The Green Voice TV

The Green Voice  TV Karibu The Green Voice TV, usisahau ku "Subscribe" You tube channel yetu. "Yes we are Green".

04/09/2026

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na msako dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya mfanyabiashara Vaileth Libaba (34), aliyeuawa baada ya kuvamiwa na kuporwa fedha na simu. Katika msako huo Septemba 3, 2026 huko Ituha Relini, watuhumiwa wawili, Venance Yasin maarufu Mnyaki na Atupele Kabale, walijeruhiwa kwa risasi baada ya mmoja kutishia kumpiga polisi kwa bastola iliyotengenezwa kienyeji na mwingine kumpiga askari kwa rungu; wote wawili walifariki wakiwa hospitalini. Polisi walik**ata pia kisu, panga, mizula miwili na bastola hiyo, huku watuhumiwa wengine watatu wakiendelea kushikiliwa kwa mahojiano.

04/09/2026

SIO KWA UBAYA Page ya inawatu milioni 50 page ya inawatu milioni 3.7 page ya inawatu milioni 5.1 Njoo na HOJA

03/09/2026

🔥 YANGA SC: JEZI KALI, LAKINI UZINDUZI WENYE MASWALI!
Yanga SC wamekuja na jezi za Ligi ya Mabingwa Afrika zenye mwonekano wa kiwango cha kimataifa, tena wameamua kumtumia Fabrizio Romano kuzitambulisha—hapa kweli wamecheza na branding ya dunia. Lakini sasa ndipo swali linapoanzia: umezindua jezi ya kimataifa kwenye nchi ambayo hata soko la mashabiki wa Yanga ni la mashaka! K**a lengo ni kuuza na kuifanya jezi iwe bidhaa ya kimataifa, kwa nini uzinduzi usifanyike sehemu ambayo kuna mashabiki na wanunuzi wanaoweza kuingia sokoni mara moja?
Na kilichochekesha zaidi ni kwamba, mara tu baada ya kuionesha kwa mbwembwe zote za kimataifa, mtangazaji anaivua na kuiweka tena kwenye begi! 😂 Yaani jezi imefika kimataifa kwa sekunde chache, halafu imerudi kwenye begi kabla hata haijaanza maisha yake sokoni. Yanga, jezi imependeza—lakini safari ya kutoka kwenye begi mpaka kwa mwananchi mfukoni ndiyo sasa tunaisubiri! 😅💚💛

02/09/2026

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LATOA WITO KUSALIMISHA SILAHA HARAMU

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawakumbusha wananchi kushiriki katika kampeni ya kusalimisha silaha haramu kwa hiari, iliyoanza tarehe 1 Septemba hadi 31 Oktoba 2026, kufuatia uzinduzi rasmi uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Paschal Katambi Patrobas (MB), Agosti 31, 2026.

Wananchi wenye silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria, silaha za marehemu ambazo hazijasalimishwa, silaha halali zinazotumika kufanya uhalifu pamoja na silaha zinazotengenezwa kienyeji, wanahimizwa kuzisalimisha kwa hiari katika vituo vya Polisi au Ofisi za Serikali zilizo karibu nao.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wananchi kutumia fursa hii kwa ajili ya usalama wao na jamii kwa ujumla.

02/09/2026

Ujumbe wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Jumanne Sagini baada ua kula kiapo cha Ukuu wa Mkoa.

01/09/2026

SIMBA WAMEANZA KUOGOPA MAPEMA! 😅🔥

Mashabiki wa Simba wameanza kukata tamaa kabla hata mambo hayajawa magumu, wengine wakisema wazi kabisa “tunaweza kufungwa hata 7 bila!” 😂 Hii ni dalili gani k**a si hofu ya Yanga SC? Ukweli ni kwamba baadhi yao hawaamini kabisa kikosi chao, wanaona Yanga ina kasi, ubora na kujiamini zaidi kiasi cha kuwafanya waanze kuhesabu mabao kabla mpira haujapigwa! 🟢🟡 Wana Simba, hii ni presha au tayari mmeanza kutafuta sababu za kushindwa? 😅🔥
Kenny Lawrence Sibonike NM Mvellah Elia Elly Sibonike Vance Evance Simba SC Tanzania

