02/06/2025
FEISAL SALUM ni kweli anahitajika na timu kadhaa ikiwemo Simba, Kaizer Chiefs na Young Africans, Mchezaji huyo ili ununue mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia unapaswa kulipa dola 500,000 kwa Azam FC ambayo haina tabu kufanya biashara ikiwa ni sawa na Billion 1.3 za Kitanzania.
Bado mkataba wa Feisal Salum ni kuwa endapo Azam watamuuza nje ya nchi basi Yanga anakula 25% ya mauzo na k**a atauzwa ndani basi Yanga anapaswa kupewa BILLION MOJA.
UHALISIA ni kuwa Simba ya Msimbazi ndio mpaka sasa ina nafasi kubwa zaidi ya kumnasa Mwanandinga huyo kutoka Visiwani ambapo wapo tayari kumpa Mshahara wa Million 50, nyumba Masaki na Usafiri, huku bonus mbalimbali pia watakuwa wanamlipa, Kambi ya Mchezaji na Mchezaji wamevutiwa zaidi na ofa ya Simba.
Kwa mujibu wa vyanzo vyangu ni kuwa Yanga walipeleka ofa yao ambayo Simba wameenda juu zaidi na inadaiwa Wananchi hawapo tayari kupanda juu ya hapo, lakini utata unasalia kuwa Simba watatumia pesa nyingi kumlipa Feisal halafu bado wana kipengele kwa Azam cha Billion 1.5 za Kumnunua, huku Azam nao wanapaswa kuwapa Yanga Billion moja, utata pekee upo hapo, fuatilia vyema cinema hii nyingine vizuri.
Ila hisia, mawazo na kila kitu cha Feisal kwa mujibu wa taarifa, zaidi ya 80% ni kucheza Simba msimu ujao."