27/05/2016
Umwagiliaji
Umwagiliaji wa njia ya matone; kwa wakulima wadogo kuna mbinu rahisi za kutumia mipira iliyotobolewa
Milango k**a hii inatawala ugawaji wa maji katika mifereji ya umwagiliaji
Vinyunyizo vikubwa vinatupa maji mashambani
Umwagiliaji katika Sahara (Misri) kwa macho ya ndege: kila duara ina kipenyo cha kilomita moja
Umwagiliaji wa pamba kwa njia ya kinyunyizo kikubwa kinachozunguka nchani
Umwagiliaji ni mtindo wa kilimo wa kupeleka maji kwa mimea shambani pasipo na mvua ya kutosha.
Hutumiwa katika maeneo yabisi au wakati mvua ni kidogo. Katika nchi baridi unatumiwa pia kwa kusudi la kulinda mazao dhidi ya jalidi.
Ni kilimo ambacho kinasaidia sana, kwa mfano nchi ya Misri tangu zamani inategemea mto Naili katika shughuli zake za umwagiliaji wa mazao.
Chanzo cha maji
Umwagiliaji hutumia maji kutoka vyanzo mbalimbali:
maji hutolewa kutoka mtoni au ziwani
mwendo wa mto huzuiliwa kwa lambo na maji kutolewa katika ziwa ya lambo
pampu yavuta maji kutoka kisima
Mbinu za umwagiliaji
Kuna mbinu nyingi za kumwagilia mazao. Tangu kale watu walichimba mifereji wa kupeleka maji mashambani. Mashamba yazungukwa kwa ukuta mdogo wa udongo na eneo la shamba lajazwa maji. Kujazwa kwa shamba kunarudiwa hadi mazao kwa mfano ngano yamekua. Mazao mengine k**a mpunga hukuzwa mara nyingi ndani ya maji yanayofunika shamba kwa miezi kadhaa. Mtindo huu uneandelea kutumiwa hasa katika nchi nyingi za Asia na sehemu kubwa ya mchele duniani inapatikana kwa njia hii.
Mitambo k**a pampu imewezesha wakulima kuachana na mifereji na kazi ya kugawa maji. Vinyunyizo vinamwaga maji kwa mashamba. Kuna mashine kubwa zenya matairi zinazozunguka kwenye ncha na kumwagilia duara. Mengine yanazungushwa kwa nguvu ya maji na kutupa maji hadi umbali wa mita 500.
Katika nchi penye uhaba wa maji kuna mbinu mpya wa umwagiliaji wa matone; mabomba au mipira yenye mashimo madogo yanapelekwa shambani. Mimea inapandwa karibu na shimo la mpira. Wakati wa usiku pasipo na joto kali maji inatoka tone kwa tone kwenye bomba au mpira hivyo yanafika moja kwa moja kwenye mizizi. Mbinu huu unatumia maji kidogo kulingana na umwagiliaji wa kawaida. Nchi ya Israeli imetangulia kulima mashamba makubwa kwa njia hii.
Matatizo
Umwagiliaji huongeza mavuno kiasi kikubwa. Lakini kuongezeka kwa umwagiliaji duniani kumeleta matatizo mengi.
Matumizi ya maji yanazidi akiba yake; mito imekauka kwa sababu watu wengi mno wamechukua maji mle. Mfano mbaya sana ni ziwa Aral iligeuzwa kuwa jangwa kwa sababu maji ya mito yake yametumiwa kwa miradi mikubwa ya pamba katika mazingira ya joto kali tena kwa teknolojia isiyofaa k**a mifereji iliyo wazi
Maji mengi yanapotea hasa pale ambako maji hupitishwa kwenye mifereji au na kujaza shamba kumwagiliwa kwa vinyunyizo. Sehemu kubwa inapotea kwa njia ya uvukizaji kuliko kulisha zao.
Pampu zimesababisha kushuka kwa uwiano wa maji chini ya ardhi. Hi ni hofu kubwa kwa umwagiliaji katika jangwa Sahara unaotumia akiba ya maji iliyojengwa na mvua wa milenia nyingi lakini inayopungua haraka tangu kuanzishwa kwa miradi ya umwagiliaji kwa pampu kubwa zinazovuta maji ya chini.
uharibifu wa mashamba ka kuongeza kiwango cha chumvi ardhini; katika mazingira ya joto uvukizaji wa maji unapeleka chumvi iliyoko ardhini juu; maji yavukiza lakini chumvi inabaki. Kuna mifano mingi ambako mashamba yameshaharibika kutokana na kuongezeka kwa chumvi. Maeneo yaliyolisha watu tangu kale yamekuwa jangwa kabisa.
Matatizo haya yote yanaonyesha ya kwamba haitoshi kumwagilia mashamba tu na kufurahia mazao mazuri kwa sababu matatizo yataongezeka baada ya miaka kadhaa. Kwa hiyo ni lazima kuangalia vema mbinu za uimwagiliaji inayolingana na mazingira na kutumia maji kidogo k**a vile umwagiliaji wa matone.