Na Jackline Minja, WMJJWMM DodomaSerikali imeeleza kuwa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuwapatia wanawake m...
01/09/2026

Na Jackline Minja, WMJJWMM Dodoma

Serikali imeeleza kuwa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya kuwapatia wanawake mafunzo ya ufundi stadi kwa lengo la kuwawezesha kuibua fursa za kibiashara, kujiajiri na kuongeza kipato.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, wakati akijibu swali la Mhe. Fatma Ally Rembo, Mbunge wa Viti Maalum, lililouliza kuhusu mpango wa Serikali wa kuwapatia wanawake mafunzo ya ufundi stadi ili kuwawezesha kuibua fursa za kibiashara.

Naibu Waziri Mahundi amesema Serikali kupitia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kisekta inaendelea kutoa fursa za mafunzo ya ufundi stadi kwa wanawake ili kuwawezesha kupata ujuzi unaoweza kuwasaidia katika shughuli za kiuchumi, ambapo miongoni mwa hatua zinazotekelezwa ni kupitia Mradi wa Uwezeshaji kupitia ujuzi unaolenga wasichana wenye umri wa miaka 18 hadi 35, ambapo hadi Juni 2026 jumla ya wasichana 1,051 walikuwa wamefikiwa na mradi huo.

Aidha, amesema kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Serikali inaendelea kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanawake katika fani mbalimbali, ikiwemo ushonaji, utengenezaji wa bidhaa pamoja na matumizi ya teknolojia.

Aidha amesema Serikali inaendelea kutekeleza Programu ya Utambuzi na Urasimishaji Ujuzi, inayolenga kutambua na kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na hadi Juni 2026, jumla ya vijana 14,400, sawa na asilimia 18 ya lengo, kutoka mikoa 11 walikuwa wamesajiliwa katika programu hiyo inayolenga kuwafikia vijana 80,000 ifikapo Juni 2027.

Sambamba na hayo, amesema Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na Vyuo vya Ufundi vya Mabughai na Misungwi vinaendelea kutoa mafunzo katika fani za uhandisi wa ujenzi na maendeleo ya jamii, ambapo katika mwaka wa masomo 2025/26 jumla ya wanachuo 1,087 walihitimu mafunzo katika vyuo hivyo, ambapo wasichana walikuwa 496, sawa na asilimia 46.

01/09/2026

Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Ibrahim Doumbia hana uwezo. Kwa mtazamo wangu, tatizo si uwezo wa Doumbia, bali ni namna Simba SC inavyomtumia. Mshambuliaji anahitaji mfumo unaompa nafasi, mipira sahihi na muda wa kuzoea wenzake. Wachezaji wangepewa hata video zake akiwa Mali, waone alikuwa akifungaje na ni aina gani ya mipira aliyokuwa akipokea, ili wajue namna bora ya kumtumia. Doumbia akipata huduma sahihi na kuelewana na wenzake, naamini mabao yake yatakuja.

01/09/2026

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari kwa wananchi na wadau kujiandaa na uwezekano wa kuwapo kwa vipindi vya mvua kubwa kuelekea miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba, huku ikisisitiza umuhimu wa maandalizi ya mapema katika kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini, Dkt Ladislaus Chang'a ameyasema hayo wakati akitoa utabiri wa kuelekea katika kipindi cha Mvua za Vuli zinazotarajiwa kuanza Septemba mwaka huu hadi wiki ya kwanza ya Oktoba. Dkt Chang'a amesema wananchi na mamlaka za Serikali zinatakiwa kuchukua taadhali kutokana na ongezeko la vipindi vya mvua linaweza kuambatana na matukio ya mvua kubwa na uwepo wa hatari za mafuriko katika baadhi ya mikoa nchini. Amewasii wakulima nchini kutumia utabiri huo kupanga shughuli zao za kilimo, ikiwamo kuchagua aina na muda sahihi wa kupanda, pamoja na kutumia teknolojia zinazosaidia kuhifadhi na kudhibiti matumizi ya maji mashambani. Aidha, amesema maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, ikiwamo mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara, inatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani ambapo mvua hizo zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya Septemba na wiki ya kwanza ya Oktoba.

