga,Septemba 1, 2026, amejionea zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa wananchi wa Kijiji cha Qaru, Tarafa ya Endabash, Wilaya ya Karatu. Akiwa katika kituo cha uandikishaji, Mhe. Dkt. Karanga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na uongozi wa NIDA kwa kuwezesha watumishi kuwafikia wananchi vijijini na kutoa huduma hiyo bila malipo. Aidha, Mhe. Dkt. Karanga amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia nyaraka halali na sahihi wakati wa kuwasilisha taarifa zao, hatua ambayo itasaidia kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza katika usajili na utoaji wa vitambulisho pamoja na namba za NIDA. Zoezi hilo limefanyika katika Kijiji cha Qaru kwa takribani siku mbili, huku leo, Septemba 1, likiwa siku ya hitimisho. Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Qaru, timu ya NIDA inatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika maeneo mengine yenye changamoto, hususan kuwafikia wananchi ambao bado hawana namba au Vitambulisho vya Taifa.

30/08/2026

MAKAMU WA RAIS MTEULE WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

10/07/2026

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo Alhamisi, Julai 09, 2026 amemuapisha Kamishna Mteule wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Massana G. Mwishawa kuwa Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA. Hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TANAPA jijini, Arusha.

10/07/2026

MWENGE WA UHURU WAWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI YA KIJIJI CHANGARAWE🇹🇿

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 Wazo Michael Mwang'onda amezweka Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa ofisi ya kijiji Changarawe Kata ya Daa wilaya ya Karatu, mradi wenye thamani ya shilingi milioni 78, 82, kiasi hicho cha fedha shilingi milioni 58.82 ni fedha za mchango wa wananchiw a kijiji cha Changarawe na milioni 20 ni mchango wa Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Changarawe Mhe.Israel Niima Kwaang amesema kuwa, kwa takribani miaka 50 kijiji hicho hakikuwa na ofisi yake, awali walitumia jengo la Chama cha Mapinduzi na baadaye kuhamia jengo la ofisi ya Afisa Kilimo ndipo walipoona kuna umuhimu wa kuwa na ofisi ya kijiji ndipo walipoamua kuanza ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo.

Ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia wannachi hao kuongeza fedha za kuendeleza ujenzi wa jengo hilo, mraci ambao Mwenge wa Uhuru umeweza kuweka Jiwe la Msingi, hali inayodhibitisha namna Serikali inathamini michango ya wananchi kwenye shughuli za maendeleo

10/07/2026

MRADI WA MAJI KAMBI YA SIMBA WAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU 2026🇹🇿

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 Wazo Michael Mwang'onda amezindua Mradi wa Maji Kambi ya Simba kata ya Mbulumbulu, mradi uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 212, milioni 122 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mfukowa Maji na shilingi milioni 90 fedha za Halmashauri ya wilaya ya Karatu.

10/07/2026

MWENGE WA UHURU 2026 WAWASILI WILAYA YA KARATU

*Miradi 8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.97 kupitiwa na Mwenge wa Uhuru 2026*

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Dkt.Lameck Ng'ang'a amepokea Mwenge wa Uhuru 2026 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Brg Jenerali Wilson Sakuro, kwenye eneo la Njia panda ya Mang'ola asubuhi ya leo Julai 07, 2026.

Akipokea Mwenge wa Uhuru Dkt.Ng'ang'a amesema kuwa, ukiwa wilayani himo Mwenge wa Uhuru 2026, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Km 118.7 na utatembelea jumla ya miradi 8 yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.97 katika sekta za Elimu, Afya, Mazingira, Uwezeshaji wananchi kiuchumi, miundombinu ya maji, Barabara na michezo Pamoja na mradi wa uwekezaji.

Mhe. Dkt. Ng'ang'a amebainisha kuwa, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuri 2026 ndugu Wazo Michael Ng'onda ataweka Mawe ya Msingi ujenzi wa ofisi ya kijiji Changarawe Kata ya Daa mradi wenye thamani ya shilingi milioni 78, 8weka, mradi wa Uwekezaji binafsi huduma za kijamii, Ujenzi wa Hoteli ya Chui Hidden lodge kata ya Marera- Rhotia mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 1.5 pamoja na Ujenzi wa wodi ya watoto na jengo la upasuaji wanawake na njia (walkway), Hosipitali ya wilaya Karatu mradi wenye thamani ya shilingi milioni 800 fedha kutoka Serikali.

Aidha Mwenge wa Uhuru utaKutembelea mradi wa matumizi ya Nishati safi na salama ya kupikia shule ya Sekondari ya Wavulana Karatu, wenye thamani ya shilingi milioni 35., kutembelea Mradi wa uwekezaji wa wananchi kiuchumi Kikundi cha Vijana wa Jeshi la Akiba kinachojishughulisha na kuosha magari (carwash), mradi unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 40.

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru 2026, utazindua miradi 3, ikiwemo mradi wa Ujenzi wa bweni la wavulana Shule ya Sekondari Awet kata ya Mbulumbulu wenye thamani ya shilingi 174.4, Mradi wa Maji Kambi ya Simba kata ya Mbulumbulu uliogharimu kiasi cha shilingi Milioni 212 pamoja na ujenzi wa Barabara/Madaraja ya kudumu Daraja la Slahhamo -Manyara Lositete kata ya Mbulumbulu mradi wenye thamani ya shilingi milioni 137 fedha kutoka serikali kuu kupitia Mfuko wa Barabara

TICO KARATU
28/06/2026

TICO KARATU

Address

Karatu

Opening Hours

Monday 09:00 - 16:00
Tuesday 09:00 - 16:00
Wednesday 09:00 - 16:00
Thursday 09:00 - 16:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 12:00
Sunday 09:00 - 12:00

Telephone

+255673941419

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Karatu Online TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Karatu Online TV:

Shortcuts

Share