28/04/2023
Baada ya kupitia CHANGAMOTO nyingi katika kuelekea ndoto yake ya kuwasaidia wananchi wenzake wa Afrika Kusini,
Baada ya kukutana na VIKWAZO vikubwa kuelekea SHAUKU yake ya kuwa RAIS wa NCHI yake,
Baada ya kufungwa kwa Miaka 27 na kila mtu akidhania kuwa amefika mwisho,
Nelson MANDELA akafanikiwa kuwa Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini.
Ndipo aliposema “The greatest GLORY in living lies not in NEVER FAILING, but in RISING everytime we FAIL”
Akimaanisha, utukufu mkubwa(Mafanikio makubwa) kwenye maisha, hayatokani na wewe KUTOKUSHINDWA bali hutokea pale ambapo UNAINUKA kila wakati BAADA YA KUFELI.
Chochote ambacho kinaonekana KIMEKUSHUSHA CHINI, tukio lolote ambalo linaonekana UMEFELI,
Usisahau kuwa huo ni MTAJI wa KUKUPA ushindi MKUBWA mbele yako. Amua kuinuka, kujipanga tena na KUSONGA mbele.
Usisahau hili, “It’s not over, until it’s over”. Haijaisha hadi imefika mwisho.
Ukimaliza Kuisoma, nisaidie kuishare tafadhali.
See You At The Top