Na Jackline Minja, DodomaSerikali imeendelea kuimarisha hatua za kulinda watoto dhidi ya ukatili, unyanyasaji, unyonyaji...
31/08/2026

Na Jackline Minja, Dodoma

Serikali imeendelea kuimarisha hatua za kulinda watoto dhidi ya ukatili, unyanyasaji, unyonyaji na madhara mengine yanayotokana na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akijibu swali la Mhe. Lucy Simirya Kombani (Viti Maalum), kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya ukatili mtandaoni.

Naibu Waziri Mahundi amesema miongoni mwa hatua zinazotekelezwa ni Kampeni ya Kitaifa ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni, ambayo imefanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kwa lengo la kutoa elimu kwa watoto, wazazi, walezi na jamii kuhusu matumizi salama na yanayolinda haki za watoto mtandaoni.

“Jumla ya watoto 1,811,212 wamefikiwa na elimu kuhusu usalama wa mtoto mtandaoni aidha, kampeni hiyo imehusisha wawezeshaji 516 kutoka ngazi za mikoa, wakiwemo Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Elimu, Dawati la Polisi la Jinsia na Watoto pamoja na SMAUJATA” amesema Mahundi.

Ameongeza kwamba Serikali imeunda K**ati ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu Ulinzi na Usalama wa Mtoto Mtandaoni, yenye jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu na kusaidia Serikali kuweka mikakati na afua madhubuti za kuzuia na kukabiliana na vitendo vya ukatili pamoja na madhara yanayoweza kuwakabili watoto wanapotumia mifumo ya kidijitali.

Vilevile, Serikali imefanya maboresho ya Sheria ya Mtoto Sura ya 13, ambapo kifungu kinachohusiana na makosa ya kimtandao kimefanyiwa marekebisho ili kuweka masharti yanayohusiana na makosa ya unyanyasaji na utumikishaji wa kingono kwa watoto kwa kutumia nyenzo za TEHAMA, hatua inayolenga kuwalinda watoto dhidi ya uhalifu wa kingono mtandaoni.

Aidha, Serikali imeeleza kuwa matumizi yasiyo salama ya mitandao yanaweza kusababisha madhara mbalimbali kwa watoto, ikiwemo kuathirika kisaikolojia kutokana na kuangalia maudhui yasiyoendana na umri wao, uraibu unaotokana na kutumia muda mwingi mtandaoni pamoja na mmomonyoko wa maadili unaoweza kusababishwa na kuiga mila na desturi za mataifa mengine hivyo wazazi na walezi wahakikishe wanafuatilia mienendo ya watoto wao pindi wanapowanunulia vifaa hivyo vya teknolojia.

Katika kuhakikisha ulinzi wa mtoto unaanzia ndani ya familia, Serikali imewataka wazazi na walezi kujenga mahusiano mazuri na watoto kuhusu matumizi ya TEHAMA, kuwa karibu nao wanapotumia mitandao na kufuatilia shughuli zao mtandaoni, ikiwemo kutumia mifumo ya Parental Control.

Wazazi na walezi wanapaswa kufundisha watoto kufikiria kwa makini kabla ya kutuma picha, video au ujumbe wowote mtandaoni, kwa kuwa taarifa iliyowekwa mtandaoni inaweza kuwa vigumu kuiondoa kabisa, Pia niwamehimize watoto kuzungumza na watu wanaowaamini pindi wanapoona dalili au kufanyiwa vitendo vya ukatili mtandaoni.

Address

Rungwe
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when The Green Voice TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share