17/05/2025
Kutoka kwenye ukurasa wa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan
Miundombinu yetu,
Treni yetu,
Fahari yetu.
Leo nimesafiri kwa treni ya SGR toka Dar es Salaam kwenda Dodoma. Hakika Watanzania tunayo kila sababu ya kujivunia hatua kubwa tunazoendelea kupiga k**a Taifa.
Nikiwa Dodoma pamoja na kazi nyingine, nitaboresha taarifa zangu katika Daftari la Kudumu la Mpigakura katika Ofisi ya Kijiji, Chamwino. Ninawasihi wananchi wenzangu tuendelee kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zetu, ili tutumie haki yetu ya kikatiba ya kushiriki Uchaguzi Mkuu, Oktoba mwaka huu.